News Alert: Polisi Wanene kukatwa mishahara, kufukuzwa kazi

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Imebainika kuwa sehemu 2/3 ya Polisi wa London ni wanene kupindukia.
Ili kuhakikisha ufanisi kazini, watalazimika kufanyiwa majaribio kila mwaka na ambaye hakukidhi kiwango cha unene kinachokubalika, atakatwa mshahara wa paundi 2,922 kwa mwaka (sawa na Tzs zaidi ya milioni 7) au kufukuzwa kabisa ikiwa ataendeleza nyam nyam.

Mimi nilidhani ni baadhi ya trafiki wetu wa Tanzania tu, kumbe hata majuu nako vitambi miongoni mwa polisi ni kitu cha kawaida. Kwa nini wanakuwa wanene kiasi hiki? Tanzania ina mpango gani wa kuwapiga landa kidogo?
 
Wa huku hata wembamba hawana lolote kazi kulewa viroba asubuhi asubuhi na kuvuta misigara,huo ufanisi utatokea wapi sasa..
 
wawatoe kabisa......mtu una majukumu ya kutunza usalama wa raia na mali zao.....unakuwa mnene kama kitumbua cha unga wa ngano.....ikitokea kashkashi hawawezi....wanabaki kuhema kama nini sijui....wanaudhi sana......
 
Teh waje na huku Tz wawale vichwa....
Hahaha, huku watawamaliza.

Wa huku hata wembamba hawana lolote kazi kulewa viroba asubuhi asubuhi na kuvuta misigara,huo ufanisi utatokea wapi sasa..
Ni kweli Mkuu! Angalau kwa wenzetu tunaweza kuchukulia unene kuwa ni sehemu ya utendaji mbovu, lakini hapa ni rushwa kwenda mbele ili wapate hizo pesa za viroba na misigara.

wawatoe kabisa......mtu una majukumu ya kutunza usalama wa raia na mali zao.....unakuwa mnene kama kitumbua cha unga wa ngano.....ikitokea kashkashi hawawezi....wanabaki kuhema kama nini sijui....wanaudhi sana......
Na halafu hawa wa petu, pamoja na unene kama hivyo vitumbua, wanakuwa waoga kupindukia, na ndio maana mara nyingi wanatembea wawili wawili ili angalau mmoja apige filimbi mwenzake anapopewa kisago.
 
Back
Top Bottom