News Alert: Masha awasalimia Keko..

Tayari sarakasi na usanii vimeanza, at least i expected it to be very covert naona tunaonekana wajinga sana kiasi cha kufanyiwa mazingahombwe mchana kweupe. Nadhani kuna haja na kupitisha petition ya Masha kujiuzulu, kutokana na kuonesha mwenendo wa ku-meddle na kasi hiyo.
 
Kwa hali ilivyo ni aibu kwa kiongozi wa serikali kujitokeza na kwenda kuzungumza na mahabusu ambao wanahusika na shutuma za ubadhirifu kama kuzungumza nao basi angewahi kabla hawajapandishwa kizimbani.Vinginevyo atashindwa kueleweka na inawezekana kabisa nae akasukumwa kwenye kundi hilo la mafisadi ,itabidi huyu achunguzwe kama kuna kiasi kikubwa cha fedha kiliingia kwenye account yake kwa siku za karibuni,unaweza kukuta ameenda kutoa habari kuwa feza imeshaingia.
 
Hivi huyu Masha atakuwa lini? Maana tuhuma zake nyingi hapa jamvini ni za kitoto toto tuuu. Hebu aache kufanya mambo ya kombolela...Asitufanye wajinga, Watanzania wanaelewa hata lugha za ishara sasa ggggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Eti kuna tatizo kwa waziri ambaye ni mwananchi wa Tanzania kama sisi wananchi kwenda gerezani, kuwaona wananchi ambao ni lets say marafiki zake? Are you guys serious au this is another April fools? What is wrong with that? Kuna sheria ya Jamhuri imevunjwa, au I am missing something here?

Mwalimu alipoenda gerezani kumtembelea rafiki yake Dr. Kaunda aliyekuwa mtuhumiwa wa uhaini nchini Zambia, kulitakiwa kuwe na problem? what problem? Kaunda mtuhumiwa wa uhaini kwa kutaka kumpindua rais Chiluba, leo rais wetu mstaafu anakwenda rumande kumuona, kwa this ideas hapa ina maana gani kwamba eti Mwalimu alikuwa anamu-undermine Chiluba na serikali yake, au alikwenda tu kumuona his firend? Au Mwalimu ndiye aliyemsaidia Kaunda katika njama zake za kutaka kumpindua the then a sitting president wa Zambia?

Wakuu sometimes tunakwenda out of the lines na hizi uncalled and unconstructive criticism! Au kwa sababu tu ni Minister Masha? a successful young man and larger than life at his age of 30s?

Wazee wa Sauti ya Umeme, Kutoka Radio Station ya FMES.
 
FMES,
Usifananishe safari ya Mwalimu kumtembelea Kaunda gerezani Zambia na hii ya Masha. Kaunda alikuwa amefunga akipinga kuwekwa jela na Chiluba. Mwalimu alikwenda kama mpatanishi, kwanza kumwomba Chiluba amwachie huru Kaunda na pili, kumsihi Kaunda asisusie chakula. They broke bread together in jail. Hapo mimi sioni comparison kabisa. Politically alichofanya Masha ni questionable akiwa kama waziri wa mambo ya ndani. Hata kama ana urafiki na Yona au Mramba haukuwa wakati muafaka kwake kuwatembelea Keko. Inaweza kuzua hisia za political interference katika shughuli za mahakama.
 
...Politically alichofanya Masha ni questionable akiwa kama waziri wa mambo ya ndani. Hata kama ana urafiki na Yona au Mramba haukuwa wakati muafaka kwake kuwatembelea Keko. Inaweza kuzua hisia za political interference katika shughuli za mahakama.

Jasusi,

Hivi ni kwa nini viongozi wetu vitu kama hivyo hawavioni lakini watu wa kawaida na walala hoi ndio tunashtukia haya mambo ya appearance of impropriety ?

Huyu Masha si wanasema alikulia Magharibi, kwenye society zilizobobea kuzingatia mambo hayo, tena hata high school kasoma nao ?

Yani ukishachanganyika katika mazingira ya Bongo unasahau kabisa mambo hayo ?

Ila kitu kimoja namsifu sana Kikwete ni pale msimamizi wake wa ndoa aliposweka lupangp akamchunia kabisa na akajifanya hajawahi hata kusikia jina la Ukiwaona Wafyatue Ditopile Risasi Mzuzuri.
 
