New revelation, Dowans in huge debt

Wakuu mliopo Brela.

Who are Directors wa Dowans?

FP... mbona tumesema mwali atafunuliwa kaka... hii ni mwanzo tu.. tulipopinga tulikuwa na sababu! Kununua Majenereta "ya" dowans hakuhusiani kabisa na tatizo la nishati. Hapa ndipo Zitto alipopotea...

Issue kwangu mimi na wengine ni Dowans the company.... nawaambia wenzenu washaandaa kwa kuhamia kabisa... nyie subirini.. it is huge.. will send shockwaves.... and it is beautiful to. Wengine kwenye hili we are putting everything on the line; mfano wa Goliathi na Daudi wala hauelezei kilichoko mbele yetu!!

Vinzi vimetawanyika hadi Canadian Royal Bank!!!!! (why..???) well.. msubirini mwali!!
 
Issue kwangu mimi na wengine ni Dowans the company.... nawaambia wenzenu washaandaa kwa kuhamia kabisa... nyie subirini.. it is huge.. will send shockwaves.... and it is beautiful to. Wengine kwenye hili we are putting everything on the line; mfano wa Goliathi na Daudi wala hauelezei kilichoko mbele yetu!!

Vinzi vimetawanyika hadi Canadian Royal Bank!!!!! (why..???) well.. msubirini mwali!!

Mkuu MM......unaonekana ''album'' yako ya Dowans imeshakamilika, if yes, we can't wait anymore, mwaga vitu tunataka kuwazika kabisa hawa ''MAJINI''!
 
Nasikia RA anakusudia kuuza share zake za Vodacom aondoke nchini. Ila serikali kupitia TCRA wamekataa kuuzwa kwa share hizo kwa mwekezaji wa nje (kuzingatia sheria ya uwekezaji). Kama kuna mtu mwenye taarifa zaidi atusaidie katika hili.

Nadhani mambo yamekuwa magumu kwa mtu huyu.
 
FP... mbona tumesema mwali atafunuliwa kaka... hii ni mwanzo tu.. tulipopinga tulikuwa na sababu! Kununua Majenereta "ya" dowans hakuhusiani kabisa na tatizo la nishati. Hapa ndipo Zitto alipopotea...

Issue kwangu mimi na wengine ni Dowans the company.... nawaambia wenzenu washaandaa kwa kuhamia kabisa... nyie subirini.. it is huge.. will send shockwaves.... and it is beautiful to. Wengine kwenye hili we are putting everything on the line; mfano wa Goliathi na Daudi wala hauelezei kilichoko mbele yetu!!

Vinzi vimetawanyika hadi Canadian Royal Bank!!!!! (why..???) well.. msubirini mwali!!

Mkuu, weekend itakuwa ndeeeefu sana kama huyu mwali hatoki..ila utakapomtoa, kila mtu afurahi maana kwa kweli jinamizi la Rostam ni zito sana
Nilinusa nusa mahali, nikaambiwa share za Caspian alishaanza kuziuza kwa Chama Tawala..
 
Naomba kuuliza,

Hiyo mitambo ingeuzwa kwa TANESCO. yaani miliki ingekuwa transfered kwa TANESCO...

Je benki zingemdai nani? assuming DOWANS asingelipa deni, maana tunabuni tu... what if DOWANS angelipa deni lake? hata hivyo ili mambo ya noge...

Tuseme dowans hawajalipa deni... lakini mitambo imenunuliwa na TANESCO. na ikawa chini ya TANESCO.

Benki zinamdai nani TANESCO ambaye hayuko kwenye vitabu vyao... au DOWANS ambaye ndiye mdaiwa?

Sijui hapa kwenye issue ya dhamana but... naanza kuona huenda issue ingeiangukia DOWANS zaidi,,, kuliko TANESCO.
 
napata wasiwasi mkubwa sana na wanasiasa aina ya ZITTO!

kwa namna nilivyokuwa namuelezeaa zitto kabla ya hili ya kulibariki hili swala la dowans,NACHELEA KUSEMA KWAMBA zitto amepoteza mwelekeo wake KISIASA!

POLE SANA ZITTO!
 
napata wasiwasi mkubwa sana na wanasiasa aina ya ZITTO!

kwa namna nilivyokuwa namuelezeaa zitto kabla ya hili ya kulibariki hili swala la dowans,NACHELEA KUSEMA KWAMBA zitto amepoteza mwelekeo wake KISIASA!

POLE SANA ZITTO!

Yaani saga hili limeweka bayana kwa wanaotaka kuona true colours za wanasiasa. Hata wakijifanya wanapinga kitu, siku wakiwa kwenye the same position usitegemee miujiza. Wapinzani walipaswa kusimama against Zitto iwapo kweli wanaweka maslahi ya Taifa mbele ya maslahi ya vyama vyao. Dr. Slaa amekuja hapa na kumtetea Zitto, kujaribu kuwadanganya wana JF kuwa official decisions za kamati ya Zitto hazijulikani etc. Na mpaka sasa hakuna hata mpinzani mmoja aliyetamka hadharani kuwa Zitto kachemka. ''mwenye macho haambiwi ona''.
Kwanza Zitto anapaswa kuja JF kuomba radhi kwa kutotoa taarifa sahihi juu ya haya:
1. Kamati yake haikuiita TANESCO na kuihoji bali hiyo kamati ndio iliyoalikwa kwenye semina na TANESCO kwa gharama za TANESCO.
2. Maamuzi aliyoielezea JF kuwa ni ya kamati hayapo kwenye minutes za katibu wa kamati kwa hiyo ni maamuzi yake binafsi.
Zitto amediriki kudanganya hata hapa nyumbani kwa ''great thinkers'' hii haiwezi kuachwa hivihivi.Kijana ni lazima aombe radhi kwa heshima ya JF.
 
Kama Zitto asingeweza kuja hapa jamvini na kuandika mwenyewe angaliweza kujitetea kuwa alikuwa quoted out of context na kwa kuitumia barua aliyoiandika kwa waziri wa nishati na madini angejivua katika hili.Worse enough alifanya mahojiano na ITV ambayo yataendelea kubaki kama ushahidi...Pia alituambia kuwa "sheria si msahafu".
I just imagined kama utetezi huo wa kununua mitambo chakavu ungekuwa umetolewa na "waziri kijana",believe me zingepazwa sauti humu ndani za kuwajibika...

Huyu ZITTO mbona mweupe tu.. hakuna kitu pale.. always time tell the truth, kujitetea mara nyingi anasema uliza enzi zangu nikiwa chuo.. hizo ni siasa uchwala na kuhusu hili suala la DOWANS nasikitika kusema kwamba Tanzania hatuna cha upinzani wala chama tawala.. kinchofanyika ni abiria chunga mzigo wako. wooote ni wajasiliamali kama alivyokuwa anahamasisha mzee kipara enzi zake.
 
Yaani saga hili limeweka bayana kwa wanaotaka kuona true colours za wanasiasa.

Kwa hapa nakubaliana na wewe. Ombi kwetu ni kwao kujifunza kutokana na yaliyomkuta Mh. Zitto.

Hata wakijifanya wanapinga kitu, siku wakiwa kwenye the same position usitegemee miujiza. Wapinzani walipaswa kusimama against Zitto iwapo kweli wanaweka maslahi ya Taifa mbele ya maslahi ya vyama vyao. Dr. Slaa amekuja hapa na kumtetea Zitto, kujaribu kuwadanganya wana JF kuwa official decisions za kamati ya Zitto hazijulikani etc.

Taifa kwanza, halafu vyama vitafuata baadaye hili ndilo fundisho letu hapa.


Na mpaka sasa hakuna hata mpinzani mmoja aliyetamka hadharani kuwa Zitto kachemka. ''mwenye macho haambiwi ona''.
Kwanza Zitto anapaswa kuja JF kuomba radhi kwa kutotoa taarifa sahihi juu ya haya:
1. Kamati yake haikuiita TANESCO na kuihoji bali hiyo kamati ndio iliyoalikwa kwenye semina na TANESCO kwa gharama za TANESCO.

Hivi sasa hii ni obvious na wala haihitaji darubini au maelezo tena. Good observation ZeMarcopolo.

2. Maamuzi aliyoielezea JF kuwa ni ya kamati hayapo kwenye minutes za katibu wa kamati kwa hiyo ni maamuzi yake binafsi. Zitto amediriki kudanganya hata hapa nyumbani kwa ''great thinkers'' hii haiwezi kuachwa hivihivi.Kijana ni lazima aombe radhi kwa heshima ya JF.

ZeMarcopolo,
Tusimhukumu Zitto kwa kauli zake juu ya DOWANS, tumpe nafasi ya kujisafisha kwani aliyofanya kwa Taifa ni mengi kuliko alilochemsha. Let's give him another chance, but keeping a strong watchful eye on him.
 
What Dowans exactly used to secure $75m bank loans

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

ALL assets owned by Dowans Tanzania Limited, including its 100-megawatt turbines and its fleet of motor vehicles and spare parts, were surrendered by the company as security for obtaining loans amounting to $75m (over 100bn/-) from at least two major commercial banks.

According to legal documents listing the controversial company's bona fide belongings and attached by the banks as collateral for the loans, the five second-hand turbines now lying idle at Ubungo in Dar es Salaam were also given up to acquire the credit line.


The turbines, as described in the documents seen by THISDAY, are four trailer-mounted General Electric (GE) TM-2500 gas turbine power generator sets, and one LM-6000 PD turbine also manufactured by GE.

Each of the mobile TM-2500 power generator sets produces around 20MW of electricity, while the larger LM-6000 PD set is capable of producing up to 48 megawatts.

The Dowans company inventory list submitted to its lenders also includes two step-up transformers for outdoor installation, plus various spare parts for the electrical equipment.

The documents show that Dowans Tanzania Ltd pledged all these assets - both movable and immovable to secure the hefty loans from Barclays Bank and Stanbic Bank, both of which have branches in Tanzania.

It is understood that the company also placed the turbines, vehicles, transformers, tools and all other remaining assets under mortgage to hasten approval of the credit facilities.


The certificates of indebtedness signed by Dowans show that the company gave up to the banks its rights to ''all entitlements which it may at any time and from time to time have to the payment of any money.''

Our investigations have established that during 2007, Dowans was awarded several loans worth a total of $55m from Barclays Bank alone, and another $20m from Stanbic Bank.

The actual bank branches that extended the loans to Dowans were Barclays Bank Mauritius, Barclays Bank Tanzania (Limited), and Stanbic Bank Tanzania (Limited).

The latest revelations come at the height of an ongoing heated public debate over the merits and demerits of a recent joint bid by Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) Managing Director Dr Idris Rashidi and Energy and Minerals Minister William Ngeleja to justify a government purchase of the Dowans' second-hand turbines.

It has yet to be established if either Rashidi or Ngeleja or both - were aware of the massive $75m debt being carried by Dowans as a company during their relentless and sustained push for a deal to buy the turbines at a much-inflated price of $60m (approx. 90bn/-).

In the circumstances, however, it becomes quite clear that if the plan to buy the Dowans power turbines were to ever succeed, someone either TANESCO or the government would end up inheriting the Dowans debt.
 

ALL assets owned by Dowans Tanzania Limited, including its 100-megawatt turbines and its fleet of motor vehicles and spare parts, were surrendered by the company as security for obtaining loans amounting to $75m (over 100bn/-) from at least two major commercial banks.



WanaJF,
  1. Kama TANESCO imeizuia mitambo kwa ajili ya malipo yake wanayowadai DOWANS, wakati mitambo tayari imeshawekeshwa kwa mabenki, sasa TANESCO wanashikilia mitambo au wanawasaidia DOWANS storage?
  2. Assuming serikali ilikuwa kipofu kiasi cha kutokujua kuwa DOWANS washaishia na kuwachia mabenki mitambo, kwa nini wasianzishe uchunguzi hivi sasa na kushirikiana na InterPol ili kuokoa malipo yao?
 
WanaJF,
  1. Kama TANESCO imeizuia mitambo kwa ajili ya malipo yake wanayowadai DOWANS, wakati mitambo tayari imeshawekeshwa kwa mabenki, sasa TANESCO wanashikilia mitambo au wanawasaidia DOWANS storage?
  2. Assuming serikali ilikuwa kipofu kiasi cha kutokujua kuwa DOWANS washaishia na kuwachia mabenki mitambo, kwa nini wasianzishe uchunguzi hivi sasa na kushirikiana na InterPol ili kuokoa malipo yao?

Duh yaani hapo umepoint out kitu cha maana kabisa.Inawezekana hawa jamaa TANESCO wanawatunzia mali hiyo bila kuwatoza storage charges basi.Kwa sababu kisheria sijui TANESCO wana encumbrance gani katika mitambo hii kama itauzwa kufidia madeni ya mabenki ambayo tayari yameshakuwa "secured creditors"?

Kweli mchezo huu ulipangwa na ukapangika...
 
Huyu ZITTO mbona mweupe tu.. hakuna kitu pale.. always time tell the truth, kujitetea mara nyingi anasema uliza enzi zangu nikiwa chuo.. hizo ni siasa uchwala na kuhusu hili suala la DOWANS nasikitika kusema kwamba Tanzania hatuna cha upinzani wala chama tawala.. kinchofanyika ni abiria chunga mzigo wako. wooote ni wajasiliamali kama alivyokuwa anahamasisha mzee kipara enzi zake.

