Newcastle na Middlesbrough zashuka daraja ligi ya Uingereza

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Newcastle na Middlesbrough zashuka daraja ligi ya Uingereza

2073566.jpg

Kevin Nolan wa Newcastle akiwa haamini kama wameshuka daraja Sunday, May 24, 2009 9:04 PM

Ligi ya Uingereza imeisha leo kwa timu ya Newcastle kushuka daraja baada ya miaka 16 katika ligi kuu ya Uingereza na sasa Newcastle itaungana na Middlesbrough na West Bromwich Albion kucheza ligi daraja la kwanza mwakani. Newcastle United ilishindwa kuwika mbele ya Aston Villa na kukubali kipigo cha bao 1-0 na hivyo kuhitimisha miaka yao 16 katika ligi kuu ya Uingereza.

Newcastle iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kubaki ligi kuu ya Uingereza ikitegemea Hull City itafungwa na Manchester United na wao kushinda mechi yao na Aston Villa.

Mambo yalikuwa si mambo pale Hull City ilipobanjuliwa 1-0 na Manchester na Newcastle nayo kushindwa kuitumia nafasi hiyo na matokeo yake na wao pia wakalala 1-0 kwa goli la kujifunga la Damien Duff katika dakika ya 38.

Damien Duff alijifunga baada ya kumpoteza maboya golikipa wake Steve Harper wakati akijaribu kuzuia shuti la Gareth Barry.

Middlesbrough nayo iliingia uwanjani ikiwa na matumaini duni ya kubakia ligi hiyo mwakani na kuonyesha kiwango duni mbele ya West Ham kilichopelekea walale 2-1.

Hakuna mtu aliyekuwa na furaha leo baada ya filimbi ya mwisho ya kumalizika kwa ligi ya Uingereza kama kocha wa Hull City, Phil Brown .

Pamoja na kwamba Hull City ilikuwa imelala 1-0 kwa Manchester United, Phil Brown alishangilia utadhania amechukua kombe la ligi ya Uingereza baada ya kupata uhakika kwamba timu yake itacheza kwa mara nyingine ligi kuu ya Uingereza mwakani.
 
kuteleza si kuanguka,we now retreat in the trenches of the championship,regroup,rearm and fight our way back into the premiership-it is a sad day indeed but the infighting was destined to led us down-NEWCASTLE FC will be back to claim her rightfull place in english soccer-sooner or later the sleeping giant will wake up and the world will have to take notice
 
Tatizo la New Castle FC ni kufukuza makocha na kwa hiyo kutokuwepo continuity. Kwa miaka 10 (zile enzi za Gullit) wamefukuza makocha 12. Washabiki wake nao hawana subira.
 
kuteleza si kuanguka,we now retreat in the trenches of the championship,regroup,rearm and fight our way back into the premiership-it is a sad day indeed but the infighting was destined to led us down-NEWCASTLE FC will be back to claim her rightfull place in english soccer-sooner or later the sleeping giant will wake up and the world will have to take notice
iwe bojo hizi methali zingine zishapitwa na wakati.....wameshaanguka hao newcastle
 
wewe yoyo,mimi hizi methali nimejifunza ukubwani,ndio maana i am still fascinated- anyway the mighty Newcastle will be back

Ofcourse they will be back! Mambo ya kawaida tu kushuka daraja. Sio kama hapa kwetu timu ata zikiwa mbovu vipi hazishuki daraja asa Simba na Yanga
 
Naona safari ya newcastle kurudi itategemea kama hao mastar alikuwa nao wataendelea kupambana na kubaki na timu kama ilivyokuwa kwa Juventus...laa wakihama timu itakuwa ndoto kwa sasa Kurudi kwenye premier league..kama mambo ya Leeds Utd
 
HAO mastar wote itabidi waondoke,they dont deserve to wear the newcastle colours.The man Allan shearer will build this team from a scratch.this team will never fold like Leeds united for NUFC haina deni
 
Wakajipange vizuri...ata Manchester United nao walishawahi kushuka daraja lakini walivyorudi mziki wake mnaujua.
 
kuteleza si kuanguka,we now retreat in the trenches of the championship,regroup,rearm and fight our way back into the premiership-it is a sad day indeed but the infighting was destined to led us down-NEWCASTLE FC will be back to claim her rightfull place in english soccer-sooner or later the sleeping giant will wake up and the world will have to take notice

Hapo ipo kazi kubwa kupanda after next season. Shear hana experience. Great players dont always make great managers!
 
Back
Top Bottom