New Song: TANESCO na Kamati; Hapo vipi wakuu?

Mkuu Nyambala,

Katika members ambao nimegundua wamekuwa makini na kilichoandikwa humu mmojawapo ni wewe. Umechukua muda kupitia ili kutenda haki kwa pande zote.

Niliposoma hiyo sehemu mwenyewe nilicheka sana... That made my w/end off course!

Kuhusu Serukamba sijamwelewa kabisa mpaka mwisho wa doc hii.

I see, haya mambo magumu kueleza... Nimefurahi kuwa ulipata muda wa ku-google na kupata data za "Lamai International", ni wachache wanaopoteza muda kufuatilia kila kitu.

Once done, come back with more comments mkuu wangu.

Tupo ukurasa mmoja mkuu wangu.

Mkuu Companero, nadhani angalia possibility ya kuirekebisha PDF reader yako... Doc iko OK kabisa

Huyu Serukamba, ameamua kuwa kucheza Devil's Advocate kwa sababu anazozijua yeye.
 
Pamoja na kwamba hakuna uwazi ni nani andaiwa kiasi gani baina ya hawa wadeni sugu wakubwa, naamini out of Jeshi, Polisi na Zanzibar- mdeni mkubwa kabisa atakuwa Zanzibar kwa kuwa hapa unaongelea supply ya umeme kwa 'nchi' nzima. Hivi ni kwanini tunawanyenyekea hawa Wazanzibari kiasi hiki? they know huu umeme haupatikani bure, unanunuliwa, sasa kwanini tuendelee kuvumilia nyodo zao? Wanataka walipe bei wanayotaka wao, hawatambui bei zinazopangwa na EWURA- na cha ajabu bado tunawapa tu umeme wetu! Have we gone crazy? Mimi naomba kama kuna uwezekano Zanzibar as kisiwa chenye serekali yake itafutiwe jiluku lake kubwaaa wafungiwe ili wawe wanalipa in advance. Wakileta jeuri kulipa deni lilopo tena kwa bei tunayotaka sisi wenye umeme- tuwakatie tu kama mteja mwingine yeyote sugu. Hii ni biashara na si siasa.

Katika mikakati ya kukusanya madeni naona TANESCO wanaplan kuintroduce matumizi ya LUKU Dar nzima lakini mimi binafsi naamini this is not fair on customers. Ningekubaliana nao kama matumizi ya LUKU yangekuwa ni compulsory kwa wadeni sugu na wateja ambao wanasumbua kwenye malipo. Clean customers wawe na option ya kutumia Bill au izo LUKU kama wanataka na siyo kuwa forced. Adha za LUKU ni nyingi, foleni kwenye vituo ambavyo to be honest vipo vichache sana kulinganisha na idadi ya wateja na sijui vita cope vipi kama Dar nzima itakuwa ikitumia LUKU. Pia kuna kero za umeme kukuishia usiku wa manane, these things happen. Kwanini wasifanye tu kama kwenye mobile phones- ni juu ya mteja kuwa na prepaid phone au pay as you go. Na if they think watu hawaibi umeme kwenye LUKU they are dead wrong.

Am not happy pia na idea ya kuunganisha wateja wa mita 30 bure halafu mzigo wa malipo watwishe existing customers! Kwani wateja wa sasa si walilipa hiyo connection fee? Sasa cost za wateja wapya kuunganishwa zikiwekwa kwao si watakuwa kama wanalipa mara mbili japokuwa ni kiasi kidogo? Kila mtu abebe mzigo wake nasema, kama wanataka kuwaunganishia free watafute source nyingine ya ku finance hilo zoezi lakini sio wateja waliopo.

Nafikiri pia migodi ni potential source ya mapato makubwa kama TANESCO watakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha na kuwauzia. Kwenye mikataba ambayo serekali inaingia na makampuni ya uchimbaji madini kipengele cha kuwabana wawe wakinunua umeme wetu kiingizwe.

Mwisho, I must say- nimeshangazwa na makosa yaliyopo kwenye hii document, hii ni very sensitive document tena ya chombo nyeti cha nchi yetu. Sijui kama ni typing error au ni umbumbu wa secretary aliyeandika hizi minutes. Na kwanini basi hata mwenyekiti au mjumbe yoyote hakuifanyia proof reading kabla haijatufikia? Kuna statement ambazo zina utata, kuna mahali wanasema kuna transfoma 850 nchi nzima na 4,400 zipo Dar peke yake, na nyingine inasema "zinahitajika dola 200 kukarabati miundo mbinu ya Dar!" Na nimekoma na kiswanglish kilichopo hapa, japokuwa english ni kuchovyachovya tu lakini imevunjwa kwa kwenda mbele, ukipitia humo utaona maneno kama 'bare in mind' which I believe should have been bear in mind, kuna 'negotiate power'- shouldnt it be 'negotiating'? kuna kali nyingine- ".... kitu kimeni- effect'!(affect), "to be franked(frank)", "very crusial(crucial)", "this guys (these)", "cross revenue (gross)", etc.
 
Nafikiri hii ni part ya yule mwali ngoja nikae vizuri maana sijaingia tangia ijumaa si mnajua box tena
 
Kweli swala la umeme Visiwani..hawa wenzetu wabebwe hadi lini? Na kwa maslahi ya nani?

Hawaitambuai EWURA na kwa hiyo wanalipa wanachopenda?

Kwa nini serikali ya Muungano iwalipie deni??

Kama hawataki kulipa market price..wakatiwe umeme!

Kama ni umaskini Visiwani hata Singida, Mtwara napo kuna maskini na wanalipa sawa!

This is not fair!!
 
Kweli swala la umeme Visiwani..hawa wenzetu wabebwe hadi lini? Na kwa maslahi ya nani?

