Baada ya Kutoka Ufaransa na Italy, JK kuelekea China Jumatatu

Kweli watanzania tumeula wa chuya. Mnaona sasa hasara za kumchagua mtu kwa sababu anapendeza akivaa suti. Kazi imeshamshinda siku nyingi sasa anaamua kuwa mtalii tu. Huyu jamaa anaona hawezi kukaa bongo kwa jinsi hali ilivyo chafuka, na anahisi akiwepo hata kwa siku moja tu atajikuta anatakiwa ajibu shutuma za rushwa na ufisadi zinazowaandama CCM. Kazi ipo!
 
Ipo siku mtasikia anaenda Sayari ya Mars kuitangaza nchi...

yaani wembemkali kweli unakata hadi mifupa! teh teh teh teh

Jamani nimecheka sana kusoma hii..... Kikwete simwamini kabisa na hivi anaenda China mbona atapitia huko kwenda mwezini kwa hicho chombo wachina walichojenga!
 
Kama kawa... mapokezi makubwa yatakuwepo airport akirejea,
kama kawa... yataandamana na vigelegele, ngoma n.k. 7,
kama kawa... gharama zote hizo ni kutoka mifuko ya walipa kodi,
kama kawa... tunajua gharama kama hizo zinge epukika kwa kutumia mawaziri husika,
kama kawa... kampeni za kuhalalisha mafanikio ya safari zitakuwa kwenye kurasa za kwanza magazetini,
kama kawa... mafanikio hayo yangepatikana na pengine kuwiana na ya waziri yeyote husika kama angetumwa lakini gharama zingekuwa ndogo zaidi.
Kama kawaida nimeanza kugadhabika na safari hizi zinavyojirudia rudia kila kukicha kama usemi 'kama kawa' hali kuna wizara husika ambazo zingetumika na kuepuka gharama na karaha za kama kutumia neno 'kama kawa...'

SteveD.
 
Kikwete kula maisha mwaya,

Hivyo vitoto vinavyokufa hospitalini bila madawa maisha yao hayana thamani sana kama suti mbili ulizonunua NY kwenye safari yako ya juzi.
Nani alisema ikulu si pa kukimbilia? Nyerere (RIP) alishakufa so wewe kula nchi mwaya!

Mwafrika wa kike leo umenivunja mbavu, pia umenikumbusha mbali.
 
kuna rumors kuwa jk ameshakaa ofisini kwake ikulu less than 100 days total in all of 2 yrs as presido.

na katika hizo siku mia ujue ndani yake allmost zote ni zile akiwa kupokea mabalozi,viongozi n.k...vinginevyo mi nampa 50 dyas tuu
 
Ipo siku mtasikia anaenda Sayari ya Mars kuitangaza nchi...

ha ha hahaaaaa yaani hapo ndugu yangu umeniua mbavu kupita maelezo...ila kwa vile ana uhakika wa kupata fungu kutoka kwa wafuja jasho wa Tanzania walio too loyal to their serikali...basi he might introduce this idea..kama aliweza bring idea ya kuileta real madrid bongo kwa gharama zetu ashindwe hilo??
 
ha ha hahaaaaa yaani hapo ndugu yangu umeniua mbavu kupita maelezo...ila kwa vile ana uhakika wa kupata fungu kutoka kwa wafuja jasho wa Tanzania walio too loyal to their serikali...basi he might introduce this idea..kama aliweza bring idea ya kuileta real madrid bongo kwa gharama zetu ashindwe hilo??

Mafanikio mengine mpaka sasa kama yalivyoelezwa ni kuwa Pope atakuja/atapita Bongo katika ziara zake, pia Prodi wa Italia atakuja na ujumbe wa wafanya biashara.... HAYA NI MOJAWAPO YA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA!!

Kama Real Madrid hawakuweza kufanikiwa kuja kufungua uwanja mpya wa Taifa.... kwa sababu hizo hizo au zinazofanana waalikwa wengine wapya wanaweza wakasitisha safari zao. LAKINI NI MAFANIKIO YA MH. RAIS HAYO. Mafanikio mengine tunasubiri kuyasikia pale yatakapo chapishwa kurasa za mbele na magazeti.

SteveD.
 
na sie wa tz kama kawa kazi yetu ni kushawishika kirahisi na kudanganywa kama watoto wa cheke chekea..maana mie sioni hata umuhimu wa viongozi wa nchi zao kuja bongo labda waje hao wafanyabiashara..mana hao viongozi wakija kwanza mji wawa kama balaaa...n as if wao ndio wanakuja kudo business huku Tz..wao kazi yao ni kutalii tuu na kufuja pesa kama mtalii wetu jk akienda nchi zingine
 
mkomboziufisadi
Senior Member


Habari Kamili
-----------------------------------------------------------------

PRESIDENT OF TANZANIA H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE NAMED HONORARY GLOBAL CHAIR OF 2ND WORLD TOURISM MARKETING SUMMIT Beijing, China, October 28-30, 2007

The President of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, was named Honorary Global Chair of the 2nd World Tourism Marketing Summit(WTMS), which will take place in Beijing, China, October 28-30, 2007. The announcement was made by Sujit Chowdhury, Secretary General, of the Canada-based World Trade University(WTU), organizer of the Summit. The Summit, hosted by the Beijing Tourism Administration of the People’s Republic of China, will bring together more than 400 travel and tourism industry leaders from around the globe.