Hivi msumari ukiugongelea kwenye ubao ukaingia wote, unazidi kuugongelea ili kiwe nini? unataka kuvunja ubao? HIli suala ni la Dowans, kwamba Zitto alipotea/alifanya makosa ya kisiasa au hata mkakati mbona halina ubishi. Lakini kujaribu kuendelea kusema "zitto, hakuna kitu" au "Zitto hivi au vile" ni kukwepa mjadala.

Hamuonekani kukerwa na Dowans, Tanesco, wizara ambavyo ndio wahusika wakuu wa suala hili. Mnasemaje kuhusu Dowans, Ngeleja, Dr. Idris, Mmiliki wa Dowans?

Issue ni chembe ndogo tu katika mjadala huu and if you ask me an irrelevant one!
 
Jamani tujiulize unajua unapokwenda kukopa pesa hasa ukiwa na dhamana kama hizi ni mitambo na spare parts ambazo value yake inaweza kuisha kadri muda unapokwenda ni vigumu sana mabunki kukuamini mpaka awepo mdhamini anayeeleweka.

Je serikali haikujiweka kama mdhamini wa Dowans wakati anaenda kukopa pesa hizi benki?

kama ilidhamini itakuwa ni big loss kwa nchi yetu maana hawa jamaa watayaacha majenereta yao na serikali ikadaiwa kwani ni mdhamini (kama kweli alidhamini)
 
Hii nimeitoa kwenye Tanzania Daima la 12/03/09 na Kama Haifai hapa yaweza kuhamishwa kunako husika. Pia nimeweka Comments za Wananchi etc


Mitambo ya Dowans: Mhadhiri amtetea Zitto
• Aonya wanajipalia makaa ya moto CCM


na Ratifa Baranyikwa




MHADHIRI Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameeleza kusikitishwa na mwenendo wa mjadala unaohusu uamuzi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kununua mitambo ya Dowans kuelemewa na hoja zenye utashi wa kisiasa zaidi kuliko utaalamu.

Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalumu ya njia ya simu jana, mhadhiri huyo, Dk. Azaveli Lwaitama, alisema wanasiasa wanafanya makosa kujadili ajenda nzima ya kununua au kutonunua mitambo hiyo kwa kutafuta kujua wamiliki wake, badala ya kuangalia mahitaji ya nishati hiyo kwa taifa.

Lwaitama, mmoja wa wahadhiri ambao pia ni wanaharakati wa masuala ya kijamii na maendeleo, alisema alikuwa akiunga mkono uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ambayo kimsingi ilikubaliana na hoja ya TANESCO ya kuhitaji mitambo ya kufidia pengo la mahitaji ya nishati yanayoikabili nchi.

Mwanazuoni huyo alieleza pia kuungana na mtazamo wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo, wa kuunga mkono pendekezo lenye utashi wa kitaaluma la Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idris Rashidi.

Akifafanua, Dk. Lwaitama ambaye ni mhadhiri wa falsafa katika chuo hicho kikuu kikongwe nchini, alisema hoja zinazotolewa na wanasiasa wengine kama Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe, zimekosa maelezo ya kitaalamu dhidi ya mitambo hiyo.

“Nimesikiliza hoja zilizotolewa na Mwakyembe na Sitta. Sijamsikia hata mmoja anayetoa maelezo ya kitaalamu na badala yake wamekimbilia kutafuta ni kina nani wanamiliki mitambo hiyo, mtazamo ambao naamini hauko sawasawa,” alisema.

Lwaitama ambaye alikiri ukweli kwamba mitambo hiyo ina historia ya ufisadi unaoiunganisha na Kampuni ya Richmond, alisema ukweli huo bado hauwezi kufuta hoja za kitaalamu na za kimazingira kuhusu kufaa kwa mitambo hiyo kununuliwa na TANESCO katika misingi ya uzima wake, bei yake na uhalisia kwamba ipo hapa nchini na si ya kuagiza au kuanza kuitafuta nje.

“Ni kweli Dowans ina mkono mchafu wa Richmond na kuna uwezekano wamiliki wake wanaweza wakatumia fedha watakazopata kwa kuuza mtambo huo kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani, na pengine ndicho wanachoogopa kina Mwakyembe.

Hata hivyo, ukweli huo hauondoi hoja za kitaaluma zilizotolewa na Dk. Rashidi pasipo kuangalia rekodi yake ya urafiki wake na watu kama Rostam Aziz, au Rais Jakaya Kikwete,” alisema Lwaitama.

Akimzungumzia Zitto, msomi huyo alimwelezea kuwa mwanasiasa wa kizazi kipya, ambaye anapothibitisha jambo la kitaalamu yuko tayari kulisimamia kwa nguvu hata kama kwa kufanya hivyo anaweza kuiweka rehani heshima yake ya kisiasa na kijamii.

Akiendelea kufafanua, alisema kuwa malumbano ya sasa kuhusu ununuzi wa mitambo hiyo ya Dowans yanawakumbusha Watanzania kusoma kitabu cha ‘Tujisahihishe’ kilichoandikwa na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema katika kitabu hicho Nyerere alitoa mfano wa mtu mwenye kibyongo anaposema kwamba, 2 x 2 =4, wanaomsikiliza wanapaswa kutafakari ni kwa njia zipi kalipata jibu hilo, badala ya kuangalia kibyongo chake.

Kutokana na hilo, alisema katika mjadala huu wa sasa, Zitto ameonyesha dhahiri kufikiri kisomi zaidi kuliko kisiasa, akizingatia mahitaji yaliyopo ya kuinusuru nchi kuingia gizani, tofauti na ilivyo kwa kina Mwakyembe, aliodai wanaliangalia suala hili kwa kuogopa kuharibikiwa.

“Ni jambo la hatari kwamba, kina Mwakyembe na Sitta wanaogopa wakikubaliana na hoja za kitaalamu za TANESCO, wataharibikiwa katika vita yao ya ufisadi waliyoidaka kutoka CHADEMA…watu hawa wako tayari Watanzania wabebeshwe mizigo kwa sababu tu ya kuogopa wasije kwisha kisiasa.

“Zitto yeye ameweka masilahi ya taifa mbele kuliko kuendeleza malumbano na makundi… mitambo hiyo ipo katika ardhi yetu na hesabu zilitolewa na kamati yake inaonyesha ni jinsi gani tunavyopata hasara, hivyo ni bora kununua mitambo,” alisema.

Alisema ingawa ni ukweli kwamba kununua mitambo ya Dowans kunaweza kuonekana kuwa ni ukora, uamuzi huo kimsingi unaweza kusadia kumnusuru mlipa kodi.

“Ninachoamini kama unajua huyu ni shetani lakini ana kitu muhimu, ni bora kuangalia kile kitu muhimu kuliko kuangalia ushetani wake,” alisema Lwaitama.

Alisema hoja ya kuwatafuta wamiliki kwa sasa haina maana, kwani serikali inawajua, jambo alilosema, ubishi wa sasa wa kina Mwakyembe na Sitta unawaweka katika hatari ya kuja kukosana na Rais Kikwete na serikali yake siku za usoni, hasa iwapo nchi itaingia gizani.

“Hawa jamaa pengine hawajui kwamba kwa jinsi mambo yalivyo ndani ya chama chao, wanatafutwa kweli kweli na nchi itakapoingia gizani wakati wa kipindi cha karibu na uchaguzi kwa mfano, wao ndio watakaonyoshewa vidole,” alisema.

Akiendelea alisema, malumbano ya sasa yanapaswa kuwakumbusha wanasiasa kitabu cha ‘The Audacity of Hope’ kilichoandikwa na Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye katika sehemu moja alisema wanasiasa wa zamani walikuwa wakiendekeza ubishi badala ya kutafuta njia za kutafuta ufumbuzi wa matatizo.




juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 71 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hata wakati wa Richmond mafisadi walileta hizihizi za kwamba wananchi tusiangalie kampuni tuangalie mitambo matokeo yake tumeyaona. Huyu Lwaitama anataka kuganga njaa yake kwa Rostam tu ili nae awekwe kwenye payroll. Na mtasajiliwa wengi sana mwaka huu na kuuza utu na heshima zenu.

Kama kila kitu ni kuangalia kiutaalam tu bila kufuata sheria halali na kuvunja kanuni, hakuna haja ya kuwa na sheria wala mahakama, sababu hata kibaka anaweza kujitetea kwa kusema kitaalam alikua hajala na angeweza kufa, hivyo alilazimika kuiba ili apate kula asife. LWAITAMA TULIKUA TUNAKUHESHIMU SANA KUMBE NAWEWE GALASA, UNATAKA KUJIPENDEKEZA KWA ******* LA KIIRAN. NJAA ITAKUUA UZEENI. WATANZANIA SI MABWEGE TENA!

na Ngosha, Dodoma, - 12.03.09 @ 11:33 | #14461

Kuwahukumu kina mwakyembe jumla ni makosa kwa sababu issue ya ownership ni muhimu sana kwenye manunuzi makubwa kama haya yanayohusisha billion of tax payers money.

Kumtetea Zitto Kabwe 100% nayo ni kosa sababu mbali na urgency ya mitambo hiyo- haitoi excuse kwa upuuzi wa huko nyuma. Kosa ni kosa tu halifutwi na mahitaji ya dharura. Culture hii ya kutisana kwamba nchi itaingia gizani ni mbaya, ni kuwafunga watu midomo; acha tuingia kwenye hilo giza kwani si mara ya kwanza.

na john, arusha, - 12.03.09 @ 11:40 | #14462

NI LAZIMA TUWAJUE WAMILIKI WA DOWANS! KUNA USIRI GANI KATIKA HILO? MPAKA LINI NCHI ITAENDESHWA KIHUNI? HAYO MANUNUZI SI YA MTU BINAFSI, YANAMGUZA KILA MTANZANIA, KWA HIYO NI MUHIMU KILA HATUA YA MANUNUZI IJULIKANE KWA UWAZI KWA WATANZANIA.
KAMA SERIKALI HAITAKI TUWAJUE WAMILIKI WA DOWANS HAKUNA HAJA YA KUNUNUA HIYO MITAMBO. KILA JUHUDI IFANYIKE MITAMBO IAGIZWE BADALA YA KUPOTEZA MUDA KUJADILI DOWANS.
HOJA YA KINA ZITO HAINA MANTIKI YOYOTE, IMELENGA KUWATETEA WAMILIKI WA DOWANS WASIOTAKA KUJITAMBULISHA KWA WATANZANIA.

NAMTAFADHALISHA RAIS KIKWETE, UFISADI MWISHO! TUMECHOKA KUITWA MASKINI WAKATI NCHI NI TAJIRI.

na KINYONGA, TZ, - 12.03.09 @ 12:08 | #14466

Suala hapa siyo ubora au uchakavu wa mitambo ya "Richmond"kwa jina jipya la Dowans,bali ni skandali iliyoihusisha serikali na Richmond katika upatikanaji wa mitambo hiyo na malipo ya gharama ya umeme uliozalishwa kupitia mitambo hiyo!Infact,siyo Lowasa tu,ilitakiwa serikali nzima ya Kikwete ijiuzulu kutokana na sakata lile la Richmond!Ule ni Ufisadi,pure and Simple!Sasa wakina Lwaitama wasitake kuturejesha huko,hapana imetosha!I have always doubted the integrity of this "Professor" in all his deliberations aired live in local TVs!Hana Kitu huyu bwana.Yeye anadhihaki jitihada kubwa iliyofanywa na kina Sitta na Mwakyembe katika kuiokoa serikali ya Kikwete kuhusiana na kashfa hiyo ya Richmond?Kashfa moja ya serikali haifutwi kwa kubadilisha majina tu ya wamiliki baada ya udanganyifu ule kufahamika!Hivi kweli,hapa dunia nzima kuna mitambo ya Dowans tu peke yake?Lwaitama na akili zake bado hatambui nini madhara yake kurudia kuinunua mitambo ileile iliyomfukuzisha kazi waziri mkuu wetu?Hata kama ni Mitambo Mipya 100%?what stupid nonsense!

na kubwajinga bishoo, manzese UDSM,tanzania, - 12.03.09 @ 12:25 | #14469

wanaojiita wasomi wa TZ siku zote hamna kitu.Na kwa huyo mhadhiri wa falsafa ndio kabisa.Hayo ni matokeo ya kupoteza muda wote wa maisha kukariri nadharia za watu wengine.Wasomi wetu wanashindwa kuhusisha hali halisi kwa kua wanaishi kwa nadharia za watu wengine.Njaa itakuua .Kaa kimya.Usituletee mambo ya kizamani.Tumeshachoka kuliwa

na DUNIA, TZ, - 12.03.09 @ 12:26 | #14470

ninashangaa kuwa na wasomi wa akina lwaitama, kabla nilikuwa ninamuheshimu mawazo yake ni ya busara, kumbe ni mawazo ya msukumo. mtu kama huyu angewepo wakati wakupigania uhuru angekua kibaraka. kutuambia kuwa wakoloni wametupa elimu kwahiyo waendelee kutonyonya bila kuangalia heshima yetu ya kujitawala. nchi yenye heshima hutawaliwa na sheria sio utashi.na vilevile ni mtu wa hatari anayechukua mstari mmoja wa kitabu bila ya kuangalia (theme)maudhui yake. Obama hakuzungumzia ukaidi kwa maana ya kupinga sheria au kuwa kibarakala wa mafisadi. Lwaitama the tip of the tongue does not cool the hot gruel.katika maelezo yako pia hujatoa hoja mnasaba ya sababu ya kununua mtambo.bali umekuwa devil's advocate.watanzania sio mabwege tena wanaweza kuchambua pumba na mchele. naomba samahani kama kuna kitu kitakuwa personal. vile vile naomba magazeti wasiangalie mrengo wa chama kinachowafadhili au mtu wanaompenda bali utaifa na heshima ya watanzania. vile vile tuangalie malumbano yasiwe kama mchezo wa kuigiza. watu wakatumia kujikweza kisiasa. Kwani nina uhakika CCM watakuja kutuuliza tena tunavaa namba ngapi ya viatu wakati washatuuliza na wakashindwa kutupatia. watanzania tuamke tusinunuliwe kwa kanga au fulana za pesa za kagoda. Malumbano ya ununuzi wa mitambo ya dawn ni mfano tosha wa kutokua na dira ya muda mrefu na na mipango ya kukurupuka yakiambatana na ushawishi na hoja za vitisho. Mpaka lini haya yataisha. we need to have long term planning. genious mind is nothing without a ....act. we will leave a scar on what we say but we will leave ....on what we do.

na karim.mussa, tanzania, - 12.03.09 @ 12:29 | #14471

Mimi nach shamgaa ni kwa nini zile bilioni 200 za vitambulisho zisitumike kununua mtambo ya umeme halafu vitambulisho baadaye?? Kuna nini hapa??

