News Alert: Masha awasalimia Keko..

tatizo mnafikiri Wakili hakujua anachofanya!!! Lazima Mramba ahudhurie harusi ya mwanae.. shangilieni mazingaombwe yanayofanana na ukweli. HIvi kwani hii ni mara ya kwanza kwa mtu aliyewahi kuwa waziri kufikishwa mahakamani? HIvi hii ni mara ya kwanza kwa mtu "kigogo" kusimama kizimbani?

Angalieni rekodi za kesi za huko nyuma!
 
Hasira! hasira kali za Mkulu! Haki ungewamata wangekutambua. Punguza hasira mkulu, vita hii bado mbichi! Tuendelee kupigana kwa ncha za vidole vyetu hadi mwisho wa dahari, na Mungu awe kinga yetu kwenye vita hii.

Hi hii hii!
Unachekesha kweli

Kama nina hasira wala chichemi najinyonga tu.
 
Masha kaenda kucheki mazingira na kufanya booking huenda naye atawekwa ndani mahela alikula mengi ya uchaguzi.
 
Jamani labda kaenda kuangelia tuu hali ilivyo.. It gives a wrong image kwa yeye kama waziri coz its not exactly fair kwa watuhumiwa wengine waliopo rumande lakini....... Sio big deal
...Ni ukereketwa wa kutembelea mahabusu au kuna kitu kinaendelea na hao akina Mramba?

Kwa nini siku nyingine alikuwa hatembelei hayo magereza kuwasalimia mahabusu? Hata akienda inatangazwa kwenye vyombo vya habari...Wameshaanza kutuchezea kanya boya nini???

Nadhani kuna haja Masha abanwe na wanahabari ili atueleze kilichompeleka huko.
 
tatizo mnafikiri Wakili hakujua anachofanya!!! Lazima Mramba ahudhurie harusi ya mwanae.. shangilieni mazingaombwe yanayofanana na ukweli. HIvi kwani hii ni mara ya kwanza kwa mtu aliyewahi kuwa waziri kufikishwa mahakamani? HIvi hii ni mara ya kwanza kwa mtu "kigogo" kusimama kizimbani?

Angalieni rekodi za kesi za huko nyuma!

Dont tell me all this is hollywood!
 
tatizo mnafikiri Wakili hakujua anachofanya!!! Lazima Mramba ahudhurie harusi ya mwanae.. shangilieni mazingaombwe yanayofanana na ukweli. HIvi kwani hii ni mara ya kwanza kwa mtu aliyewahi kuwa waziri kufikishwa mahakamani? HIvi hii ni mara ya kwanza kwa mtu "kigogo" kusimama kizimbani?

Angalieni rekodi za kesi za huko nyuma!

Hapo umenena mkuu, Hata ukiangalia aina ya mashtaka waliyonayo inaonyesha kuwa huu ni usanii mtupu. Mi naoana hii mechi imeshachezwa mezani na matokeo yanafahamika. Ushindi ni tumepigwa Tatu bila.(3:0)

Kama unafuatilia hata kwa taarifa za habari za jana jioni maoni mengi ya wadanganyika yalikuwa ni kutoa pongezi nyingi tu kwa Kikwete na Kwa Serikali. Utadhani Kikwete ndo kawafungulia Mashtaka. Na hilo ndo liliokuwa lengo. Kupunguza presha za Wadanganyika. Na kama hamuamini huo ni Usanii subirini muone. Kesi haitaisha itapigwa kalenda weee then kama kawaida yetu tutasahau na ndio mwisho wa kesi

Lengo kuu la SISIEM hata kwenye katiba yao linasema ni Kushinda Uchaguzi so kwa gharama yoyote ile hata kama ni kutoa kafara baadhi ya watu watafanya ili mradi tu Washinde UCHAGUZI.

Wadanganyika Wenzangu Wake-Up please siyo muda wa kulala tena.
 