“My selection as Honorary Global Chair, as an African leader, reflects the strong and growing trade and economic ties between Africa and China, and the vast untapped potential that China represents. Travel and Tourism is the World’s largest Industry and is critical to sustainable economic development and the generation of productive employment. For this reason, the Summit is very timely,” stated H.E. President Kikwete.

Mr. Chowdhury, in making the announcement, said “H.E. Kikwete will bring to the Summit the dynamic and outstanding leadership that he has already demonstrated in Tanzania with his ability to attract major international investment. This is reflected in that Country’s dramatic growth and development path, especially in the booming tourism sector. We are looking forward to President Kikwete inspiring delegates to use this converging platform to create new joint venture opportunities.”

MkomboziUfisadi,

Political matured people, ambao Tanzania tunawahitaji sana sasa hivi than ever before, huwa wana tabia na uwezo mkubwa kama wako, yaani kutizama pende mbili za shilingi bila makengeza,

Ubarikiwe, na niaamini utafanikiwa kwenye lengo lako la ukombozi wa ufisadi, maana fisadi yoyote ni hatari sana sio kwa taifa tu, bali hata kwa familia yake, maana ukishaonja ufisadi huwezi kuwa na mwiko, naomba ufanikiwe mkuu na hii clear message kuwa pamoja na mabaya yanayofanyika hapa bongo, pia kuna na mazuri na yanaonwa na wenzetu huko nje!

Heshima mbele mkuu!
 
Sasa kwa vile mmekuwa hodari kujadili ziara zake huyu bwana je kuna yeyete ambaye ana keep track ziara zake za Nje ya nchi tangu ashike Urais?

Je katika zaiara hizo ipi ambao inatucost zaidi walipa kodi?

Je ni zipi ambazo hazina ulazima?

Na je nani anajua mchanganuo wa matumizi ya IKULU kwa kila safari moja ya Nje ya nchi ya Rais?

Je kuna ulazima yeye kuongozana na mkewe kila kona ya dunia?


La mwisho ambalo naweza kumtetea ni uamuzi wake wa kuishi CHURCHILL HOTEL LONDON badala ya ile mijihoteli aliyokluwa akifikia Rais wetu mpenda mambo ya kizungu kwa jina la BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Naamini kuna watu wa mahesabu wapo mtatupa hiyoexpenditure ya rais
 
La mwisho ambalo naweza kumtetea ni uamuzi wake wa kuishi CHURCHILL HOTEL LONDON badala ya ile mijihoteli aliyokluwa akifikia Rais wetu mpenda mambo ya kizungu kwa jina la BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Kwa hili hata mimi ninampa heko, maana hata kule US, mkuu wa zamani alikuwa akiishi Waldorf-Astoria, dola $ 5,000 kwa siku, Yes presidential suite,

Lakini Muuungwana, kayakataa hayo na kufikia Hyatt, bei poa $ 800 tu kwa siku!
 


Kwa hili hata mimi ninampa heko, maana hata kule US, mkuu wa zamani alikuwa akiishi Waldorf-Astoria, dola $ 5,000 kwa siku, Yes presidential suite,

Lakini Muuungwana, kayakataa hayo na kufikia Hyatt, bei poa $ 800 tu kwa siku!

lakini hapo CHURCHILL nako kuna siri vile vile ambayo ukiwauliza watu wako wa karibu watakuwambia

Niambie binadamu gani asiyetaka kufikia hii hoteli ya DORCHESTER?
especially kama ni rais wa nchi ambayo PUBLIC ACCOUNTS COMMITTEE haitii neno juu ya matumizi ya IKULU?
junior_suite.jpg


ES kama huna jibu basi wasiliana na MSWAHILI au MLALAHOI watakupa siri nzito za bosi kuamua kuweka kambi hao CHURCHIL ambaye ukilinganisha na hoteli ya MKPAYA ya DORCHESTER ni sawa na countryside B & B ( BED AND BREAKFAST)
 
wakuu hivi hakuna mwenye habari za ndani za yaliyojiri katika mkutano wa mkuu na wafanyabiashara wa milan?
mi nimesikia mwakilishi wa tanzania investment center alitoa mada na kuitaja barrick kama moja ya mifano ya makampuni bora yanayowekeza tz.
aidha mkuu aliwahamasisha wataliano kwa kuwaambia wakichelewa kuja bongo watakuta makampuni ya kichina, sauzi, nk wamemaliza uhondo.
 
he hehe ee wamemaliza uhondo so its means kuna uhondo watakiwa uje ufaidiwe na hao wazungu ehh
hakufika viwanja vya mpira?ac milan,inter milan au aliomba asipigwe picha??maana anaona aibu kwa sasa
 
Jamani utani mbaya, JK amechoka hata na yeye na hizi safari, si mmemuona kwenye msiba.
 
Niemona alikuwa ameuchapa usingizi, alafu looks like ana mawazo sana.

so wanaweza kuwa kweli wanahusika???
aibuu kiongozi mziimaaaaa kusinzia sinzia msibani...na aliyeuliza swali la ulazima wa ye kusafiri na samsing yake huyo anataka kuhalalisha mengine jamani..si bora sasa wasafiri kama picha tuumengine yanakua siri kuliko akienda kibachela kabsaaaa??
 
Back
Top Bottom