Hivi raisi kikwete kweli unashindwa kuona umuhimu wa umeme ulivyo zaidi ya vitambulisho ?? Kipi hapa ni dharula??

Angalia hao washauri wako, wana hoja binafsi akina membe!! na huyo mjinga Kyaruzi!

Mimi nasema na nakuamuru ndugu rais kikwete hebu ahirisha vitambulisho na wape pesa tanesco wiki ijayo waagize mitambo mipya kutoka US.

na Salome, bunda, TZ, - 12.03.09 @ 12:42 | #14479

SIASA MCHEZO MBAYA. HAITA UKIMWULIZA MTOTO MDOGO ATAKATA HIYO MITAMBO ISINUNULIWE. HAPA HAKUNA USOMI NA TATIZO WATU WAKISHA KUWA WASOMI WANAFIKIRI WATASIKILIZWA HATA KATIKA MAWAZO YASIYO NA LOGIC YOYOTE. NILIFIKIRI WASOMI NDIO WANGEKUA WA KWANZA KUZUIA HII ISSUE KWANI WAO NDIO TUNAMINI HATA MATH KICHWANI KIDOGO ZINAENDA. TANZANIA TUNAO UWEZO WA KUNUNUA MITAMBI MIPYA N MIZURI KULIKO HIYO TUNAYO PIGIANA KELELE ZA KIJINGA , TUNGEKUWA SASA TUNAUZA UMEME HATA NJE YA NCHI KAMA WATU WANGEKUWA NANAONA MBALI.


na FIKIRIKWANZA, Tz, - 12.03.09 @ 12:44 | #14481

ZITTO kachemka na hakuna kumtete ,alitaka kujionesha anajali wananchi kumbe sio. sisi wananchi tunataka kiongozi anaye ona future yetu sio naye tupa hongo leo kisha tuendelee na mishida milele.

na leo - 12.03.09 @ 12:48 | #14483

Huyu dactari wa wapi tena jamani mbona anaanza kujichanganya,anaposema hoja za akina Mwakyembe zimekosa utaalamu anamaanisha nini? utaalamu huo ni upi?je huyo zito hoja zake zina utaalamu gani? kwamba tutakuwa na janga la ukame?huo ndio utaalamu.Nachelea kusema huyu dactari ndiye aliyekurupuka bila ya kuliangalia hilisuala katika mapana yake halisi (BIG PICTURE),ameangalia hoja ya kukosa umeme kwa kuikataa mitambo ya Dowans tu.Hakuangalia tutakuwa tumevunja sheria ngapi?tutakuwa tumejidhalilisha kiasi gani na repucation yake internally and internationally,hakuangalia ubora wa mitambo hii na faida ya alternatives zilizopo (cost-effectiveness),hakuangalia ghalama ya mitambo hii na faida yake,ukilinganisha na kutafuta suluhihisho la kudumu na imara.

Yeye alichoona ni siasa tu,hakusikiliza wala kujituma kuchambua logic iliyojificha ndani ya siasa.Yeye kama mtaalamu wa philosophy anatakiwa awe wa kwanza kujua "the role of politics in development","the role of politics in changing people's behavior and culture",the role of politics in not only shaping but also directing and showing proper ways to liberation from emancipation of mind and physical slavery.

Hajafanya critical analysis ya responses reaction ya watanzania kwenye suala hili.Yeye ndiye anajiona anaweza kuona mbali kuliko asilimia 89% ya watanzania amabao wameshitukia uozo huu,achilia mbali waliosema hata kama ni giza bora tukae giza.Kwanza napenda kumuuliza hako kadaktari,sio kwamba nabeza doctorate yake,nabeza uchambuzi hafifu na mfu uliotolewa na aliyehodhi hiyo doctorate,nataka atwambie ni asilimia ngapi ya watanzania wanafaidi huu umeme,baada ya hapo ajibu hoja hii,kwa kutonunua mitambo feki ukame umesema utakuja baada ya kusikia tumekataa mitambo hii,je ni lini walijua jambo hili,je walipojua na huku wakifahamu fika kwamba mitambo hii ni feki na ina kesi walichukua hatua gani,Ofisi ile na wizarani wamejaa maingeneer maelfu walikosa kweli contingency plans ambazo ni more efficient,sustainable,free of conflicts and more productive zaidi ya kung'ang'ania mitambo.

Mpaka hapo nachelea kusema kama hawa ndio maprofesa wetu wa chuo kikuu,wenye uwezo finyu kuanalyze conflicting paradigm kama hii,basi tuendako na kizazi cha wasomi tutakachokuwa nacho kitatisha.

na Romwald, USA, - 12.03.09 @ 12:53 | #14484


DARUBINI YANGU INANIONYESHA KUKUMBWA NA GIZA MBELENI NA HILI LITATUGUSA WOTE MIMI NA WEWE KWA KUWA INCHI YETU INAONGOZWA KWA MANENO NA SI VITENDO WANASISA WAMENASWA KWA HILI!!MGAO WA UMEME NA NJAA LAZIMA VITUKUMBE SISI HATUONI MBALI. KAMASERIKALI HAIKUWEKEZA KATIKA UMEME MUDA HUU SI WA KULUMBANA ETI TUKAE GIZA!!HAKUNA MWANASIASA ALIYE TOA UFUMBUZI MBALI NA LAWAMA WOTE TUKO NDANI YA DARAJA NA DARAJA LINAKATIKA TUSIJADILI NANI KASABABISHA TUTAFUTE NAMNA YA KUJIOKOA!!TUACHE USHABIKI WA KISWAHILI.MAONI YANGU MIMI TUVUNJE MKATABA WA VITAMBULISHO NA TUNUNUE MITAMBO MIPYA YA KUZALISHA UMEME!!WATANZANIA TUMEKALIA MANENO MANENO NA NDIO MAANA TUNACHAGUA VIONGOZI WABUVU HATUHUI KUTUMIA KURA ZETU NA HAYA NDIYO MATOKEO!!TULIDANGANYWA MVUA YA MABOMU TUKAKUBALI !!SASA TUACHE KULUMBANA NA WATALAAMU WA TANESCO WEWE NA MIMI HATUJUI CHA MSINGI NI KUWAPA TANESCO PESA AU TURUHUSU TANESCO NYINGI ZIJE KAMA MAKAMPUNI YA SIMU YALIVYOKUJA!!MWISHO TUFUTE VITAMBULISHO TUNUNUE MITAMBO KABLA YA GIZA KUINGIA!!


na CONFIDENS, TANZANIA, - 12.03.09 @ 13:01 | #14486

Sasa wewe msomi ni kweli nchi itaingia gizani lakini je hiyo mitambo itatufikisha wapi? leo hapa tunatafuta long term solution. mie naona kina mwakyembe hukuwasikiliza vizuri mzee na sioni haja ya kumtetea ZITTO HII NI SIASA TUU ,NA KUFAGILIANA NA HUYO ZITTO KACHEMKA KABISA. HATUTA WEZA ENDELEA KAMA USOMI MNAO USEMA NDIO HUU. NASIKIA SERIKALI INAPITISHA KUONGEZA WABUNGE 100 KWANINI NISIFIKIRIE KUONGEZA VITUO VYA KUZLISHA UMEME PAMOJA NA MITO MIKUBWA ILIYO TAPAKAA NCHINI ?

na NO - 12.03.09 @ 13:01 | #14487


NAONGEZEA NA HILI KUONYESHA UZAIFU WA SERIKALI NA VIONGOZI TUNAOWACHAGUA!!JAMANI KAMA MNAKUMBUKUMBU JE MNAKUMBUKA KIONGOZI MOJA WA JUU ALISEMA TANZANIA HAITAKUMBWA NA MTIKISIKO WA UCHUMI WA DUNIA??NA LEO KIONGOZI HUYO HUYO ANASEMA UCHUMI WETU UMEANZA KUYUMBA KWA SABABU YA MTIKISIKO WA UCHUMI DUNIANI!!HUU NI UDHAIFU MKUBWA SISI WATANZANIA HATUNA KUMBUKUMBU WALA UDADISI WA MAMBO TUNAKAKAA KIENYEJI NA SASA TUTAENDELEA KUVUNA MATOKEO!!AMKENI JAMANI NCHI NI YETU SI YA VIONGOZI HATA WEWE MCHANGIAJI UNANAFASI YA KUONGOZA NCHI SI WATU WALEWALE!!UKIBADILIKA WEWE NA INCHI ITABADILIKA TUMIA KURA YAKO VIZURI!!

na CONFIDENS, TANZANIA, - 12.03.09 @ 13:14 | #14488

tafadhali msijaribu kabisa kuchanganya ubama na uzembe mlionao ili kuonekana na nyie mnafikria kama obama.sidhani hata kama mlikielewa hcho alicho kiandika kwenye ktabu chake ila sema tuu kiliwagusa lakini hakina uhusiano kabisa na hii issue.

na siri - 12.03.09 @ 13:24 | #14492

Huyu anataka kuleta compromise ya ufisadi na wizihatuwezi kmuelewa haya mambo ya kilevilevi ya wasomi wetu hatuyataki yeye atulie tu tumeshakaa gizani sana kama hicho kiza cha hawa mafisadi kitafanya tufe acha tufe wapo watakaobaki.
Huu usomi wao wa kinyumenyume si ndio walipasua mtu kichwa badala ya goti na goti badala ya kichwa mnataka kitokee nini mjue kuwa wanabahatisha hawa wasomi feki wa kitanzania wanajaribu kuwaghilibu watanzania na vi-phd vyao vya kununua huko USA na kwingineko?Hawahawa ndio wlitoa ushauri wa kutoboa ile Mv Bukoba ikazama wakati uwezo wa kuivuta mpk mwaloni ulikuwepo watu zaidi ya elfu wakapotea eti wasomi!
Wamesoma nini nikuiibie halafu nikuzunguke eti nikuuzie kitu ambacho unadhani labda ni cha kwako watanzania tuamke ni wakati wetu kufikiria vizuri tusiwaache mafisadi na vihiyo wakafikiria kwa niaba yetu fikira sahihi huja kwa lugha sahihi na wakati sahihi.
Wakati wa kuila nchi hii umeisha ama zao ama zetu

na Banet., Bongo., - 12.03.09 @ 13:28 | #14493


TATIZO HILI LINAONYESHA JINSI GANI HATUJALI UCHUMI WET!!UMEME NI KITU MUHIMU SANA KATIKA MAENDELEO YETU!!SISI NI MASKINI BADALA YA KUIMARISHA MISINGI MIKUBWA YA UCHUMI KAMA UMEME ETI VITAMBULISHO VYA URAI NANI KAKUAMBIA WEWE SI MTANZANIA!!HIVI HAKUNA ORODHA MUHIMU YA VIPAUMBELE MUHIMU NA KURUKIA VITAMBULISHO??SIKATAI VITAMBULISHO ILA MUDA BADO KABISA TUWEKEZE KWENYE VITU VYA MSINGI!!NA NDIO MAANA YULE TAJIRI MKUBWA MR MO (IMF)KATUTOA NISHAI TUACHE KUOMBA OMBA KAMA HATUNA MIKONO NI AIBU KALI YA TAJIRI INAAMANISHA TUJITEGEMEE KWA RASLIMALI ZETU NA AKILI ZETU SIO AKINA DOWANS!!CONFIDENS NAKUUNGA MKONO TUACHANE NA VITAMBULISHO TUWEKEZE UMEME!!

na NYUNDO, TANZANIA, - 12.03.09 @ 13:33 | #14494

Kwa mtazamo wangu hawa watu wanaotetea unuzi wa mitambo ya Dowans hueda wameandaliwa kwanza na hao wanaomiliki mitambo hiyo ambao kwa jina rahisi tunawaita mafisadi. Kuinunua mitambo hiyo ni kukubaliana na matakwa ya Mafisadi, kwani sasa hivi hawa watu (mafisadi) wanafikiria wapi pa kuipeleka mitambo hiyo wanakosa ndiyo maana wamewatafuta akina Dr. Idrisa Rashidi, Zitto Kabwe, Dr. Lwaitama, na wengine wanaofanana nao ili wafanikishe azma yao.