FMES,

Watu wanavyopigia kelele suala hili la Waziri Masha kwenda gerezani nadhani wameangalia historia ya huyu ndugu yetu katika masuala mazima ya kuwa linked na ufisadi unaoendelea hapa nchini kwetu Tanzania. Kumbuka, huyu jamaa alikuwa anajihusisha moja kwa moja kama mshikadau mkubwa wa IMMMA (Ishengoma Karume Masha and Magai) advocates, ingawa kwenye website yao bado anaonekana kuwa active lawyer kama inavyoonekana kwenye hii link: Ishengoma Karume Masha & Magai (IMMMA Advocates)

Hata ndugu yetu Mramba naye aliwahi kuandika nakala kuelezea suala la waziri wetu huyu kujishughulisha moja kwa moja na Deep Green ambayo ilichota mabilioni mengi ya fedha za EPA - link ya article : Makala -Waziri Masha anayo hadithi tamu kuhusu mafisadi wa EPA

Hivyo basi ndugu yangu FMES, Mimi nadhani ni busara kuziheshimu hisia za wachangiaji ambao bado wana wasiwasi na kujichomekeza kwa huyu mheshimiwa huko Keko, tena akiwa kaenda kuwatembelea waheshimiwa wengine walio katika kundi la wanaohisiwa (innocent until proven guilty) kuwa wamefidasisha nchi yetu. Ni hilo tu.
 
Lakini si alienda kama Masha na si Waziri Masha?
Icadon,
Granted alikwenda as a private citizen, bado ile appearance ya Waziri wa serikali kuingilia suala la mahakama haitaepukika miongoni mwa Wagalatia.
The timing was not appropriate.
 
Icadon,
Granted alikwenda as a private citizen, bado ile appearance ya Waziri wa serikali kuingilia suala la mahakama haitaepukika miongoni mwa Wagalatia.
The timing was not appropriate.

Kama alikwenda as private citizen kwa nini alitumia pesa ya walipa kodi na gari la serikali?
 
FMES,
Usifananishe safari ya Mwalimu kumtembelea Kaunda gerezani Zambia na hii ya Masha. Kaunda alikuwa amefunga akipinga kuwekwa jela na Chiluba. Mwalimu alikwenda kama mpatanishi, kwanza kumwomba Chiluba amwachie huru Kaunda na pili, kumsihi Kaunda asisusie chakula. They broke bread together in jail. Hapo mimi sioni comparison kabisa. Politically alichofanya Masha ni questionable akiwa kama waziri wa mambo ya ndani. Hata kama ana urafiki na Yona au Mramba haukuwa wakati muafaka kwake kuwatembelea Keko. Inaweza kuzua hisia za political interference katika shughuli za mahakama.

- Jasusi unakwenda kupatanisha mtuhumiwa wa uhaini na aliyetaka kumpindua? Ninaamini kwamba vitendo vyote ni sawa, Masha waziri ambaye pia ni mwananchi amekwenda kuona marafiki zake who happened to be watuhumiwa, na Mwalimu alienda kumuona rafiki yake who happened to be mtuhumiwa.

- Eti haukuwa wakati muafaka wa kuwatembela "marafiki" zake watuhumiwa gerezani? Then upi ni wakati muafaka mkuu?

- Jasusi ukienda rumande kutembela "marafiki" zako as a human beings unaweza kuleta interference katika shughuli za mahakama? Is that so? Una maana viongozi wetu Tanzania wanatakiwa wasiwe binadam ambao wakikatwa mwili inatoka damu kama wengine wote?

Kutokujiamini na sheria zetu kusitufanye tukaanza kudai viongozi wasiwe kama sisi binadam wengine wote, kama politically Masha kwenda kuwaona at this stage ni makosa then ni lazima aje alipie kwenye uchaguzi ujao, lakini otherwise turuhu binadam wawe binadam, kama Masha ana makosa kisheria kwenye EPA believe me hawezi kupona maana kimbunga kinachokuja sio kawaida, lakini for now turuhusu awe binadam na mwananchi kama sisi wengine!

Nothing personal but just trying to see the otherside othe coin!
 
Eti kuna tatizo kwa waziri ambaye ni mwananchi wa Tanzania kama sisi wananchi kwenda gerezani, kuwaona wananchi ambao ni lets say marafiki zake? Are you guys serious au this is another April fools? What is wrong with that? Kuna sheria ya Jamhuri imevunjwa, au I am missing something here?