Ahsante Oldman Mwanakijiji!! naona kuna undercurrents nzito hapa, nini kinaendelea baada ya waheshimiwa hawa kuswekwa lupango?Hatujamsahau mheshimiwa Masha vilevile aliwahi kusema BBC kuwa lupango si Kempinski!! kafuata nini lupango-kubook nafasi nini?
 
Sijakuelewa

Mheshimiwa Zitto,

Hata mie sijamwelewa Mwanakijiji na kauli yake..

Between the Line,Hivi ile sheria ambayo inakataza Mbunge kushtakiwa ni sheria ipi?


ishu nyingine ni kuhsu huu utaratibu wa kupelekwa watu mahakamani na kuachiwa na utaratibu wa kesi haujulikani,mie naona kama ni njia ya kuzugwa tu ambayo tumeshaizoea kutoka kwa chama chetu.

Hivi hauni kwamba hii ni mbinu ya kunyamazisha upinzani?sababu wameamua kujiunga na nyie na kuwapa mnachotaka.?

kuna mtu kanidokeza toka huko nyumbani kuwa Yona aliliza waandishi wa Habari,Mmefurahi?

Mytake
Nahisi mtakuwa mmekosa na kuzungumza kwa sasa sababu mnachotaka CCM inafanya na mtakuwa mmenyong'onyea kwa kiasi flani na kuzooofishwa.

I think you should now find another way of campaign sera Zenu kuliko kuponda serikali(siyo kwamba muache).
 
Si Masha peke yake labda wengine hamkufanikiwa kuwaona tusubiri naamini na wengine wataonekana..!!
 
MAADILI GANI MNAYOYAZUNGUMZIA HAPA? MASHA HATA JUZI ALIKWENDA PALE KISUTU NA ALISALIMIANA NAO PUBLICLY.

UWAZIRI WAKE HAMFUNGI KUONGEA AU KUMTEMBELEA MTUHUMIWA PALE ANAPOSHIKILIWA NA VYOMBO VYA SHERIA.

KAMA NI DHAMANA, NI KWELI HAKIMU MWANKENJA(MTUMISHI WA MUNGU/mlokole) HAKUFANYA MAAMUZI KWA KUZINGATIA SHERIA ZINAZOMUONGOZA NA MBAYA ZAIDI ALIJIKUTA AMESUKUMWA NA UTASHI WAKE KAMA MWANANCHI NA SI MTAFSIRI WA SHERIA.

KIPENGERE ALICHOTUMIA KINARUHUSU NJIA MBADALA KTK DHAMANA LAKINI YEYE AKASISITIZA CASH, LAKINI HATA KTK REASONING YA KIJANA WA KIDATO CHA NNE TU ANGEWEZA KUTAMBUA SHARTI LA KUMZUIA MRAMBA ASITOKE DAR ES SALAAM HALIKUWA LINA MAANA NA SI HAKI KWANI YULE BADO NI MBUNGE HIVYO LICHA KUSHITAKIWA MBELE YAKE BADO ANALO JUKUMU LA KUWATUMIKIA WANA ROMBO NA BUNGE LA TANZANIA.

HATUMLAUMU HAKIMU KWA UPUNGUFU HUU ULIOJITOKEZA ILA NI FUNZO KWA WENGINE KUWA KABLA HUJAFANYA MAAMUZI YOYOTE YANAYOMUHUSU BINADAMU MWENZAKO NI VEMA UKATAFAKARI NA KUJIRIDHISHA KABLA HUJAJITOKEZA HADHARANI NA KUAMUSHA MORI KWA UMMA HALAFU BAADAYE ALIYE JUU YAKO ANATENGUA MAAMUZI YAKO NA KUIFANYA TAASISI KAMA MAHAKAMA IDHARAULIKE HUSUSANI KTK MASHAURI YENYE MASLAHI YA MOJA KWA MOJA NA WANANCHI.