Lazima wajue kwamba Tanzania ya sasa ni yatu waoweza kupambanua mabo si kama zamani tulivyokuwa tukipelekwa.

Kauli ya Dr. Rashidi si ya kiungwana (Kizalendo) anapaswa kuwajibika kwayo.Anatutisha Watanzania ili tuogope tumkubalie ili apate kamisheni yake mara mitambo hiyo itakapokuwa imenunuliwa na shirika analoliongoza.

Nashauri ununzi wa mitambo ya kuzalisha umeme inunuliwe mipya kwa kufuata utaratibu na sheria inavyosema.

Mwisho Watanzania nawomba ifike mahala tusema sasa basi kufanywa hayani na mafisadi.



na Makubi Masoga, India, - 12.03.09 @ 13:50 | #14499

NDG lwaitama (kaishaja mkazi wange) hapo umechemka, umeanza kuongelea utalaamu wa hoja nikatamani sana kuona na kutambua hoja ulizonazo kama dk.Na kama hoja za kitalaam ni kusema eti spika anaogopa endapo hii mitambo ikiuzwa basi hawa watu watatuimia hizo hela ktk uchaguzi basi mi sijaona utalaamu bali ushabiki. Kimsingi sioni sababu kumpa faida richmond fida mara mbili zaidi eti kwa kuogopa nchi itaingia kwenye giza. Eti mwakyembe na spika Sitta watakosana na rais kwa ajili ya kutokununua hii mitambo. KICHEKO.
hongera wa changiaji kwa kuliona hilo

na mwenye akili, Arusha, - 12.03.09 @ 13:54 | #14501

TCU-Nawapatia kazi nyingine,Waliopitia kozi anayofundisha Lwaitama katika pHD zao Warudi darasani upya kwa ajili ya kozi hiyo tuu!Maana walidanganywa.Dr gani asiyejua kufikiri huyu?Maslahi ya Taifa ndio,Lakini Taifa si lina sheria zake?Na waliotunga sheria hizo au wote walisoma darasa lako,maana nao wawe vimeo/vihiyo wakufikiri kama wewe.Sheria tutazivunja mpaka lini kwa maslahi ya taifa?Zitto bila shaka alikuwa mwanafunzi wako maana ni mbishi balaa.
Kukukumbusha Bw.Lwaitama usivyokuwa na akili na uwezo wa kufikiri,Mwezi wa Nne au watano Ulishiri kipindi kimoja Cha Bwana Adam Simbeye THIS WEEK IN PERSPECTIVE.Na mada ilikuwqa viongozi wa kiafrika na Mlimlenga Asilimia kubwa RAis Mugabe.Mmoja ya washiriki ukiachia kimeo wewe ni Profesa Samwli Wangwe,na Balozi(nimemsahau)ila alikuwa wa kudumu Umoja wa Mataifa.
Mjomba zile pumba zako ulizokuwa unaziongea siku ile sidhani kama Bwana Simbeye atakualika tena!Maana mimi kwa akili yangu kiasi(ila hunizidi na kila kitu)labda kwa sababu ulizaliwa zamani ukasoma bure,na uturudishie kodi zetu ***** wewe!Kazi yako kubwa siku ile ilikuwa kumpinga Profesa Wangwe,bila hata mantiki.
Sasa Zitto umemtetea tunashukuru,lakini wewe huna jipya!Nafikiri Waandishi wa Habari badilikeni,sio kila msomi ana cha kusema,Kuna watu hawajagonga vidato lakini wana mengi sana ya kutufaa.Fid Q alisema"SAMAKI ANA MENGI YA KUSEMA ILA MDOMONI ANA MAJI!"
Msomo hujui umuhimu wa sheria,Ninachoshukuru umejaribu kuwakosoa watu ambao Wamebobea kwenye Sheria SITTA,MWAKYEMBE,utashindana nao kwa hoja Kibaraka wa Mafisadi wewe!Unatuambia kwamba wanaitumikia hoja ya ufisadi waliyoiiba CHADEMA,Yaani we kweli chizi,kwani CHADEMA si ipo klwa ajili ya Watanzania!Ndio maana nasema wewe kufikiri ni sifuri!Sijui umepitisha shahada za vy****u**p na sasa ma8888****ardhi yana kumega,maana akili huwa zinaruka ati!
Sasa Mnali sijui unasubiri nini kuchapa wahadhiri feki kama hawa?Inawezekana waalimu uliowachapa walifundishwa na wakufunzi waliopitia mikononi mwa Lwaitama.Ukimtandika mtu kama huyu JK atakurudishia Taito yako upo!!!!!!!!!!

na Simba wa Yuda, Semtema-Iringa, - 12.03.09 @ 14:12 | #14503

Tanzania siasa kila kona. Mtaalamu tena profesa mzima anatuambie yaliyo kweli na bayana, tunazusha ngebe za kisiasa. Tutafakari hoja badala ya kuangalia MABIFU ya wanasiasa wa kibongo.
1 Hata kama hela zote za tanesko na hizo za vitambulisho zikichanganywa halafu tukatumia hiyo hoja ya SHERIA YA MANUNUZI (Ya kipumbavu na ya KIFISADI hakuna mfano wake duniani) ina maana umeme huo hatuupati mpaka baada ya mwaka mzima na ukichanganya na nginja za kibongo hiyo tena weka miaka 3. Na hali mbaya ya uchumi duniani wee ndio kwanza unapoteza mapato na uzalishaji kwa kukosa umeme.
2 DOWANS wako kwenye mahakama ya kimataifa. Kwa hawa wanasheria wetu tunaowajua ni wazi tutapigwa bao huko mahakama za kimataifa kama wakati ule wa IPTL. Tutaishia kulipa mabilioni ya FIDIA, halafu tena na kulazimishwa kuendelea kununua umeme huo huo.
3 Mitambo ya DOWANS imefanyiwa tathmini ilinunuliwa lini? uwezo wake wa kuzalisha ni wa kiwango gani? Kama mitambo hiyo imekidhi vigezo, na kwamba hadi kuvunjwa mikataba ilikuwa inazalisha bila matatizo ikiwa ni mwaka na nusu tu tangu ianze kazi TZ, mantiki ya wazi ni kufikiria kuendelea kuitumia. Kwa utaratibu upi, hiyo ndio hoja ya kujadiliana na si kelele za kyehu kama vyura bwawani. Watanzania yatupasa tuwe wenye kutumia vichwa vyetu kufikiri na kuweka jazba kando:
A Mitambo ikinunuliwa na tanesko kwa taratibu zao za ununuzi (sio kila mtu/kampuni inahusika na sheria ya kijinga ya manunuzi) itawapa faida? watatatua kero ya umeme? watakuwa bado na uwezo wa kutekeleza mipango ya muda mrefu kuongeza umeme hata kwa kupewa hela za vitambulisho?

B kwa tanesko kununua mitambo hii - kutakuwa kumeondoa adha ya hao DOWANS kwenda mahakani za kimataifa bado kudai? Kama ndio zogo litaishia hapo, busara iko wapi, kungoja matokeo usiyoyajua ama kuchukua hatua na kupiga ndege wawili kwa jiwe moja?

C hivi wateja wa tanesko wangapi ambao watakuwa bado na hali ya nzuri kiuchumi baada ya mwaka mzima au zaidi wa kukosa umeme? tujue kwamba ukishapiga chini kiwanda kama ALAF kwa kushindwa kukipa umeme basi ujue umetibua mambo mengi mno ambapo kwa kushindwa kuzalisha watapunguza wafanya kazi (ajira), kwa kushindwa kuzalisha kwa kiwango wataporomoka zaidi ktk hali mbaya ya uchumi wa dunia hivyo hata ukija weka hiyo mitambo yako iliyonunuliwa kwa kufuata SHERIA YA MANUNUZI hovyo mwaka mzima baadaye itaishia kung'ongwa inzi maana huyo ALAF atakuwa anatengeneza vibatali na madebe ya samli sio tena BATI za nyumba.
Sasa hawa kina ALAF wako wangapi watakaokumbwa na hii kasheshe? Zito Kabwe lina akili timamu na tafakuri yake ya masuala kama haya bila shaka imempa picha ya shimo ambalo nchi yetu inaliingia.... sasa tena kina spika SITTA wanatafakari kwa misingi ya ushindani wao na kina Lowasa tehe tehe tehe, nani atamcheka mwezie mwisho wa sakata? ACHENI UBAZAZI VIONGOZI WETU. NCHI kama US leo hii wanaweka mikakati ya BAIL-out kwa makampuni hata yaliyowaibia watu fedha - siye bado tunajichoma kisu cha mgongo kwa mambo yasiyo tija. TUTAFIKA WAPI?

na Kunga Bwera, TZ, - 12.03.09 @ 14:18 | #14505

Mimi nionavyo hakuna ambaye yuko sahihi asilimia mia moja wala amabye amekosea asilimia mia moja, ni kweli kwamba kuna wakatu hatupaswi kuangalia nani mmiliki wa kitu fulani lkn pia historia inatulazimu kufanya hivyo na zaidi tabia yetu ya Ufisadi ndio inatusukuma mara dufu kujiridhisha na umiliki maana tayari tulishauziwa mbuzi kwenye gunia, na kwa mantiki hiyo ndipo ninapouliza je hakuna mitambo mipya kabisa na kwa muda gani itapatikana? maana hilo hatujaelezwa, tokaionekane haja ya kuwa na mitambo hiyo si tungekuwa tushatoa order na ishakamilika,na viwanda vya hayo madude si kweli kuwa mpaka utoe order ndipo utengenezewe, la hasha labda kama unataka ya nyukilia kama Irani nk lkn ya kuzalishia umeme si ngumu kihivyo,je sasa what next, I think hilo ni la muhimu sasa au tumekubaliana na Dr.Idrisa kuwa asije akalaumiwa na TANESCO yake,nani sasa anapswa kutoa kauli ya KIUTEKELEZAJI,I think ni mamlaka kuu ya Nchi,-ofisi ya Rais na ifanye hivyo

na kalulu, London, - 12.03.09 @ 14:26 | #14511

Chonde chonde mimi nasisitiza KIKWETE achana na vitambulisho, nunua mitambo mipya ya umeme!! Achana na mashoga akina membe na wenzake wao shida yao ni kula pesa tu ya vitambulisho.

Naomba mtu mwenye namba ya kutumia ujumbe kwa rais kikwete anipe labda nikituma ujumbe mfupi kwa simu ataelewa, ah!

na Salome, bunda, TZ, - 12.03.09 @ 14:32 | #14514

Huyu Lwaitama akili yake haijaathirika kweli? Hivi mtu hawezi kunyang'anywa phd, Nona huyu kaithalilisha taaluma yake. Halafu katuabisha sana sisi washomire. Usimsingizie Nyerere kibiyongo alichosema yeye si hiki cha dowans, inaonyesha unasoma kitu au hukielewi au unatoa tafsiri kufuatana na matwakwa yako si ya mwandishi, hapa dr umelinganisha kifo na usingizi. Safari hii umechemsha kama alivyo chemsha huyo zitto unayejaribu kumtetea. Kuna kila dalili mmelipwa na wenye dowans.

Kwanini unataka kuturudisha kujadili suala ambalo limeshatolewa maamuzi. Mbaya zaidi maamuzi yenyewe kununua mitambo chakavu ni yakipuuzi kabisa.

Unataka kutuchanganya kuwa Sitta na Mwakyembe wamekosea na wanafanya maamusi ya kisiasa, kama hujui basi ngoja ni kuambie wao nchi hii ikiwa kiza wako salama kabisa. Watakao kiona cha moto ni dr iddrisa, ngeleja na kikwete wao kwa kushindwa kuwawajibisha.

