News alert: Dkt Slaa na Mh Tundu Lissu wafikishwa kizimbani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wakiwa kizimbani leo jijini Arusha.


Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii, Arusha


Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na wafuasi wao kadhaa wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kutuhumiwa kufanya mkusanyiko wa watu kinyume na sheria.


Mbali na mashitaka hayo Dk. Slaa pia anakabiliwa na shitaka lake peke yake la kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi akiwa katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC.


Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Devotha Kamuzora,Mwendesha mashitaka wa serikali Haruni Matagane aliiambia Mahakama hiyo kwamba kosa la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote 27 ambalo ni kufanya kusanyiko kinyume cha sheria na kutokutii amri ya jeshi la polisi.


Akisoma shitaka la pili Haruna aliiambia mahakama hiyo Dk. Slaa anayekabiliwa na mashitaka ya uchochezi ambalo ni kosa la tatu anadaiwa kutoa kauli zenye uchochezi akidai kuwa atahamasisha wafuasi wake waandamane hadi Magogoni Ikulu kuhakikisha wanamg'oa madarakani Rais Jakaya Kikwete.


Kipengele kingine kilichotajwa na mwendesha mashiataka huyo ni Dk. Slaa kutangaza kwamba watakodisha ndege kwa ajili ya kumbeba Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Zuberi Mwobeji na kisha wampeleke Dar es Salaam kwa IGP ili kumuuliza kwanini hadi leo hajamhamisha kazi OCD huyo.


Katika kesi hiyo upande wa watuhumniwa wote 27 unawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Method Kimomogolo na Albert Msando ambao kwa pamoja waliiambia mahakama hiyo kuwa wateja wao walikuwa na watu wa kuwawekea dhamana kama mahakama hiyo itaona kuna umuhimu huo.


Kwa upande wake Hakimu Mkazi Devotha Kamuzura aliwaambiwa watuhumiwa kwamba dhamana yao ipo wazi lakini kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na ahadi ya dhamana ya shilingi milioni tano.


Hata hivyo hadi mahakama hiyo inaashiriwa watuhumiwa 17 ndio walikuwa wamekiwisha kupata dhamana huku watuhumniwa tisa wadhamini wao wakishindwa kutimiza masharti ya dhamana.


Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 22, mwaka huu mahakamani hapo.

chanzo:
http://issamichuzi.blogspot.com/

woinde 153.jpg
 
Back
Top Bottom