NARUDIA TENA MASHA YUKO SAHIHI KAMA MTANZANIA, KIONGOZI NA MWANASHERIA.
huyu hakimu ni kweli hAWATENDEI HAKI WATUHUMIWA, UNAWEZA KUTUHUMIWA LAKINI IKAGUNDULIKA BAADAYE HUHUSIKA, WEWE NA MIMI HATUJUI KAMA AKINA MRAMBA NA WENGINE WANA MAKOSA,

NILIKUWA KISUTU NA HUYU HAKIMU ALITAKA WATU WALETE CASH 104,000,000 PALE MAHAKAMANI KUDHAMINI NDUGU ZAO KWENYE ILE KESI ZA EPA, HATA ALIPOAMBIWA KUWA WALETE BANKERS DRAFT ALIKATAA HUKU AKISEMA LETENI CASH KWA KUWA NYIE MMEZOEA KUSHIKA MAHELA MENGI HAMUWEZI KUOGOPA 104M, NI WAZI KWA UTASHI WAKE AMESHAWAHUKUMU HAWA, AMESAHAU KUWA HUENDA WALIOLETWA KWAKE NI KIINI MACHO TU, NA KUWA KUNA WENGI ZAIDI WAMEFICHWA, WACHACHE WAMETOLEWA KAFARA
 
...........AMESAHAU KUWA HUENDA WALIOLETWA KWAKE NI KIINI MACHO TU, NA KUWA KUNA WENGI ZAIDI WAMEFICHWA, WACHACHE WAMETOLEWA KAFARA


Danny Yona na Basil Mramba.......ni KAFARA!!!..........duhh ushabiki mwingine bana........
 
Kuna moja ya thread hapa nilichangia na kuwataadhalisha watanzania kuwa tuwe wajanja na changa la macho. Masha kuwatembelea hawa mafisadi tena nje ya ratiba yake ya kiofisi inaleta UTATA tena si kidogo.
SISIEMU wanajua wana uchaguzi, sasa kupeleka hawa fisadiz mahakamani isije ikawa ni changa la macho. Uchaguzi ukiisha basi na kesi nazo zinatupiliwa huko. Naamini masharti ya dhamana yao itakuwa sawa na wale washitakiwa wengine katika kesi ya EPA. Naamini Hakimu pamoja na upande wa mashitaka wanaangalia ni kiasi gani mshitakiwa kasababisha hasara kwa Taifa, na dhamana yake itatokana na kiwango kilichopotezwa kwa Taifa.

Serikali inatakiwa kuwa MAKINI, Don't play GAME. Watanzania wanaelewa kila upupu mnaoucheza.
 
- Ni kweli kwamba Masha alienda kuwaona watuhumiwa kule rumande hilo nimethibitisha baada ya kuongea, na nikauliza why kwa nini alienda? nimeambiwa kwamba kwanza Yona ni family friend na besides kuna "mkono mzito sana" uliomtuma na kumpa baraka za kwenda huko.

- Wakuu again kama ninavyosema mara nyingi kuna ambayo huwa hatuwezi kuyaweka hapa mpaka papoe, nimejaribu sana kuyasema anyways as much as I can, ninaomba nijaribu kuiweka ninavyoweza bila kugusa nisipotakiwa besides all inafahamika kwamba anayetafutwa hasa ni nani!

I hope this post inaweza kusaidia angalu kidogo on this ishu ya Masha kwenda huko rumande!

Thanxs!
 
Habari za ndani kabisa ni kuwa Masha hakwenda Keko hizi ni rumors ambazo hazina msingi wowote.
Tuwe waangalifu.

The sycophants wanaongezeka siku hadi siku na lengo kuu la hii zecomedy ni kuwazuga wanaozugika na Tz wako wengi tu. Siku ukiona mlemavu ambaye tunajua wazi hawezi kutembea akianza kusogeza mguu ujue nyuma yake kuna jambo. Ukiona gari la mkono (wheel-barrow) linasogea ujue linasukumwa na bila kumwona anayelisukuma ni heri kutahayari. The last kicks of a dying horse, can be deadly too. Wapiga filimbi watajaribu kufunika kombe lakini wazalendo wa kweli hawatakaa kimya tena.