Wanasheria wa serikali hii na tanesco sijui mnafanya nini, mimi nadhani tungetakiwa tuongelee ni kwa vipi tuna itaifisha mitambo hii ya dowans. tunasubiri nini si hawa wameitapeli serikali kupitia richmond , mbona mambo haya yako wazi kabisa.

na Longii Tigwa, Tanzania, - 12.03.09 @ 14:35 | #14517

HII NI LAIVU MUVII KUNAKITU KITATOKEA MBELENI NA HAPO TUTAJUA ZITO ANA MAANA GANI NA SITTA MWAKYEMBE ANAMAANA GANI!!MUVI IMEEANZA.....

na MTABIRI, SUMBAWANGA, - 12.03.09 @ 14:37 | #14519

tangu lini walimu wa chuo kikuu wakawa na maana. kitu gani wamesaidia taifa ili mbali ya kufuga kuku? nchi nyingi zinawatumia maprofessa kuendesha nchi ila kwetu hakuna hata mmoja. kama wangelikuwa na akili ule uwanja wa chuo usingeuzwa kufanyia maduka badala yake wangeongeza madarasa. Nyamaza endelea na kutafuta wanawake.

na jicjo, morogoro, - 12.03.09 @ 14:37 | #14520

Zitto ana akili za saisa za sasa haiwezekani maoni ya Kitaalamu yakapuuzwa kwa utashi wa kisiasa au dhana kama ni hivyo basi Wataalamu wasiwepo na Wabaki Wanasaisa peke yao.

na sudi Jamal, Ughaibinu., - 12.03.09 @ 14:43 | #14524

Mtambo usiponunuliwa kwa sababu ya WIVU, HYPOCRACY NA CHEAP POPULARITY YA KINA SITA na MWAKYEMBE ubunge wasahau...****** sana
1. wasilipwe mishahara kwakuwa hawajali biashara zetu na hasara wanajali siasa ..akili zao zina **** nafikiri

na Londa, tz, - 12.03.09 @ 14:55 | #14528

Mhhhh...!
Bado viongozi wanafikiri kuwa watanzania tuna akili sawa na za kuku....!?
Namshukuru mtoa maoni mmoja hapo juu aliye tukumbusha issue ya bwana mkubwa mmoja aliyeueleza umma wa watanzania ya kwamba nchi hii haitokubwa na mtikisiko wa kuyumba uchumi wa Dunia...leo alaa kumbe juzi/jana anawaeleza wale wale kuwa nchi itakubwa na msukosuko wa kuyumba uchumi...duh Viongozi hawa wa Tanzania!?
LEO IDIRISA ANATUTISHA ETI ITAKAPO KUWA GIZA NCHI NZIMA.....?? BINAFSI SIKUMUELEWA HATA CHEMBE. Sipati picha ya kile alichokuwa anakimaanisha, kwani nadhani anafahamu ya kuwa ni asilimia isiyo zidi kumi (10%)ya nchi hii tanzania ambayo inapata umeme wa shirika lake! Au halijui hili!?
Kwa mantiki hii nchi kuwa giza siyo habari mpya, haijawahi kuwa na mwanga/nuru ya nishati yake ***** huyo...alaaa! Hata hiyo 10% nayo haipati umeme wa uhakika, mara mgao oh matengenezo nk! Yote haya yanafanyika kuratibu ufisi wa Idi. wizi.....mtupu!
ONYO:
Kuanzia sasa wale wote wanao simamia au kufanya kazi katika ofisi zetu 'umma'wajue kuwa tunaanza kuzinduka, awe kiongozi wa siasa au wa kuajilia hanabudi kufuata maadili, kanuni na taratibu za kazi yake. Sheria, kanuni taratibu zipo japo bado zinamapungufu hivyo zirekebishwe kwa kuzingatia maslahi ya watanzania wote siyo mafisadi na zile zinazojitoshereza zifuate.
Wanasiasa fanya kazi yenu na zingatia maadili yenu na kamwe usiingilie kanuni na taratibu za kitalaam (siyo utalaam kama wa akina Lwaitama).

KIKWETE:
issue ya vitambulisho weka pembeni kwa sasa hadi uchumi wetu na wadunia utakapo imarika. Ili kukata mizizai ya fitina za Idirisa na timu yake nje ya 'TANESCO' kiasi wanacho pungukiwa kununua mitambo Mipya approx. 30~35% kimegwe kwenye bajeti iliyokuwa itumike kutengeneza Vitambulisho na kiasi kinacho baki fasta kipelekwe kwenye KILIMO mradi maalum wa UMWAGILIAJI (isiwe kilimo cha kutegemea mvua).
Rais ukitekeleza haya nina imani watanzania watakuona umejali masilahi yao, umesikiliza maoni na utakuwa umewapatia maji safi na salama kutibu kiu yao japo kwa kipindi. Rais hutakiwi kuwa kukaa kimya lolote linalo kwenda mrama wewe ndiye unayebebeshwa lawama nyingi na chache sana kwa wale walioko chini yako. Unahitaji kuwa Mipango thabiti ('Strategic plans'), utekelezaji na usimamizi mzuri ('proper implementation and supervision') na Ukaguzi endelevu wa mafanikio au la wa mipango iliyojiwekea ('continuous improvement').
Asanteni sana wadau.

na Happy, Ngara, - 12.03.09 @ 14:55 | #14529

jamani kweli unaweza kuwafundisha watu kula kwa kijiko wakti wewe mwenyewe hujui kijiko kilivyo wala kukitumia.

namheshimu sana dr. lwaitama kwani ndiye alinifundisha somo la "philosophy" pale UDSM, somo linaitwa "CRITICAL THINKING AND ARGUMENTATION-PL 101"

nikajua kuwa kwa kujenga hoja kwa maana yakufikiria na kutafakari na kutoa kauli/maamuzi ya swala unalofikiri dr lwaitama atakuwa fit kumbe bureeeeeee!!!

mitambo hatujui mmiliki wala ilitengenezwa wapi na ni nani aliyeingiza nchini tumeshtukia tu inajengwa leo tuinunu jamani we are tired with these issues tuongelee maendeleo muhimu tukanunue mitambo durable wenyewe!!

kama kuvunja sheria ya manunuzi basi tuvunje ya kutangaza tenda twende wenyewe huko marekani au sehemu nyingine inakopatikana mitambo mipya na imara kwa muda mrefu siyo hii yakununua mitambo chakavu a.k.a used.

mwisho naomba ndugu zangu tumkumbushe kikwete kuwa mkapa pamoja na ufisadi wake katuachia uwanja mzuri wa mpira hata mwakani tunategemea tuwapokee wakina ricardo kaka au thiery henry, namshauri atuachie mitambo ya kuzalisha umeme wa maji, babangu kikwetu think about ruvuma river, river rufiji and many the like in our country and lastly take back kiwira coal mining. HAPO TUTAKUKUMBUKA DAIMA!!

na komba, malawi, - 12.03.09 @ 14:57 | #14531


CHADEMA CHAMA MAKINI SANA!!KWA MTIZAMO WETU TUNAMWONA ZITO KACHEMKA ILA KAMA UNAUWEZO MKUBWA WA KUFIKIRIA HAPA HAKUNA UTAIFA BALI CHUKI NDANI YA MAKUNDI YA CCM!!HAPO ZITO KACHEZA ALICHOFANYA NI KUANGALIA HASARA KWA MAANA HATA TUKIISUSA TUTAITUMIA TUU!!HAPO HATUNA UJANJA!!PICHA ITAKUWA KAMA IFUATAVYO UMEME UTAPUNGUA NA MGAO UTAANZA VIWANDA VITAFUNGWA NA UCHUMI KUZIDI KUDIDIMIA ITAKUWA SAWA NA MGONJWA ANAYETAKA KUFA KWA KUKATAA KULA CHAKULA!!CCM NDIYO WALIYOILETA HIYO MITAMBO NA NDIO WAO WANAYOIKATAA LEO SASA KAMA NDIO WAO WALIO ILETA HIYO MITAMBO WANAMAANA GANI KUIKATAA !!

na MWONAKESHO, MPANDA, - 12.03.09 @ 15:00 | #14532

Nadhani kuna chuki ambazo hazina maslahi na taifa hili ambazo zinaendelea baina ya makundi fulani ya watu lakini lazima Watanzania waangalie kwa makini Zito siyo CCM lakini ametoa mawazo yakumpunguzia makali mwananchi hao WanaCCM nadhani wanaendeleza chuki katika makundi yao JK Stuka ikiwezekana hamia CHADEMA,chama gani hakina huruma na Wananchi zaidi ya kuweka kipaumbele ubinafsi na uroho wa madaraka.

na sudi Jamal, Ughaibuni, - 12.03.09 @ 15:06 | #14534

Magazeti msitumiwe na makundi ya watu fanyeni uchambuzi wa kweli kulisaidia taifa,kifupi Watanzania hawapati ukweli wa mambo kuhusu mambo muhimu,ebu shindanisheni hoja za hao Wabunge na wala msiangalie chuki za Waroho wa Madaraka.

na sudi Jamal, Ughaibinu., - 12.03.09 @ 15:11 | #14537

Hatutaki porojo. Tunataka tuambiwe, baada ya kuachana na Dowans jitihada gani zinaendelea kupata mitambo mipya. Haitoki mbinguni, sasa hivi tulitakiwa kuwa na quotations wakati wa mjadala huu!!

na mpingo, Bongo, - 12.03.09 @ 15:16 | #14540

Haa lwaitama unadhalilisha elimu yako na chuo kikuu cha dsm ,yaani umefikia hatua yakutetea mafisadi

na sultan juma, tznia, - 12.03.09 @ 15:24 | #14542

Kama usomi na Uhadhiri ndo huu, Mie ninachoka kabisa.Huyu msomi anataka tuamini kwamba,njia pekee ya kutatua matatizo ya umeme NA amabayo inamsilahi kwa nchi ni kununua mitambo ya Down!.Huyu naye ni walewale tu.

na wapotipoti, kigoma, - 12.03.09 @ 15:34 | #14543

HAPA HAKUNA CHA UTASHI WA KISIASA WALA HAKUNA CHA UTAALAMU WALA KITU GANI.SHERIA ZA BUNGE ZINASEMA KUWA MTAMBO WOWOTE ULIOTUMIKA USINUNULIWE NA SEREKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.HUU MJADALA UFUNGWE MARA MOJA KAMA WAZIRI WA NISHATI HAJUI MAHALI MITAMBO HII INANUNULIWA ATOE TENDA ZA KULETA MITAMBO HII KWA MAKAMPUNI YA NJE TULETEWE MITAMBO MIPYA.MITAMBO CHAKAVU NO WAY.LOWASA APELEKEE WATU WA JIMBO LAKE KULE MONDULI AWAZAWADIE KWA KUMPIGIA KURA ZA NDIO TOKA ENZI YA UJANA WAKE.HAPANA AMPATIE ROSTAMU AZIZ AKAFUNGE KWAKE.

na OLE LETIPIPI, TANZANIA, - 12.03.09 @ 15:57 | #14549

KWA ZITO KABWE

KWANZA NAOMBA UNISAMEHE ILA NILIKUTAADHARISHA KUUNGA UNUNUZI WA MITAMBO YA DOWANS NILIJUA WATU WATAKUPINGA KABISA NA KUKUONA SEHEMU YA MAFISADI NA KWELI IKAWA HIVYO.NIMEGUNDUA MITAMBO ILILETWA NA CCM WENYEWE LEO WANAIKATAA WAO WENYEWE WANATAKA TUNUNUE MIPYA KWA MAANA WANATUTIA HASARA MARA MBILI WAKUBWA WA TAIFA WAMEONA NI HASARA KUNUNUA MIPYA WATAHUKUMIWA MARA MBILI!!INCHI YETU NI MASKINI NI BORA TUIKARABATI HIYO CHAKAVU TULIYOIVUNA KWA KURA ZETU!!KWA UJUMLA VIONGOZI WA KITAIFA WAMEJITOA KUNUNUA MITAMBO MIPYA WASIJE WAKAHUKUMIWA MBELE YA SAFARI NA NDIO MAANA WAKO UPANDE WA KABWE(CHADEMA) SITTA NA MWAKYEMBE WAMESHIKA KULIKO OZA CHADEMA NI MAKINI SANA WANAONA MBALI SANA!!!

na MTABIRI, SUMBAWANGA, - 12.03.09 @ 16:13 | #14553

Who is Lwaitama? Wewe nani kakutuma? Na sioni utaalamu kwenye unayoongea.Tatizo si makampuni bali uchakavu na bei za mitambo husika. Zitto aliingizwa mjini. Ukweli huu tuukubali hata kama tunampenda.

na Gamba Byona - 12.03.09 @ 16:37 | #14560

NINA WASIWASI SANA NA MSIMAMO NA MAWAZO YA DR AZAVELI LWAITAMA,NI MSOMI NILIYEKUWA NA MUAMINI NA KUMSIKILIZA SANA LAKINI SUALA HILI LA DOWANS LINAMUINGIZA KATIKA KUNDI LA AKINA ZITTO NA WENGINE WALIOKO KATIKA PAY LIST YA MAFISADI!.
DR.LWAITAMA ANAFIKIRI NI YEYE TU NDIYE ANAYECHAMBUA KWA UNDANI MASUALA YA KIJAMII HAPA NCHINI,NA NDIYE MWENYE UCHUNGU WA DHATI NA NCHI HII.
KAMA KWELI AMETOA MAKALA HII KWA NIA NJEMA BASI KABLA YAKUITOA ANGEJARIBU KUPATA MAONI YA WALIO NDANI YA SAKATA HILI KUJUA KWA KINA MCHEZO MCHAFU ANAOJIINGIZA KUUTETEA,KWA KUWA NINAMHESHIMU DR LWAITAMA JAPOKUWA MAONI YAKE KWA SIKU ZA KARIBUNI YANAELEKEA KUNUNULIWA NA MAFISADI NA KUTAFUTA POPULARITY KWA KULAANI MAMBO YANAYOFANYIKA NCHINI CHINI YA UTAWALA ULIOPO BILA KUTOA SULUHISHO-KUMBUKA KULAUMU NI RAHISI KULIKO KUTENDA!.
NAKUSHAURI DR AZAVELI PUNGUZA MUKARI NA MWENDOKASI WA LAWAMA NA KUFANYA FAIR ANALYSIS KWA FAIDA YA NCHI YAKO NINAYOAMINI UNAIPENDA KWA DHATI.

na Maskini Mzoefu, Dar, - 12.03.09 @ 16:53 | #14562

Zitto kachemka, Lwaitama naye kumbe ni buree, watu wanataka kujisafisha na kuendeleza deal za Richmond, halafu sisi tuwasafishe kwa kununua mitambo ya Dowans!

