NEWS ALERT: IDD SIMBA aanza kwa mkwara...

Sidhani kama kuna mpango wa siri hapa, ama sivyo Idd Simba angekuja na dhamana yenye reasonable value, mimi nafikiri kitendo cha yeye kujilipua na hiyo dhamana yenye thamani ya 8 Billioni ni kwamba alihisi wanataka kumlaza ndani kijanja janja hivyo akaja fully prepared kama noma na iwe noma
 
hivi ule mjumba wa Iddi Simba kule Mikocheni ni bilioni 8 tuuu?

haiwezekani

nijuavyo mimi ile nyumba na kiwanja na ufukwe ni zaidi ya bilioni 20 unless Simba kaonyesha hati nyingine
 
Nchi ya kitu kidooogo, ni Nchi ya Watu wadooogo, Ukitaka chai wewe trafic nenda Mufindi!
 
mi nashangaa sana sasa kwa kwel cjui 2nakwenda wap ? Kimsingi huyo bwana mdogo id simba hayo mapesa yote kayatoa wap kwa mda mfup aliofanya kaz hapo na kujidhamin kwa bl.8, hao ndo wez sugu 2nao watafuta, wa2 2mefanya kaz serikalin na kwenye mashrka na makampun binafsi makubwa ha2jawah kushka hata bl.2 ama kwel mcheza kwao hu2nzwa!!
Tuongelee kesi kwa utajiri Idd simba nitajiri wa miaka nenda rudi tena ni mrithi wa utajiri wa baba yake, yasemekana hata corporate branch ya nbc pale city centre ilikuwa yao. umatemate wa simba si wa jana wala juzi tuongelee hili la kesi yake.
 
Ni Idd Simba mbele ya Hakimu Mfawidhi Ilvin Mgeta,Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Anasomewa mashtaka ya ufisadi na kusababisha hasara kwa UDA.Mashtaka yakasomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU,Benny Lincoln.Mawakili wasomi wawili wakajitambulisha kama wanaomtetea Simba.Ni Said El-Maamry(pia Mjumbe wa Tume wa Maoni ya Katiba) na Alex Mgongolwa.

Baada ya kusomwa mashtaka,Mawakili wa Simba wakasimama na kuomba dhamana kwa mteja wao kwakuwa mashtaka ambayo kwayo mteja wao anashtakiwa yanadhaminika.Lincoln hakuonyesha upinzani.

Hakimu Mgeta akamtaka kila mshtakiwa adhaminiwe na wadhamini wawili wenye bondi ya shilingi milioni 500 kila mmoja.Fedha nyingi eeh? Kwako tu.

Mawakili wa Simba wakawasilisha hati ya kiwanja na nyumba ikiwemo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.Bondi yake ilikuwa na uwezo wa kudhamini washtakiwa 8 kwa masharti kama ya Hakimu Ilvin Mgeta.Kuonyesha kuwa Simba 'anajali',akaruhusu wenzake wawili pia watumie hati yake kupata dhamana.

Wenzake wakafaidi kuwa na Simba.Simba anakuwa kigogo wa kwanza kutokwenda mahabusu siku ya kwanza ya kupelekwa Mahakamani.Ni kigogo wa kwanza ambaye upelelezi wa kesi yake ulikamilika kabla ya kuletwa Mahakamani.Ni tofauti na wote waliotangulia.

Picha imeanza...

dah,,,aisee hii picha title yake ni:SARAKAS ZA TAKOKURU NA VIGOGO WALA RUSHWA TANZANIA-PART III
 
......si wa tasnia ya sheria, lkn uzoefu wa kufatilia mambo umenifunza kuwa hata sheria wakati mwingine (na mara nyingi zaidi ktk nchi zetu za ulimwengu wa tatu) uihalifu haki...laiti tungegeuka kidogo tukatazama kwa wenzetu wa indonesia wanavyoshughulikia ufisadi kwa muondoko wa "mahaka za umma", kisha tukatazama rafiki zetu wa uchina wanavyohukumu wala rushwa, hakika lugha yetu juu ya rushwa ingekuwa jambo lingine...kucheza na rushwa ingekuwa sawa na kushika nyaya za msongo mkubwa wa umemena mikono mitupu!

sure mdau,,,,,ila wenyewe wanadai suala la haki za binadam zinaangaliwa.......,hata hoseah ashawai kusema hayo,including Jk
 
Tuongelee kesi kwa utajiri Idd simba nitajiri wa miaka nenda rudi tena ni mrithi wa utajiri wa baba yake, yasemekana hata corporate branch ya nbc pale city centre ilikuwa yao. umatemate wa simba si wa jana wala juzi tuongelee hili la kesi yake.

isitoshe ni mwenyekiti wa Mababu na mamwinyi wa Dar es Salaam,sasa siku wakimshawish JK ujue kesi inafutwa......Hata Jk alipokubali Iddi Simba amkaribishe kwa wazee wa Dar,haikua fair kabisaaaa,,,,,,
 
Nashangaa hati na thaman ya nyumba zimekubaliwa bila hata mjadala kama ule wa Mramba hadi wathamini wa serikali wazifanyie uthamini!au walishajua wakazifanyia uthamini serikalini?
 
yani hapo ni kama vile ameweka statement kua hapo hafungwi mtu..atahonga hakimu,witnesses na wengineo wote watakoitwa hapo mahakamani...kua na hela raha sana ukiwa hapa bongo
 
Akili Kumkichwa....hapo ujue kila kitu kilikamilika pamoja na dhamana na uigizaji utakaofanywa mahakamani...Pale walikuwa wakiperfom walichokuwa wamepractice kabla....Tanzania ni zaidi ya uijuavyo...

Unafikiri TAKUKURU walipokuwa wanachunguza walikuwa hawamuulizi maswali? Kama jibu ni ndio basi alijitayarisha na kujuwa kuwa hii itafika mahakamani. Kuna nini cha ziada hapo? Hapo ndio utaona tofauti ya Mramba na Simba.
 
bonge la movie lakini mara zote 'stering' huwa hauwawi akiuwawa ujue picha limekwisha. N atusubiri ili tuone mwisho wake
 
Hao kesi zao zitakuwa za kweli kuanzia 2015 magwanda wakishika nchi, sasa hivi acha wacheze maigizo yao tu
 
Kama ana Umatemate wa jinsi hiyo kwa nini aliruhusu pesa za UDA kuingia kwenye akaunti yake? Maana sijaelewa hilo somo alilotupa Wadanganyika!
 
kila mtu ana haki ya kupata dhamana.isipokuwa kwa makosa ya robbery,mauaji ya kukusudia na madawa ya kulevya ya mamilioni ya pesa.habari ndio hiyo someni sheria zenu za nchi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom