News Alert - Mashamba ya Ballali yavamiwa

...hao Watu Wa Bagamoyo Waache Uchuro..wametumwa Na Mtu Kuvamia Hayo Mashamba Ili Iwe Propagamnda???? Polisi Wako Wapi..mbona Kuna Mashamba Ya Wakuu Fulani Walivamia ..juzi Tu Amri Ikatoka Ikulu Kuwa Waondolewe???..tena Chini Ya Usimamizi Wa Mkuu Wa Mkoa Christine Ishengoma..tena Mashamba Yenyewe Jana Yake Walikuwa Wameruhusiwa Kuyalima Na Waziri Wa Ardhi Baada Ya Wananchi Kulalamika Kuwa Viongozi Wenye Mashamba Hayo Wameyafanya Msitu ..na Yanahatarisha Maisha Yao Kwa Chatu....na Hawayaendelezi Wanahodhi Tu..waziri Aliwaruhusu Kulima Lakini Akawaambia Wasijenge Hadi Rais Atakapotengua Hati Na Kugawiwa Upya....matokeo Yake Amri Ilkitoka Ikulu Na Mkuu Wa Mkoa Akamkandia Waziri Kwa Wananchi Kwa Jeuri....wakawartoa Wananchi Na Kuchoma Moto Maandalizi Yao Yoote...

Sasa Inakuwaje Haya Ya Balali Polisi Wakae Kimya Wakati Wana Jukumu La Kulinda Usalama Wa Raia Na Mali Zao...si Halali Hata Kidogo!!!!..hawa W3ananchi Wanatumika Kipropaganda Na Mafisasadi!!!
 
Mgomo wa ombaomba...? Naona jamaa wameshachoka kuomba sasa na wenyewe wameamua kuchukua kilicho chao.Mzee PM huko kwenye mashamba ndipo walipoamua kuanzia, siku si nyingi tutawakuta Msasani, Masaki na Mbezi beach wakijigawia majumba.
 
..hilo Shamba La Bunju Lilikuwa Na Ugomvi Wa Mipaka Kati Ya Balali Na Peter Bakilana...na Warioba Ndio Aliyefanya Arbitration..nadhani Bado Haijaisha...kuna Uwezekano Mkubwa Watu Kutumiwa Kuchukua Sheria Mkononi Nasisitiza!!!!...nchi Hii Inaongozwa Kwa Sheria ...huyu Mtu Anatolewa Kafara ..na Wananchi Wa Kawaida Hawajui Chochote Zaidi Ya Neno Moja Tu....balali Mwizi!!!
 
Ingawa ni kweli, bado siamini kama Watanzania tumefikia hatua hii ya kuvamia mali za watuhumiwa, naona sasa watuhumiwa mafisadi wataanza kurushiwa mawe mara wapitapo njiani na magari yao.
Tuwe macho, tunakoeleka siko!
 
Idimi,
Hata mimi sikuamini kuwa siku itafika Wakenya watashambuliana kwa misingi ya kikabila licha ya kwamba wameishi majirani miaka mingi na licha ya kwamba nao walisaidia kuwatunza wakimbizi kutoka Rwanda. Lakini yametokea. Tusipoziba ufa tutalazimika kujenga ukuta.
 
Lunyungu hii ni kweli kabisa, unajua kuna mambo mengine yanasikitisha sana. Angalia issue ya Prof Mahalu, Brother Ditto, Karamagi na Buzwagi, Richmond, ni kama zinaelea elea tu, na ni kama zinataka kuwekwa kapuni. I am starting to belive that hii ya Balali inatumika kama issue ya ku cover up yote. aanza kuelewa polepole ni kwanini Balali alikataliwa kujiuzulu au kujiuzulu kwake kulikuwa kunafichwa, naona kama lengo lilikuwa ni kumtangaza kuwa amefukuzwa ili story yake ifunike mengine yote!!
Hizo issue nyingine tukizisahahu kweli tutakuwa wa ajabu sana. I wonder tunakwenda wapi!

Bongolander, nikweli kuwa saa nyingine scandal fulani inaibuliwa ili kuzima scandal nyingine. Lakini sidhani kwa mwamko wako na wangu tutayaacha haya mambo yapotelee kapuni. Kila leo hii tutayaibua na kuyaongelea... hata hapa JF, kuna siku tutawaomba ma mods na Invisible waziweke hoja ambazo hazijapata suluhisho na zinahitaji uchambuzi zaidi mstari wa mbele kwenye majukwaa.