Kama nchi kuingia gizani na iingie, ina maana giza suluhisho lake ni mitambo ya Dowans na si mitambo mipya!
UFISADI MTUPU.

na Geoman, Dar, TZ, - 12.03.09 @ 17:00 | #14565

Kwanza nadhani ni vyema nikaonyesha msimamo wangu mapema,naunga mkono hoja ya zitto na hoja ya dr,rashi na Lwaitama.pamoja na kwanza mheshimiwa sitta na mwakyembe,Tundu na Mkinga ni wanasheria wanachonishangaza ni kwa nini hawaelewi suala la richond lililisha baada ya kampuni kununliwa na mtu mwangine na kuendelea kuzungumzia matatizo ya richmond huu ukihusisha na dowans ni kuonesha kuwa hauelewi kabisa sheria za makampuni.pia lazima ujue mgogolo haukuwa mitambo ni njia za kutoa kazi kwa richimond,
naunga mkono hoja ya zitto na serikali kwa sababu nne
1.kesi iliyopo kwenye mahakama ya usuluhishi ya kibiashara hatma yake ni mmoja kumlipa mwenziye kama pande mbili hizi zinaona kwa kila namna kila upande una haki zake njia pekee hata ukiichelewesha ni kulipanana
2.mitambo hii ipo tayali tanesco na tayali mafundi wetu wanaijua,tayali tumeona uwezo wake,a tunajua fika mitambo iliyotumika miaka miwili haiwezi kuwa ime depreciate hata kwa 10%.
3.mahitaji ya umeme yamesababisha nchi hii kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwenye makampuni ya umeme,hata ukifanya hesabu ya darasa la kwanza,mfano iwapo leo utaingiza megawati 100 kwenye grid ya taifa na ukaondoa misamaha ya kodi amabayo itasababisha wawekezaji waanze kulipa immediately, na kwa muda wa kuanza kuagiza mpaka kununua thamani ya msamaha itakuwa juu ya kununua ni vyema tukamaliza tatizo hili leo na tuzibe misamaha yote.
4.lazima watanzania wajue hali ya nchi hii siyo marrekani,kama kila mtambo uliyoko tanzania tunaagiza nje ni vyema ukajua kuwa dhalula itaendelea kuwepo,tunajenga kwa mkopo kila kitu, umeme tunaotaka kutumia makaa ya mawe nao pia unahitaji mitambo ambayo pia ni kwa mkopo tu,inamaana hamjui kuwadunia nzima kuna mgogolo wa fedha?

na kanyasu costa, mwanza, - 12.03.09 @ 17:02 | #14566

Lwaitama is learned but not knowledgable. We will respect one for ones commonsense and not doctorate. Try to listen to his contributions in workshops, perspective-tbc ****** mtupu. Has nothing to over.Talk talk no context no contents. Another educated fool roving around on grounds of a lecturer and Dr upuuzi mtupu. Please keep your frustations away from confusing public.

na lwakatare, tz, - 12.03.09 @ 17:21 | #14568

NANUKUU “Ninachoamini kama unajua huyu ni shetani lakini ana kitu muhimu, ni bora kuangalia kile kitu muhimu kuliko kuangalia ushetani wake,” Siamini kama huyu Lweitama anaelewa kitu anachonukuu kina madhara gani. Shetani akikuambia kakate mkono wa albino utapata fedha, basi yeye atafanya hata kama ni kinyume cha sheria, ni kauli ya mtu asiyechambua mambo kwa kiina. Anapozungumzia utaalamu ana maana gani? utaalamu wa mitambo tu? je utaalamu wa kisheria vipi (sheria ya manunuzi)? kiuchumi ni vipi? Huyo DR amenichosha kabisa. Na uelewa wake ni mdogo anaonekana ni mtu mbishi tu. Poleni wanafunzi wake ikiwa ni pamoja na Zito. Tangulini mtu wa falsafa ukaanza kuungea mambo ya kisheria na uchumi.



na Mshauri, USA, - 12.03.09 @ 17:50 | #14577

jamani hoja za huyo lwaitama ni ishara tosha kwamba tusiumize vichwa vyetu kuhusu yeye!! angalau ametuonyesha kuwa yeye ni msomi wa namna gani. ukiendelea kubishana na mjinga halafu mtu akaja akakukuta unabishana na mjinga, kamwe hataweza kujua ni nani mjinga kati yako wewe na huyo mjinga!! manake sasa atakuona nawewe pia mjinga kwa kupoteza muda wako kuhangaishana na mjinga!! hakika lwaitama kwa hilo ametuonyesha ujinga wake na kwa namna gani hafai tena kufuatwa na waandishi ili kutoa maoni kwa issues zihusuzo maslahi ya taifa.
Mimi jamani nalia na issue ya vitambulisho!! HIVI JAMANI HUYU RAISI WETU AMESOMA KWELI?? HAO WASHAURI WAKE WA MAMBO YA KIUCHUMI WAMESOMA KWELI?? hata kama wangekuwa hawajasoma(kama inavyoashiria), but do we need to be professors to even realize these small things?? sidhani, nadhani hata common sense tu inatosha kufanya maamuzi makubwa. Ni ajabu kuona kuwa rais wetu ambaye anajiita mchumi na washauri wake wanashindwa kujua na ku-practice kitu kinachoitwa 'prioritization' katika kuamua ni kipi kifanyike kwa maendeleo ya taifa na kwa wakati upi. hivi tukianza ku-rank mahitaji ya kiuchumi,kijamii, na hata kiusalama ya nchi maskini kama tanzania halafu tukafanya prioritization kweli ni sahihi kulipa suala la vitambulisho vya taifa first priority kweli??!!!..kwa hakika ni 'personal interests' TU zinazoweza kumotivate kipaumbele kwa vitambulisho vya taifa na kuyasahau matatizo mengine yahitajiyo hatua za haraka. ukiangalia hela zilizotengwa kwa ajili ya zoezi hilo halafu ukamwambia mtu tanzania ni nchi maskini yenye matatizo mengi hatakuelewa!! kuna nchi nyingi sana tajiri na ambazo wananchi wake wanaishi bora lakini hazina vitambulisho vya taifa. kwa raisi wetu kulipa kipaumbele suala la vitambulisho ni dhahiri kwamba matatizo ya kiuchumi katika nchi yake sio kwmba hayatambui, bali hayajui. watu wako hawana maji, hawana umeme, miundombinu mibovu, tatizo la usafiri hapo dar namaanisha msongamano wa magari sasa liko ktk hatua isiyovumilika, ujambazi hausemekani, sekta ya afya shida, nk wewe unakimbilia kuwapa wananchi hao wanaoteseka vitambulisho!! watu wale hivyo vitambulisho? budget yetu iko externally funded kwa over 40 percent! misaada hiyo tungeitumia kutatuta matatizo muhimu ya kiuchumi, sababu tangu uhuru tumeweza kuishi bila hivyo vitambulisho! inashangaza kuona mabilioni yanapelekwa kwenye zoezi la vitambulisho halafu tunawageukia wajapani tunawaomba watujengee fly-overs kutatua tatizo la usafiri dar, rais anayetumia kila awezalo kuifanya nchi kuwa ombaomba. instead of making the country a self sustaining country developmentwise the kikwete is spending sleepless nights to seeing that his country is becoming a sustainable begger! manake unaomba unapewa unaziharibu unarudi unaomba tena unaziharibu unarudi unaomba tena na kwa mana hiyo unakuwa ombaomba wa kudumu usiyebebeka!!
watanzania tunatakiwa kujua kwamba zoezi la vitambulisho ni la kifisadi lililojaa rushwa tuungane tulipinge kwa nguvu zote kabla halijatekelezwa. na ni vyombo vya habari tu vinavyoweza kufanikisha hili. ni vizuri kuziba ufa kuliko kuja kujenga ukuta. hawa mafisadi tusiwasubiri waibe kwanza wajenge majumba yasiyosemekana ndo tuanze kuwafuatilia inakuwa too late.
kuna bwana mmoja ameshauri zoezi la vitambulisho lisimamishwe na hela ziongezwe kwenye kutatua tatizo la umeme mimi binafsi naunga mkono hoja hiyo ya kizalendo iliyojaa fikra haswa. lakini pia rais anatakiwa kuwatimua kazi washauri wake wa kiuchumi hawana wanalolifanya zaidi ya kumpotosha. hawana sifa za kuwa washauri wa kiuchumi kwa mambo yahusuyo maendeleo ya nchi.

na Elvis, US, - 12.03.09 @ 18:32 | #14589

sioni haja ya kumtetea zito kwani yeye kama msomi agejuwa kama unapotaka kununuwa kitu chochote kikubwa kama gari au machine lazima kwaza ujuwe title au deeds ina jina la nani. hivyo unapo sema kuwa mmiliki sio mhimu sijui unatumia sheria gani. ukikutani na mtualiye toka kupola gari halafu akwambia ukuzie hilo gari la uporaji bila kujuwa kama gari lake au laa basi wewe uliye nunuwa gari hilo ndiye utakaye kuwa mporaji. kwa hoja hiyo tanzania egelisi madeni yote ya richmong na dawns ingekuwa ndiye ***** aliye kamtwa na mali. hivyo huyo mtaalamu philosophy naona ununuzi sio ujuzi wake.

na emanu bita, tanzania, - 12.03.09 @ 19:44 | #14604

Kumbe na Kanyasu Costa ni FISADI!,Watanzania tumeshaibiwa saaaanaa!,kudhalilishwa sanaa,kunyanyaswa saanaa na MAFISADI!.SASA TUMESEMA BASI,CHOCHOTE TUNACHOKIHISI SI CHEMA KWETU HATUKITAKI NA KAMA GIZA NI LIWE GIZA!.Sie hatubabaiki na HIYO TISHA TOTO YA DR RASHID NA MAFISADI WENZAKE!.
Ikiwa suala la kuagiza mitambo mipya inawekwa mizengwe lakini ukiwapa MAFISADI TENDA ZAO FEKI mitambo inashushwa kwa ndege ya kukodi!!,kwani wanajua wameshatuibia !.
NADHANI UMEKARIBIA WAKATI WALALA HOI WATAANZA KUHUJUMU MALI ZOTE ZA MAFISADI NA HATIMAYE ROHO ZAO!,WAMEZIDI KUTUFANYA WAJINGA!.

na Maskini Mzoefu, dar, - 12.03.09 @ 21:05 | #14614

Kwani Kikwete na wenzake wapo hapo kwa maslahi ya Wananchi au Walanchi? mbona hawakati mzizi wa fitna? mpaka sote tuwe akina "Ma-ibrahimu" eeh!!! aaah jamani wote sisi wakubwa tusitishiwe nyau - Chonde. Na huyo Prof. wa choo ni "***vi" tu, au katokea Mzumbe nini?

na NYAU - 12.03.09 @ 21:30 | #14616

Nakuunga mkono maskini mzoefu kama watu wakianza kuhujumu mali za mafisadi na mafisadi inaweza ikatusaidia. Kwani wataona hakuna umuhimu wa kutuibia. Mkimjua fisadi anapita njiani vunja gari lake hata kioo tu. Chomeni nyumba zao n.k. Ili wajue kuwa kutajirika kwa kutuibia sio dili tuwaandame mpaka waikimbie tanzania.

na Longii Tigwa, Tanzania, - 12.03.09 @ 21:31 | #14617

tatizo letu sisi watanzania ni kufuata mkumbo bila kufanya japo utafiti wa kimazingira. Hoja za huyu mhadhiri sio kumsafisha Zitto bali ni kuifumbua jamii macho ili wajue ni viongozi wa aina gani tulio nao. Ukweli ni kwamba ktk mazingira yanayogubika Dowans[Richimond] sio kwamba serikali haiwajui wamiliki wake bali ni kwa kutambua kuwa wamiliki wa Dowans ni baadhi ya viongozi ambao jamii imewaamini bila kuwajua hivyo kuwaweka hadharani ni kuisambaratishe serikali ya CCM jambo litakaloweza kuiondoa ccm ktk ulimwengu wa siasa.Kwa bahati mbaya hawa wanaosema mitambo isinunuliwe kwa madai ya kutaka kujua wamiliki wake ni wanafiki maana wako ktk NEC ya CCM na wanapoibua hoja za kuwajadili wanaotuhumiwa wao hukaa kimya kwa kuogopa kujiweka ktk wakati mgumu kiuchaguzi hivyo wanabaki kulalama tu mitaani.Wao walitoa maazimio kupitia kamati ya Mwakyembe ili kuwabana wahusika na sio mitambo maana wanawajua cha msingi ni wao kutokubali kupitisha bajeti ya serikali hadi hapo serikali itakapo tekeleza maazimio yao ikiwa ni pamoja na kutaifisha mitambo hiyo kama wamiliki wake watashindwa kujitokeza au kuipeleka Dowans mahakamani ili iwalete waliouza mitambo hiyo. Wakifanya hivyo sio tu kwamba wataeleweka bali tutajua wana nia na maslahi ya taifa tofauti na sasa ilivyo ambapo wanakomoana tu bila kujali wanaoathirika ni wananchi walipa kodi huku wao wakigawana posho na mafao mazuri bunge linapo malizika.

na ben, tz, - 12.03.09 @ 22:05 | #14621

Hii ni issue ya kusikitisha sana. Ndiyo tunashida na umeme, hivyo la kufanya ni kutafuta jawabu nini kifanyike kihalali na kwa kuzingatia hali yetu ya uchumi na matumizi yetu ya umeme hapo baadaye.