Nawaomba wenye uchungu wayachukulie matukio haya kama motisha ya kuendeleza mapambano - asilale mtu mpaka kieleweke. Vita dhidi ya mafisadi ndiyo kwanza kabisa vinaaanza na hizi ni mbinu zao tu za kujipanga upya. Hayo mabandiko kama ya moelex23 yawe kichocheo cha kuwashikia bango siyo tu Yona na Mramba ambao ni kiini macho bali akina Masha na wote wanaotumika kwa kujua ama kutojua. Nyoka amekamatwa mkia na anajaribu kujiokoa lakini kichwa chake ni halali yetu.
 
Kuna moja ya thread hapa nilichangia na kuwataadhalisha watanzania kuwa tuwe wajanja na changa la macho. Masha kuwatembelea hawa mafisadi tena nje ya ratiba yake ya kiofisi inaleta UTATA tena si kidogo.
SISIEMU wanajua wana uchaguzi, sasa kupeleka hawa fisadiz mahakamani isije ikawa ni changa la macho. Uchaguzi ukiisha basi na kesi nazo zinatupiliwa huko. Naamini masharti ya dhamana yao itakuwa sawa na wale washitakiwa wengine katika kesi ya EPA.

Hivi mmeshasahau kwamba kwenye hizo noti zenu hapo Tz kuna sahihi ya bwana B.P Mramba??? kama bado hizo noti zenye sahihi yake zipo kwenye mzunguko basi mtapata majibu
 
Habari za ndani kabisa ni kuwa Masha hakwenda Keko hizi ni rumors ambazo hazina msingi wowote.

Tuwe waangalifu.

Moelex23, Nadhani hii article ni uthibitisho wa kutosha kwamba Masha alikwenda Keko.

Date::11/27/2008
Waziri Masha azuru gerezani waliko Mramba, Yona
Mwanamkasi Jumbe na Rosina John
Mwananchi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, jana alitembelea gereza la mahabusu Keko jijini Dar es Salaam, siku moja baada ya mawaziri wawili wa zamani kuwekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti.

Masha alifanya ziara hiyo wakati mawakili wa mawaziri hao wawili-Basil Mramba na Daniel Yona- wakiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hezron Mwankenja ombi la kutaka mwenendo wa kesi na hukumu ya amri ya dhamana ili wakate rufaa kupinga masharti yaliyowekwa katika kesi hiyo ambayo wanasiasa hao wameshtakiwa kwa kutumia vibaya ofisi kwa kuipa kampuni ya M/S Alex Stewart mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria.

Dhamana hiyo ni ya Sh3.9 bilioni kila mmoja na watuhumiwa wote wawili walishindwa kutimiza masharti na hivyo kulazimika kwenda kulala mahabusu ya Keko. Masharti mengine ni pamoja na kuikabidhi hati za kusafiria baada ya mawaziri hao kusomewa jumla ya mashtaka 13 kwenye kesi hiyo.

Siku moja baada ya mawaziri hao kulala Keko, Waziri Masha alionekana akifanya ziara kwenye gereza hilo lililo wilayani Temeke.

Masha alijitetea kuwa, alikuwa amefanya ziara ya kikazi kwenye gereza hilo, lakini kinachoshangaza ni kwamba alitumia gari binafsi.

Masha alionekana akiwasili gerezani hapo na alipotakiwa kuzungumzia lengo la ziara hiyo kwenye mahabusu hiyo, alikataa na kuondoka zake.

Wakati alipopigiwa simu baadaye, Waziri Masha alisema alikwenda kwenye gereza hilo la mahabusu ikiwa ni sehemu ya majukumu yake.