Mwalimu alipoenda gerezani kumtembelea rafiki yake Dr. Kaunda aliyekuwa mtuhumiwa wa uhaini nchini Zambia, kulitakiwa kuwe na problem? what problem? Kaunda mtuhumiwa wa uhaini kwa kutaka kumpindua rais Chiluba, leo rais wetu mstaafu anakwenda rumande kumuona, kwa this ideas hapa ina maana gani kwamba eti Mwalimu alikuwa anamu-undermine Chiluba na serikali yake, au alikwenda tu kumuona his firend? Au Mwalimu ndiye aliyemsaidia Kaunda katika njama zake za kutaka kumpindua the then a sitting president wa Zambia?

Wakuu sometimes tunakwenda out of the lines na hizi uncalled and unconstructive criticism! Au kwa sababu tu ni Minister Masha? a successful young man and larger than life at his age of 30s?

Wazee wa Sauti ya Umeme, Kutoka Radio Station ya FMES.

You are missing a point. Look for another example. Facts za Nyerere na za Masha ni tofauti kabisa. Please, lead between the lines and you will come to the conclusion that something is wrong somewhere na ugeni wa Masha Gerezani.

Wake up, buddy
 
FMES,
Usifananishe safari ya Mwalimu kumtembelea Kaunda gerezani Zambia na hii ya Masha. Kaunda alikuwa amefunga akipinga kuwekwa jela na Chiluba. Mwalimu alikwenda kama mpatanishi, kwanza kumwomba Chiluba amwachie huru Kaunda na pili, kumsihi Kaunda asisusie chakula. They broke bread together in jail. Hapo mimi sioni comparison kabisa. Politically alichofanya Masha ni questionable akiwa kama waziri wa mambo ya ndani. Hata kama ana urafiki na Yona au Mramba haukuwa wakati muafaka kwake kuwatembelea Keko. Inaweza kuzua hisia za political interference katika shughuli za mahakama.

Naam, nakubaliana na wewe kabisa Jasusi. Urafiki kwenye kesi nzito kama hii ni lazima uwekwe pembeni ili kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake bila mkono wa yeyote yule bila kujali wadhifa wake. Kitendo cha Masha kwenda kuwatembelea Keko tayari kinaweka alama kubwa ya kuuliza kuhusu kesi hii. Je, kulikoni Waziri wa mambo ya ndani ambaye DPP anaripoti kwake aende akawatembelee washtakiwa wakati yeye anatakiwa awe upande wa mashtaka? Kuna kasoro hapa tena kubwa sana.
 
Kutoka mwanakijiji.com

...Bw. Masha aliyeenda gereza hilo kwa gari lake la binafsi na ambaye hakuwa ameonekana kuvaa "kiofisi" alishindwa kueleza ni kwanini kama amekwenda kule kikazi aende kwa kutumia gari la binafsi na bila ya kutoa taarifa ya awali kwa umma. Bw. Masha alishindwa kuelezea hilo hasa ikizingatiwa kuwa katika eneo la Dar kuna magereza mengine makubwa mawili ya Ukonga na Segerea ambayo angeweza kuyatembelea lakini aliamua kwenda kwenye gereza la Keko ambapo "jamaa" zake wanashikiliwa....

nimuhimu kufahamu kama masha alikwenda kuwaona mahabusu hao "kibinasi"
jee alikwenda muda rasmi wa kuwaona mahabusu au alikwenda nje ya muda
huo? kama alikwenda nje ya muda wa kuona mahabusu basi "amechanganya madawa".

ukishakuwa kiongozi mara nyingi inabidi uwe mwangalifu kwa mambo unayofanya kwani yapo mambo utayofanya yanayoweza kuleta picha/hisia mbaya kisiasa hata kama huvunji sheria.

mwalimu alikwenda kumuona kaunda waziwazi kabisa sasa sijui kama masha alikwenda kihivyo. tusikie atasema nini (kama atasema).
 
Huu ni uchambuzi mzuri, maana kama alivosema ndugu kafara, huko Keko kuna mda rasmi wa ndugu na marafiki kwenda kuwatembelea wafungwa. Sijawahi kufungwa Keko hivyo sina data za mambo yanavyokwenda uko, ila kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba mtu huwezi kukurupuka tu na kwenda tembelea ndugu na jamaa ambao wamefungwa gerezani. Kuna utaratibu maalumu wa kufuatwa, na kutokana na u-sensitive wa eneo hilo (magereza) matembezi hayo hufanywa within working hours, na si vinginevyo.

Kama Masha alikwenda nje ya mda huo, na kama anatumia kigezo cha kwenda huko Keko kwamba ilikuwa sio ziara rasmi (ya kikazi), then inabidi atoe maelezo why alifanya hivyo na why alitumia cheo chake vibaya kuwaghiribu walinzi wa Keko kumkubalia kufanya ziara isiyo rasmi nje ya mda wa kawaida wa magereza kwa kutumia mgongo wa uwaziri... Tunahitaji majibu ya kueleweka kwenye hili.
 