Katika sheria za manunuzi ni muhimu kumjua muuzaji kiundani na hasa katika ununuzi wa mitambo. Mitambo kama hiyo itatakiwa kufanyiwa maintanence za mara kwa mara na pengine hata spear parts mpya pale inapoharibika.
Sasa kama muuzaji mpaka leo hajulikani kwanini nchi ijiingize katika biashara za kitapeli kama hizi?. Nchi inashindwa nini kutumia balozi zake zilizopo nje ya nchi ili kutafuta mitambo mingine?. Mitambo ya Dowans kuwa ndani ya nchi si kigezo cha kutufanya tununue mitambo hiyo, ni lazima tuangalie vigezo husika katika ununuzi wa mitambo kama hii. Hatununui shati wala pipi ambazo hazitakiwi kuwa na guarantee ama service after sale.

Watanzania tumechoka kuchezewa na watu wachache ama mafisadi. Mitambo hiyo ya Dowans ililetwa na mafisadi na wametuumiza sana kwa kutumia mitambo hiyo. Pesa zetu wamechukua na wameshindwa kutupatia umeme. Ni bora na hekima kuwaachia mitambo yao ambayo ime-prove failure waangaike nayo. Tutafute mitambo mingine taaratibu kwa kuzingatia hali halisi tuliyonayo katika Tanzania bila kusahau kwamba watumiaji wa umeme wataongezeka kadri siku zinavyokwenda.

na Kidatu, Tanzania, - 12.03.09 @ 23:04 | #14628

LWAITAMA UMEPOTOKA,NA NIMEKUONDOA KABISA KWENYE ORODHA YA WATU MAKINI. I THINK YOU ARE A FOOL DR. HUJUI UNACHOSEMA WALA HUJUI HOJA ULIYOTETEA BALI ULICHOTETEA NI JINA LA ZITTO KABWE ALIYEKUWA ANAPINGANA NA HOJA ZA MWAKYEMBE NA SITTA,BILA KUJALI MASLAHI YA TAIFA NA BILA KUJALI SHERIA. MSIJIFANYE SPOKESMAN WA HILI TAIFA NYINYI NI VILAZA TUUU.

na DENTI MAKINI, UDSM, - 12.03.09 @ 23:56 | #14637

Kwa kweli Dr Lwaitama laiti ungekuwa kiongozi wa nchi, tungekuundia tume kwamba tuna mashaka na wewe.Na hata Phd ungepokonywa.Naomba ujue kwamba kuwa CRITICAL sio lazima upingane na serikali, unaweza ukaungana hata kwa hoja makini kama ya akina Mwakyembe. Mimi ni mwanafunzi wako hapa chuoni lakini nashangaa sana kusikia ukiunga mkono hoja mgando kama ya kaka yangu Zitto. Kweli wewe ndiye umetoka chama kimoja kwenda kwenye chama kimoja kimoja!nakumbuka hii kauli uliitoa pale DDC survey kwenye mkutano wa Chadema, kumbe wewe ndiye! hata Chadema hawawezi kukuchukua kwa kauli kama hizo utawaalibia chama, au umetumwa na CCM uchafue upinzani. INAWEZAKANA MZEE WETU UMECHOKA KUFANYA ANALYSIS, PUMZIKA KIDAGO MZEE, HATA MWA MMOJA ILI UNOE KIPARA VIZURI.

na LAWRENCE LUVANDA, Dar/Tanzania, - 13.03.09 @ 01:25 | #14641

ah! nchi yetu jamani ukiifikiria sana yani unaweza kuwa chizi. kila ajaye ana kasoro zake!! yule wa awamu ya tatu alikuwa na yake huyu tuliye nae nae amekuwa so cheap kiasi kwamba wa chini yake wanamgeuza watakavyo. sasa ishu kama hizi yeye yuko kimya tu kana kwamba haoni. wenzake wanataka kutoana macho kule dodoma yeye aaah bado yupoyupo kwanza!!! sasa watanzania na umaskini wetu mtu anaibuka tu from nowhere anatuongezea machungu kwa kututisha kuwa tutakaa gizani na tusiilaumu tanesco!!..hata nchi iwe na giza kiasi gani ikulu kamwe haiwezi kukumbwa na giza hilo sasa sijui hiyo ndo sababu ya ukimya huo!!
kwa hali ya ufisadi ilipofikia nchini kwetu usishangae hata iyo bei ya hiyo mitambo ya dowans inayotajwa isiwe halisi. na kwa nini basi tununue mitumba sisi kama nchi?? inawezekana zitto alipendekeza inunuliwe mitambo lakini hakupendekeza kwamba lazima tununue hiyo ya dowans na kama alipendekeza tununue hiyo ya dowans basi nae sasa amechoka au kaingia kwenye ufisadi!!
lwaitama si wa kumtetea kwani ameonyesha udhaifu mkubwa katika kuanalyse hii isssue. ameangalia utaalamu katika masuala machache sana!! hapa kuna utaalamu wa kisheria, kuna utaalamu unaoweza kufanywa na wataalamu wa pricing/valuing kuona kama bei inayokuwa stated ni imekuwa over au under-stated in which case the former is our interest, kuna utaalamu wa kuangalia ubora na uwezo wa mitambo kufanya kazi kwa muda mrefu ili tusije inunua leo kesho tunaita wataalamu wa kuirekebisha, nk sasa huyu MR. lwaitama sijui haoni kama anafanya shallow analysis!!!!


na elvis, USA, - 13.03.09 @ 02:41 | #14655

New revelation: Dowans in huge debt

-Controversial turbines named as collateral for massive loans from Barclays, Stanbic banks

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE controversial Dowans Tanzania Limited company is carrying a massive debt resulting from loans received from various commercial banks to the total amount of $75m (over 100bn/-), THISDAY can reveal today.

Our investigations have established that the loans were secured by registered company assets including the 100-megawatt power generation turbines that the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) has been trying to purchase through its parent government ministry.

Documents seen by THISDAY show that during 2007, Dowans was awarded several loans worth a total of $55m from Barclays Bank alone, and another $20m from Stanbic Bank.

In May 2007, a debenture in favour of Stanbic Bank Tanzania Limited was taken out, under which all present and future assets of Dowans Tanzania Ltd - both movable and immovable were placed under mortgage for the loan.

A month later (June 2007), Dowans initially secured a loan of $20m from Barclays Bank’s Mauritius branch, and five months later, landed another credit line of $5m - this time from Barclays Bank Tanzania Limited.

Again, the company put up its registered assets as collateral.

Yet another certificate of indebtedness shows that Dowans secured another loan of $30m from Barclays Bank in November 2007.

It could not be immediately established if either the TANESCO Managing Director Dr Idris Rashidi or the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, were aware of these debts when vigorously pursuing their bid to pave the way for a government purchase of the company’s used turbines at an astronomical price of $60m (approx. 90bn/-).

However, the fact that Dowans still has such debentures in place with a number of banks could have further complicated any deal for the purchase of the turbines presently sitting idle in Ubungo, Dar es Salaam.

According to the certificates of indebtedness signed by Dowans, the company acknowledges its debts with each of the banks for specified sums of money, on all of which interest is due until the principal amounts are paid back.

Going by these latest findings, it is clear that if the dubious plan to buy the Dowans power turbines had succeeded, someone 'either TANESCO or the government' would have ended up inheriting these colossal debts.

Although Rashidi announced last week that the public power utility had abandoned the controversial plan to buy the Dowans machinery, the whole issue appears to have ignited a heated public debate that shows few signs of cooling down any time soon.

Somewhere at the centre of the debate is the Kigoma North Member of Parliament Zitto Kabwe (CHADEMA), who has raised many an eyebrow in publicly backing the Dowans turbines purchase proposal in his capacity as chairman of the parliamentary public corporation accounts committee.

The opposition legislator, who has steadily built up a reputation as a refreshingly maverick and strong-minded politician, has even found himself at direct loggerheads with fellow MPs, notably members of the parliamentary energy and minerals committee which had already vetoed the proposal.

The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, has also made his position clear as strongly opposed to the proposed Dowans deal, pointing out that it would effectively revive the nationally-embarrassing Richmond scandal saga of last year.

The Speaker minced no words in cautioning the government against getting itself involved in such a deal.


na Sikonge, Tanzania, - 13.03.09 @ 02:50 | #14659

Lwaitama naona sasa uendelee kukariri darasani,Obama unayemsema ajavunja sheria bali ameziheshimu,Profesa mzima umepoteza muda wako mwingi kwenye vyombo vya habari kuetetea uvunjaji wa sheria ya manunuzi,kwa mwendo huo hautaweza kuisaidia taifa hata kidogo zaidi kafuge kuku kama ilivyokawaida kwa Maprofesa wengi wa UDSM

na kurenga, Tanzania, - 13.03.09 @ 05:36 | #14671

Huyu Prof/Dr. Ni kati ya watu waliotumia 1/2 ya maisha yao kukalii nadhalia za watu wengine kama zilivyo bila kuongeza za kwao, akijaribu kuongeza tu unaotoka ni upupu kama huu. Huyu Prof. kama angefanya research kidogo tu ya dakika 10 kwenye Internet na kujua gharama za hizo mitambo asingesema haya **** tena mbele ya Watanzania. Au ni frasturation ya maisha amepoteza muda mwingi shule lakini return yake ni zero.

na kimbisa, tanzania, - 13.03.09 @ 06:35 | #14672

Prof. njaa huyu.
Kabla hata ya kununua, kwanza lazima kufikiria uhalali kisheria wa kununua hizo mashine kabla hata ya kufikiria kama zinafaa au hazifai. Kufikira Owner inafuatia, na kwa hizi za Dowans, kwa kua ziko owned kitapeli si halali kuhalalishwa na serikali kwa kuzinunua. Ni njia moja tu ya kuzihalalisha, nayo ni kuzitaifisha.

na Kib, DSM, - 13.03.09 @ 08:10 | #14681

HUYU MSOMI WA CHUO KIKUUU HANA JIPYA,AMESAHAU KUANGALIA SHERIA YA MANUNUZI INASEMAJE,KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VILIVYOTUMIKA?.IWEJE LEO MSOMI NAYE ANATETEA UFISADI AKUMBUKE KWAMBA DOWANS NA RICHMOND NI MTU NA MJOMBA WAKE,MSIMAMO WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI YABAKI PALE PLE.

na S.S SHADRACK, MASASI, - 13.03.09 @ 09:06 | #14683

Mitambo ya Dowans:
*Issue hapa nikwamba imekuwaje swala la umeme na dowana linatumika kuwateka mateka watanzania(blackmail)?
na siyo Mhadhiri amtetea Zitto au Idirisa.
*Namuunga mkono Mh. Mashilingi ya kwamba Umeme ni issue ya usalama wa Taifa na
*Dr Idrrisa ametumia kwa matamshi yamezidi madaraka na amama taifa tiliyo mkabithi.Ni kiongozi hatari na anapashwa kuwajibishwa
*Namuunga mkono Mh. Spika -Kununua mitamabo ni kuvunja sheria labda ibadilishwe maana nchi inaongozwa kikatiba.
*Je Kamati ya mipangao ya Wizara husika ilikuwa wapi mapaka tumefikia hapa? hapa uwongozi wa wahusika uwajibishwe maama huu ni Uzembe(incompetence)
*Na kama ukilipa swala hili sura ya KITAIFA hii ni HUJUMA(sabotage)
*Na ukilipa sura ya USALAMA basi ni UHAINI(treason)
KUNA MTU AU CHOMBO KINAPASHWA KUWAJIBISHWA HAPA!!!!!!


na kazikazi, tz, - 13.03.09 @ 09:44 | #14685

UMEME NA VITAMBULISHO KIPI BORA, KWENU WANA INZI WA INZI HII.......

CHA MUHIMU NI SERIKALI KUCHUKUA HIYO HELA YA VITAMBULISHOA NA KUNUNUA MITAMBO MIPYAAAAAA. KUNA USALAMA GANI KATIKA GIZA???

JARIBU KUJIULIZA HATA WEWE MWANA INZI!!!!!!

na Mcha Mungu , Mwanza, - 13.03.09 @ 09:59 | #14686

kwa mtazamo wangu huyu msomi kasema kweli, lakini kwa kuwa tulio wengi tunaliangalia suala hili kisiasa na chuki basi na tungoje tuone ukweli utajitokeza uko mbele.
kama ni kukaa giza na kufa njaa hili ni suala la walala hoi. hakuna hata mbunge atakayeguswa na vitu hivi. kila mmoja ana jenereta nyumbani kwake na chakula cha kutosha
Vumbi litarudi kwetu tu na hapo ndipo tutakapoanza kurukana.

na kabwe makanika, Daresalam, - 13.03.09 @ 10:46 | #14688

New revelation: Dowans in huge debt

-Controversial turbines named as collateral for massive loans from Barclays, Stanbic banks

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE controversial Dowans Tanzania Limited company is carrying a massive debt resulting from loans received from various commercial banks to the total amount of $75m (over 100bn/-), THISDAY can reveal today.

Our investigations have established that the loans were secured by registered company assets including the 100-megawatt power generation turbines that the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) has been trying to purchase through its parent government ministry.

Documents seen by THISDAY show that during 2007, Dowans was awarded several loans worth a total of $55m from Barclays Bank alone, and another $20m from Stanbic Bank.