"Ni kweli kuwa nilienda gereza la Keko, lakini nilienda huko kwa ziara ya kiofisi kwa hiyo hakuna sababu ya wewe kuwa na wasiwasi na ziara yangu huko," alisema.

Na alipoulizwa kama alipata nafasi ya kuwaona mawaziri hao wa zamani walio kwenye gereza hilo baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana juzi, Masha alisema si jukumu la gazeti kujua amemuona nani kwenye mahabusu hiyo na kusisitiza kuwa alifanya ziara ya kikazi.

Lakini alipozongwa zaidi kwa maswali, alisema: "Nashangaa unataka unipeleke wapi. Nimeshakuambia kuwa Keko ni moja ya taasisi zilizo chini ya mamlaka yangu kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Hakuna ubaya kwangu kutembelea huko."


Katika mahabusu hiyo kulikuwa na ndugu wengi wa wanasiasa hao, akiwemo mke wa Mramba, ambaye aliwasili mapema asubuhi akiwa na baadhi ya ndugu.

Katika hatua nyingine, kampuni ya uwakili ya Trust Mark Attorneys, iliwasilisha barua ya kutaka kupewa nakala rasmi ya mwenendo wa kesi na uamuzi wa masharti ya dhamana ili wakate rufaa kupinga masharti hayo.

"Tunaomba tupewe nakala za mwenendo, uamuzi na amri kuhusu suala la tarehe 25 Novemba ili tuchukue hatua muhimu," inasema sehemu ya barua hiyo iliyowasilishwa kwa Hakimu Mwankenja.

Hakimu Mwankenja alisema kuwa amepokea barua hiyo na kuagiza nakala hizo ziandaliwe haraka iwezekanavyo, akisema kuwa hatua kama hiyo ni muhimu kwa yeyote anayeona kuwa hakutendewa haki katika maamuzi ya masharti ya dhamana.

Mawaziri hao wa zamani, Mramba, ambaye ametumikia serikali za awamu zote tatu akishika wizara nyeti ikiwemo ya fedha, na Yona, ambaye aliongoza Wizara ya Nishati na Madini katika serikali ya awamu ya tatu- walikana mashtaka yote matatu ambayo inadaiwa yameiingizia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Juzi wakili wa upande wa utetezi, Joseph Thadeo, aliiomba mahakama kutoa masharti nafuu ya dhamana kwa kuzingatia kuwa watuhumiwa wote walionyesha ushirikiano na kwamba walienda mahakamani wenyewe.
 
This is what I reported:

"Jinsi alivyokuja kwa kweli aidha alikuwa na ujumbe fulani ambao ni yeye tu angeweza kuutoa au alikuja kuchukua ujumbe kutoka kwa washtakiwa" amesema afisa mmoja ambaye ana uhakika wa anachosema.

lakini for whatever reason.. watu wanasoma "Masha katembelea Gereza la Keko"!!! It is disheartening. Wengine wanahoji kama ni taarifa ya kweli kwani kutwa nzima ya jana hakuna chombo kingine cha habari kilichotoa ripoti hiyo.

Haya mapambano yamechukua sura mpya hivi karibuni ni wapambanaji wa dhati wataweza kuona yanaelekea wapi. Sisi Cheche tutaenda next step and continue to lead this ideological battle of which there is no retreat and surrender is not an option. We are in for a long haul.

Good day! Happy Thanksgiving!
 
....
Haya mapambano yamechukua sura mpya hivi karibuni ni wapambanaji wa dhati wataweza kuona yanaelekea wapi. Sisi Cheche tutaenda next step and continue to lead this ideological battle of which there is no retreat and surrender is not an option. We are in for a long haul.

Good day! Happy Thanksgiving!

Hiyo next step natamani iwe inahusisha pia kuongeza frequence ya kijarida kutoka, iongezeke zaidi ya mara moja wka wiki
 
Back
Top Bottom