Kama Masha alikwenda nje ya mda huo, na kama anatumia kigezo cha kwenda huko Keko kwamba ilikuwa sio ziara rasmi (ya kikazi), then inabidi atoe maelezo why alifanya hivyo

Fair and balanced analysis.
 
Mramba, Yona wahaha kutoka rumande Keko
Shadrack Sagati
Daily News; Wednesday,November 26, 2008 @21:15

Masharti ya dhamana yaliyowekwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, yamezidi kuwaelemea mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, na sasa wameonyesha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu.

Mawaziri hao wa zamani wanashitakiwa kwa kutumia vibaya madaraka waliyokuwa nayo ya uwaziri kwa kuipendelea Kampuni ya Alex Stewart na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7, kati ya mwaka 2003 na 2007.

Kampuni hiyo ilikuwa inajishughulisha na ukaguzi wa hesabu za kampuni zinazochimba dhahabu nchini. Mawakili wa upande wa utetezi jana waliwasilisha barua kwa Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja ambaye ndiye aliyewapa sharti wanaloona gumu la kuweka fedha taslimu Sh bilioni 3.9 kila mmoja.

Barua hiyo inaiomba mahakama hiyo kuwapatia mawakili wa washitakiwa mwenendo wa shauri hilo ili wawasilishe rufani yao Mahakama Kuu kuomba kulegezwa kwa masharti hayo.

Masharti mengine yaliyotolewa na Hakimu Mwankenja ni washitakiwa kukabidhi hati zao za kusafiria kwa waendesha mashitaka na hawaruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama. Sehemu ya barua ya mawakili hao inaeleza kuwa,

"We request to be supplied with certified copies of the proceedings, ruling and order in respect of the above matter dated 25th November 2008 for our necessary action." Katika tafasiri isiyo rasmi mawakili hao wanasema kuwa wanaomba kupatiwa nakala ya mwenendo, uamuzi na amri za shauri hilo lilitolewa uamuzi Novemba 25, 2008 kwa ajili ya hatua zaidi.

Hakimu Mwankenja tayari ameagiza mahakama iwapatie haraka mwenendo wa shauri hilo ili wakamilishe taratibu zao za kutaka kukata rufaa. Washitakiwa wanatetewa na kundi la mawakili ambao ni Joseph Tadayo, Michael Nyaro, Mafuru Mafuru, Sam Mapande na Elisa Msuya.

Jopo hilo juzi liliomba mahakama iweke masharti nafuu ya dhamana. Juzi Tadayo aliomba mahakama wakati inatoa masharti ya dhamana kuhusu kipengele cha fedha taslimu, iangalie pia uwezekano wa kuweka sharti mbadala ambalo ni kuwa na hati yenye thamani ya nusu ya fedha zinazodiwa kusamehewa Kampuni ya Alex Stewart.

Sharti jingine ambalo Tadayo aliomba ni mahakama iangalie kanuni ya washitakiwa kuchangia kiasi hicho cha fedha kama sheria ya dhamana inavyoelekeza. Upande wa mashitaka unaoongozwa na wakili wa Serikali Boniface Stanislaus, haukuwa na pingamizi lolote kuhusu maombi hayo ya washitakiwa na wakaiomba mahakama itumie busara yake katika kuamua masharti.

Kutokana na mahakama kuweka masharti hayo, washitakiwa hao walishindwa kutimiza masharti hilo na kulazimika kupelekwa kortini. Mramba katika kesi hiyo anaguswa na mashitaka yote 13 wakati Yona anaguswa na mashtaka sita. Mashitaka yanayomgusa Yona ni yale ya kushiriki kuipendelea kampuni ya Alex Stewart kwa kuipa nyongeza ya mkataba.

Lakini pia waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini anatuhumiwa kuipendelea kampuni hiyo, kuiachia suala la ukaguzi wa hesabu za kampuni zinazochimba madini nchini kufanywa kiholela na kampuni hiyo bila kuishirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutokana na kutokuwa makini, Yona anahusishwa kuchangia kuisababishia hasara ya Sh bilioni 11.7 Serikali ya Tanzania.

Mramba, licha ya kuguswa na mashitaka hayo, lakini pia anatuhumiwa kutoa misamaha mbalimbali ya kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart na kusababisha hasara hiyo ya Sh bilioni 11.7. Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 2, mwaka huu kutokana na upande wa mashitaka kuendelea na upelelezi wa shauri hilo.