Kwa hivi sasa, Ballali na BoT is hot news, watu wanapata pesa kwa kuuza magazeti na vipindi vya Tv, kila tukio lina wakati wake na uzito wake. Hivyo hilo soo lililozuka kwenye shamba, kama ni la 'kupikika' kwa nia kama hiyo unayosema, bado halitanyamazisha madukuduku yetu katika maswala mbalimbali. Simply, It won't wash! Hayo makashfa mengine ninamatumaini makubwa yataendelea kuongelewa. Na kama unavyojua, JF ikiongelea kitu,vyombo vya habari hapa nyumbani navyo hufata.

SteveD.
 
Ni kweli kwamba mambo uvamizi huu si halali kisheria, lakinik mimi nimefurahishwa na kitu kimoja kwamba wananchi wansema gavana amechukua fedha za nyingi sana, tofauti na diwani (I guess ni wa CCM). Yeye alisema kwamba "huu ni ugomvi kati ya serikali na Balali sasa nyie wananchi inawahusu nini?". Na hayo yanayoitwa mashamba hamna kitu mle hata kibanda cha mlinzi nadhani thamani yake haifiki kilo!!!!!
 
Mimi nilikuwa maeneo ya tukio siku ile ya Jumamosi, kuna kitu ambacho waandishi wa habari wala TV station hakiolezesha kwenye habari zao, wananchi hao wanaojiita wenye hasira walianza kuvamia MIFUGO kwanza ya mh. Balali na kuuza yote, mifugo hiyo ni NG'OMBE PAMOJA NA MBUZI walipomaliza zoezi hiyo sasa ndio wakaanza kugawana mashamba ya balali kwa kila mtu alipewa miguu 20 x 20.

Mafisadi wameamua kumtoa kafara fisadi mwenzao hatimaye joto ya jiwe anaipata peke yake. Wakati mijihela wamekula watu kibao.

Mimi nasubiri siku ambayo wananchi wataenda kugawana mali za MKAPA, na mimi lazima niende nikapate chochote kitu.
 
Tunawasaka waliovamiashamba la Balali - Polisi

2008-01-21 08:43:58
Na Khalfan Said


Polisi mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, wanamsaka mtuhumiwa na washirika wake walioandaa mpango wa kuvamia shamba la gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Daudi Balali lililoko Mbweni-Maputo, nje kidogo ya Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Bw. Jamal Rwambow, alisema polisi imeanzisha msako wa kumtafuta aliyepanga mpango huo na washirika wake ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la kuvamia eneo lisilo lao.

Kamanda alisema imethibitika kuwa ardhi waliyovamia iliyoko kijiji cha Maputo ni mali ya Dk. Balali.

``Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio la uvamizi wa ardhi ya gavana wa zamani wa BoT,`` alisema.

Wavamizi hao walijitosa ndani ya shamba la Dk. Balali mwishoni mwa wiki na kujigawia wakidai kuwa alipata mali hizo kidhalimu wakihusisha madai ya ubadhirifu wa Sh. bilioni 133 ndani ya Benki Kuu zilizolipwa kwa makampuni yasiyokuwa na stahili.

Kamanda Rwambow alisema taarifa za kuvamiwa zilifikishwa kwake na diwani mmoja aliyemtaja kwa jina la Mbonde
``Niliarifiwa na diwani Mbonde kuwa kundi la watu wanafanya uvamizi kwenye ardhi ya Balali na nilipotuma vijana wangu wale watu walitawanyika,`` alisema Kamanda Rwambow.

Alisisitiza kuwa polisi haina mpango wa kuweka ulinzi kwenye eneo hilo na jambo linaloweza kufanyika ni kuwasaka wahusika.

Kamanda Rwambow hakutaja ukubwa wa ardhi yenyewe ingawa alisema ameelezwa kuwa ni eneo kubwa.

Mkazi wa Maputo Bw. Mfaume Khamis, alisema juzi kuwa sehemu hiyo ni pori lenye ukubwa wa karibu hekta 15 na kwamba kilichojengwa hapo ni kibanda cha mlinzi na wanachokiona porini hapo nyoka na wadudu wengine.
 
Back
Top Bottom