Hawaitambuai EWURA na kwa hiyo wanalipa wanachopenda?

Kwa nini serikali ya Muungano iwalipie deni??

Kama hawataki kulipa market price..wakatiwe umeme!

Kama ni umaskini Visiwani hata Singida, Mtwara napo kuna maskini na wanalipa sawa!

This is not fair!!

Yote haya ni kwa sababu ya kuingiza politics kwenye biashara kaka, watu wanaogopa 'political consequences'. Tuwakatie umeme tu, wiki moja gizani am sure watatafuta hiyo hela na kutulipa deni letu.
 
Asante mkuu inv. kwa kuweka hii doc. hapa! Sijaisoma yote...lakini nitaivulia shati jioni!

Kwa kifupi nimeiona sehemu mojawapo ambayo Mh. Zitto alianza kupotezwa kuhusiana na ununuzi wa mitambo ya Dowans...ukiangalia uk.17 na 18 Dr. Idrisa ndipo alipoigandamiza hoja ya kununua mitambo ya Dowans kwa kutumia visingizio vya;

a) muda (time limit) kama mitambo mipya kama hiyo hiyo ingeagizwa,

b) Upungufu wa umeme unaotarijiwa(kuanzia sept 09)

c) Upya wa mojawapo ya mitambo hiyo (ule wa 46MW) kwamba umefanya kazi 800 hrs

b) Uwezo wa mitambo hiyo.....inaweza kufanya kazi kwa miaka 10-11 bila kufanyiwa overhaul na kama inkifanyiwa overhaul sasa itafanya kazi kwa 20yrs bila matatizo

Hapa mi naona ndipo Zitto alipoanza kupotezwa mwelekeo kwenye suala hili!

Kitu kingine ambacho sijakipenda, niuchanganywaji wa lugha.....si Dr. Idrisa, si Mwenyekiti wa kamati, si wajumbe wa bodi ya Tanesco, si wajumbe wa kamati...kila mmoja alipota nafasi ya kuuliza swali au kuzungumza alichanganya lugha...anaongea neno moja, mawili, kwa kiswahili,mara la tatu ni kiingereza, nne kiswahili nk hii inafanya ufuatiliaji wa mtiririko wa hoja zao kuwa mgumu sana.....pengine hili tutalijadili sehemu nyingine!

Zaidi ya hilo....nitarudi kuchangia nikimaliza kuzoma karabasha lote!
 
Lugha ndugu yangu unajua kama ukipata PhD ktk ya Uchumi Kiingereza.. halafu ukaambiwa utoe mada 'technical' kwa Kiswahili hata kama ni mimi naona ingeniwia vigumu!

Wewe next level hiyo ripoti yote ungeweza kuijadili kama Zitto au Rashid kwa Kiswahili tu Mkuu??

Basi mimi nakuvulia kofia Mkuu na yawezekana huenda basi umeboboa ktk Kiswahili!
 
Invisible,

Nashukuru kwa kuweka hapa hii nyaraka (umepataje?). Nyaraka za Kamati za kimahesabu kama hii huwa ni siri ya Bunge.

1. Hii ni Hansard na sio minutes. Hivyo hakuna katibu anayeandika. Kila mbunge hurekodiwa anachosema na baadae transcription hufanyika. Sasa matamshi ya maneno huwa yanakosewa sana kutokana na transcriber na ndio maana final version in ile iliyohaririwa na msemaji mwenyewe. Hii haijahaririwa.
2. Kuna wachangiaji hapa walisema na hata baadhi ya magazeti kusema kamati haikuamua nilivyosema. Hii ndio ushahidi wa kibunge kuonesha kamati iliamua nini. Sasa mtatoa hukumu kama niliyokuwa nasema ni yangu au ni ya kamati. Nashukuru sana Invisible kwa kazi hii. Ndio maana JF ni mwisho wa maneno maana haki hata ichelewe namna gani, hatimaye itatendeka tu.
3. Kuchanganya lugha - hili ni tatizo letu kubwa sana. Tusameheeni tu.
 
duuuhhhh gharama zao za uwekezaji ni balaaaa....kwani TANESCO lina uwezo wa kusustain hizo garama kwa mwendo huu...??? IPTL garama kuiiconvert na buyout ni 9bn!!!!

sasa kwa tabia na uwezo wa wateja wao wadogo walio wengiiii watawezaaaaaa.....
tambua pia kwamba ofisi za umma nazo ni wakwepajiii????

TANESCO hapo ni sanaaa kwa kwenda mbelee jamani....bora liende.

shirika liuzweee haraka tuwe wadau na share tununueeeeee.....
 
Mimi kwa upeo wangu mdogo naona kuna kiza kizito sana kwa swala la Dowans. Inakuaje kwenye optiond zilizokua documented kuwe na Option ya IPTL tu halafu wanapokuja kwenye kikao wanatumia muda mwingi kujadili option ya Dowans ambayo haikuwepo kwenye first paper?

1. Kwanini waliacha kuijumuisha kama mojawapo ya options
2. Je haikuachwa makusudi?
3. Kama ni clear option, kwanini waliogopa kuijumuisha?
4. Kamati inakubali vipi kujadili off topic item kama one of the option?
5. Ukifanya Investment appraisal kwa hizo option Mbili IPTL and Dowans, Huoni kuwa IPTL is more attractive deal from savings
6. Kwanini IPTL isiwe ndo kipaumbele cha kwanza sababu kwanza kila mwezi twalipa 3.2billion ka c.charge?
7. Who are behind IPTL?
 
Ukiangalia hii nyaraka, utagundua kwenye kikao chenyewe umeme uliwakatikia wajumbe!

Interesting indeed
 
Back
Top Bottom