Serikali iliingia mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo Juni, 2003 kwa lengo la kuhakiki uzalishaji na gharama za usafirishaji wa dhahabu pamoja na uwekezaji na uendeshaji wa migodi mikubwa na mkataba huo ulimalizika Juni mwaka jana. Baada ya mkataba huo kumalizika, kampuni hiyo iliongezewa mkataba mwingine kinyemela.

Bunge liliwahi kuelezwa na serikali kuwa katika kipindi cha miaka miwili kampuni hiyo ilikuwa inalipwa zaidi ya dola za Marekani milioni 31 (zaidi ya Sh bilioni 38) kwa wakati huo. Baada ya kumalizika mkataba huo, serikali haikuitisha zabuni nyingine, bali kwa kifungu namba 2.4 cha mkataba iliongezewa tena mkataba huo kwa kile walichodai baada ya kuridhika na utendaji wake wa kazi.

Katika hatua nyingine, imefahamika kuwa baadhi ya wafanyabiashara nchini wamekuwa na vikao tangu juzi wakihaha kusaka fedha kwa ajili ya kuwadhamini mawaziri hao wa zamani. Imefahamika kuwa vikao hivyo vimekuwa vikiratibiwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao ni watendaji katika kampuni mbalimbali kubwa nchini.

Aidha, imefahamika kuwa keshokutwa Jumamosi, binti wa Mramba anatarajia kufunga pingu za maisha Dar es Salaam, baada ya kuwa amekwisha kufanyiwa tafrija ya kuagwa hivi karibuni. Wakati huo huo, Iman Mwakyosa mshitakiwa pekee katika kesi ya kuchota mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ambaye amebaki bila kudhaminiwa, amekata rufaa Mahakama Kuu kupinga masharti kadhaa ya dhamana.

Sharti analopinga Mwakyosa ni la kuweka fedha taslimu ambalo limewekwa na Hakimu Mwankenja. Wenzake watatu tayari wameshapata dhamana. Wenzake katika kesi hiyo, Esther Mary Komu, Bosco Kimela na Rajab Maranda wamedhaminiwa baada ya kutoa fedha taslimu zaidi ya Sh milioni 103.
 
........Kuna utaratibu maalumu wa kufuatwa, na kutokana na u-sensitive wa eneo hilo (magereza) matembezi hayo hufanywa within working hours, na si vinginevyo.

Kama Masha alikwenda nje ya mda huo, na kama anatumia kigezo cha kwenda huko Keko kwamba ilikuwa sio ziara rasmi (ya kikazi), then inabidi atoe maelezo why alifanya hivyo na why alitumia cheo chake vibaya kuwaghiribu walinzi wa Keko kumkubalia kufanya ziara isiyo rasmi nje ya mda wa kawaida wa magereza kwa kutumia mgongo wa uwaziri... Tunahitaji majibu ya kueleweka kwenye hili.

............na hayo maelezo itabidi ayatoe.........as soon as possible ku-clear (if possible) the image portrayed
 
Huu ni uchambuzi mzuri, maana kama alivosema ndugu kafara, huko Keko kuna mda rasmi wa ndugu na marafiki kwenda kuwatembelea wafungwa. Sijawahi kufungwa Keko hivyo sina data za mambo yanavyokwenda uko, ila kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba mtu huwezi kukurupuka tu na kwenda tembelea ndugu na jamaa ambao wamefungwa gerezani. Kuna utaratibu maalumu wa kufuatwa, na kutokana na u-sensitive wa eneo hilo (magereza) matembezi hayo hufanywa within working hours, na si vinginevyo.

Kama Masha alikwenda nje ya mda huo, na kama anatumia kigezo cha kwenda huko Keko kwamba ilikuwa sio ziara rasmi (ya kikazi), then inabidi atoe maelezo why alifanya hivyo na why alitumia cheo chake vibaya kuwaghiribu walinzi wa Keko kumkubalia kufanya ziara isiyo rasmi nje ya mda wa kawaida wa magereza kwa kutumia mgongo wa uwaziri... Tunahitaji majibu ya kueleweka kwenye hili.

Tanzania kuna watu ambao ni above the law - they do no wrong even when they err. Behind each one of them lurks the mysterious servile flatterer who will always try to find some way to rationalize their suspicious and irresponsible acts. Hasn't this been the trend all along in this land where the rule of law is best defined as the law of rule ? What Masha did should act as an indicator as to the direction i.e. where this much ado-about-nothing will lead to, any bets ?
 
Back
Top Bottom