In May 2007, a debenture in favour of Stanbic Bank Tanzania Limited was taken out, under which all present and future assets of Dowans Tanzania Ltd - both movable and immovable were placed under mortgage for the loan.

A month later (June 2007), Dowans initially secured a loan of $20m from Barclays Bank’s Mauritius branch, and five months later, landed another credit line of $5m - this time from Barclays Bank Tanzania Limited.

Again, the company put up its registered assets as collateral.

Yet another certificate of indebtedness shows that Dowans secured another loan of $30m from Barclays Bank in November 2007.

It could not be immediately established if either the TANESCO Managing Director Dr Idris Rashidi or the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, were aware of these debts when vigorously pursuing their bid to pave the way for a government purchase of the company’s used turbines at an astronomical price of $60m (approx. 90bn/-).

However, the fact that Dowans still has such debentures in place with a number of banks could have further complicated any deal for the purchase of the turbines presently sitting idle in Ubungo, Dar es Salaam.

According to the certificates of indebtedness signed by Dowans, the company acknowledges its debts with each of the banks for specified sums of money, on all of which interest is due until the principal amounts are paid back.

Going by these latest findings, it is clear that if the dubious plan to buy the Dowans power turbines had succeeded, someone 'either TANESCO or the government' would have ended up inheriting these colossal debts.

Although Rashidi announced last week that the public power utility had abandoned the controversial plan to buy the Dowans machinery, the whole issue appears to have ignited a heated public debate that shows few signs of cooling down any time soon.

Somewhere at the centre of the debate is the Kigoma North Member of Parliament Zitto Kabwe (CHADEMA), who has raised many an eyebrow in publicly backing the Dowans turbines purchase proposal in his capacity as chairman of the parliamentary public corporation accounts committee.

The opposition legislator, who has steadily built up a reputation as a refreshingly maverick and strong-minded politician, has even found himself at direct loggerheads with fellow MPs, notably members of the parliamentary energy and minerals committee which had already vetoed the proposal.

The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, has also made his position clear as strongly opposed to the proposed Dowans deal, pointing out that it would effectively revive the nationally-embarrassing Richmond scandal saga of last year.

The Speaker minced no words in cautioning the government against getting itself involved in such a deal.


na Salome, bunda, TZ, - 13.03.09 @ 10:55 | #14700

Kumbe hata huyu msomi naye fisadi tu! sio ajabu hata Zitto mwenyewe alimtaja katika barua yake kwa watanzania. hapa hakuna hoja ya utaalamu wala siasa bali uhusiano wa kifisadi wa mitambo hiyo na Richmond na dowans kwa upande mmoja, mitambo ni mitumba na sheria ya manunuzi, lwaitama "no research no right to speak" soma barua ya Zito kwa serikali mbona huko hataji umuhimu wa kununua mitambo ya Dowans? sikiliza hoja za wajumbe wengine wa kamati ya hesabu, hoja hiyo waliikataa! Kamati ya Zito ni ya hesabu sio nishati kiherehere chake cha nini? Acha kuganga njaa nenda kwa Rostam akukatie, mtaalamu feki, Zitto kaukoroga mwache aunywe!

na Muganyizi Kashasha T, Arusha, - 13.03.09 @ 11:01 | #14701

Wasomi wa Tanzania bwana we acha tu,
Msomi ambae unafundisha watu chuoni unatetea sera za ufisadi au na wewe fisadi angalia sana,Ukweli unabaki pale pale hakuna kununua mitambo chakavu.Au na huyu msomi kapewa chochote na mafisadi angalia unasomesha wanafundi usiwapotoshe darasan.Usomi wako bado nenda kasome ufikie uprofesa ndio utatoa ujinga bado ujinga unao.Au na wewe kama Zitto.
Watanzania wenzangu tuangalie sana wasomi hawa wanapotosha jamii hawafai katika jamii tuwe makini sana.


na Juma Ally, Mwanza , - 13.03.09 @ 11:18 | #14704

You fools stop calling dam MSOMI...huyu ni cramer...ame invent kitu gani kilichomnufaisha mtanzania jamani?...nashanga vigazeti na viredio ikitokea ishu..utasikia eti hebu tumsikia mtaalamu na mchambuzi wa mwaswala ya kisiasa...loh!...over my dead body huyu mnywa gongo was mlimani siwezi hata kupoteza muda nae...LWAITAMA nakufahamu huna tofauti na shyroae bhanji...unaspenda sana press...

na kaji kaji, DSM TZ, - 13.03.09 @ 11:49 | #14711

ili ni suala la kitaifa hivyo basi maamuz yote yalenge kumnufaisha mtz

na blaise,V.M, tanzania, - 13.03.09 @ 14:02 | #14734

I would like to express my deep felt appreciation to the Honourable Editor of the daily "THISDAY" and a hundred times more to the very specific Reporter who gathered enormous courage to expose and bring to light this yet "another stinking revelation of this incredibly heinous and blood-sucking swindle" which was again to be 'bambikizwaad" to the Danganyikans! Haya huyu Zitto na "Profesa"wake hawakuyajua haya?Walikuwa na nia gani na sisi Wadanganyika? Kweli kikulacho,ki nguoni mwako!Kweli haya ndiyo "kwa maslahi ya umma"yaliyokuwa yakitetewa na Zitto na Porosoo wake!Kwa haya yanayozidi kujitokeza sasa,na mengi yatajitokeza zaidi huko mbeleni,Watu kama Idris Rashid bado anatafuta nini pale TANESCO?Alitakiwa awe amesha jiuzulu nafasi yake WIKI ILIYOPITA!What the hell is he waiting for?Waiting to hear from the State House?Jamani tuache utani na UTUMISHI WA UMMA.Utumishi wa Umma its something sacred!If for one reason or the other a Chief Executive of a Public Utility commits a serious irresponsible blunder or a miscarriage of ethical codes of conduct purposely for personal gain or with an inclination of diverting the country into an economic sabotage of unimaginable proportions, then that CEO is no less than A TRAITOR to the Nation!He should immediately be removed from office,and be subjected to the scrutinity of the Laws of the Land!Hakuna ushikaji hapa.Do Him before We Do You!

na benitoz awaadh Njaggu, Morogoro road, DSM., - 13.03.09 @ 14:26 | #14739

Kumbe wakina Ngeleja na Idris Rashid waliposhupalia Taifa likubali kuinunua mitambo ya Dowans kwa bei "poa" ya shs.90 billioni,KUMBE,tayari Mitambo hiyo ilikuwa ikidaiwa na mabenki deni la shs.100 billioni!Walitaka kuwaingiza watanzania mkenge mwingine ili serikali ikubali kununua mitambo hiyo chakavu na kisha pesa hizo zitumike kulipia madeni ya Richmond/Dowans yanayodaiwa na benki za Barclays na Stanbic kiasi cha shs.bilioni 100 (?).Hapa kwanini MTU HAJAWAJIBIKA? This is very serious indeed? Haya Zitto kiko wapi sasa? Na huyo "profesa" akafundishe Kivukoni pale patamfaa,ndio mahala pake pa kupakua hizo pumba!lakini si pale Manzese,umechemsha kichizi!Whom To Trust in this Political Rust that has gone Bust for Lust of Must!

na ntendezeze, Bomani,Ilala;Dsm., - 13.03.09 @ 14:45 | #14741

Ukiangalia kwa makini kwa historia hizi wiki tatu zilizopita hasa Magazeti, Tanzania Daima, Majira,Mtanzania n.k waliipigia saana Dowans debe kuwa kwanini mannunuzi yasihalakishwe,ohoo bunge haliusiki, muhariri akaandika kupendezesha tenda mpaka nilishtuka!! Kuna magazeti wamekula pesa za Rostam Mungu ndiye anajua. Baada ya Nipashe na Mwananchi kukamalia hayo hayo magazeti yakabadilisha uhandishi ndo hii bado wanaendelea kuchokoza kuangalia upepo! Sasa tumeshawashtukia Tanzania Daima, Wananchi wako ngangali hata aje Slaa achana na Zitto hakiuziki kitu, bado tunakodelea kwa karibu vitambulisho sio tumesahau!! Take care

na maggy, tz, - 13.03.09 @ 15:09 | #14744

Hivi unaweza kununua kitu bila kujua MMILIKI wake? Je utamlipa NANI pesa za kununulia?.. Wasiotaka mmiliki ajulikane wajibu swali hili.

Tukubali kuwa Zitto amechemka kwa kushirikiana na mafisadi kujaribu kupigia debe ununuzi wa mitambo chakavu ya Richmond/Dowans.

Dk Rashid anatumia ushkaji wake na Mzee Mzima kujaribu kuwatisha waTz kwamba kama wasiponunua mtambo huo wa kifisadi basi Tz itaingia gizani, na eti asilaumiwe. THAT'Z BLACKMAILING!

Tunataka Serikali itaje rasmi jina la mmiliki wa Richmond/Dowans na Kagoda Agriculture ambayo nayo iliiba sh 40 Bilioni toka akaunti ya madeni ya nje (EPA) ya Benki Kuu. Jina hilo linatajwa sana mitaani na maofisini.
Kwanin m2 huyu anaogopwa na Serikali???!!!
Is this person the power behind the throne or what?

"WATANZANIA SI MABWEGE TENA!"



na Gota, Tz, - 13.03.09 @ 15:15 | #14745

HILI GAZETI LIMEISHIWA HABARI, HABARI INACHUKUWA SIKU 4 BILA KUBADILISHWA, HABARI NI ILEILE! INACHOSHA ANDIKENI HABARI ILI ZIENDANE NA WAKATI!KAMA HAMUWEZI KUTULETEA HABARI MPYA FUNGA MTANDAO WENU KAMA WALIVYOFANYA MAJIRA,POTELEA MBALI TUTASOMA MAGAZETI YA CCM NA IPPMEDIA

na Maisha Dunia Ngumu Jr, kisarawe-Tanzania, - 13.03.09 @ 15:46 | #14749
Andika maoni yako:
Jina:

Barua-pepe:

Mji/Nchi:

Maoni:
 
Hii nimeipata toka Raia Mwema la wiki hii 11/03/07 to 17/03/09 Toleo No. 72
Siri ya Zitto na Ngeleja yavuja

Mwandishi Wetu Machi 11, 2009




WAKATI hali ya umeme nchini ikiwa bado tete, barua ya siri kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuhusiana na sakata la umeme na hali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imevuja.

Barua hiyo inagusia ushauri wa kamati ya POAC kwa Serikali kuhusiana na kukabiliana na hali ya umeme, ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali kuingilia kati na kuinusuru Tanesco kifedha, bila kugusia mitambo ya Dowans ambayo imekua gumzo kwa sasa.

Ndani ya barua hiyo ya mwishoni mwa mwezi uliopita, ambayo Raia Mwema imeiona, Zitto, kwa niaba ya kamati yake, ameishauri Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwapo msaada wa dharura kwa Tanesco ili ijikwamue katika tatizo kubwa la kifedha na kuisaidia kununua mitambo ya kuzalishia umeme inayofaa bila kukiuka sheria za nchi.

"Kamati inawasilisha kwako ushauri wa kuiomba Serikali iiwezeshe Tanesco kununua mitambo ya umeme inayoona inafaa kulingana na mahitaji yake na bila kukiuka sheria za nchi ili kuliokoa Taifa kuingia kwenye giza na hivyo kuathiri uchumi wa taifa letu," inaeleza sehemu ya barua hiyo kutoka kwa Zitto.

Zitto, ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa shughuli za chama chake, alikataa jana kuzungumzia kuhusiana na kuvuja kwa barua hiyo akisema: "…nilikuwa nje ya nchi na nimekuja moja kwa moja huku Machame kwa shughuli za chama."

Kuvuja kwa barua hiyo kunakuja wakati Zitto anatajwa kama mmoja wa wanasiasa wanaoiunga mkono Tanesco katika mpango wake wa kununua mitambo ya Dowans, msimamo ambao umezua utata na kumuweka pabaya kisiasa, lakini alipoulizwa kuhusiana na msimamo wake kwa sasa alisema: "Msimamo wangu ni kuona nchi haipati giza na Watanzania wajifunze kuwa na viongozi ambao wana mawazo tofauti na wengi."

Ndani ya barua hiyo, ambayo nakala yake imepelekwa kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, kuna maelezo yanayoonyesha jinsi shirika hilo la umeme lilivyo na hali mbaya kifedha kutokana na sehemu kubwa ya mapato kutumika kununua umeme kutoka kampuni binafsi zinazozalisha umeme nchini.

Kuhusiana na ushauri wa serikali juu ya ununuzi wa mitambo barua hiyo inaeleza: "Kamati inapenda kuikumbusha Serikali kuwa maamuzi ya kununua mitambo ni maamuzi ya Serikali na si ya Kamati ya Bunge. Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali na si utendaji wa kila siku. Kamati yangu imetoa ushauri huu kuisaidia Tanesco kupunguza gharama za kununua umeme na kuongeza mapato yake kwa kutekeleza mpango wake wa wateja 100,000 kwa mwaka. Tanesco hawataweza kuunganisha umeme kwa wateja 100,000 kwa mwaka kama hakuna umeme wa kuwapatia."

Habari zaidi kutoka ndani ya Kamati ya Zitto zinaeleza kwamba baadhi ya wajumbe wameonyesha kuchanganywa na taarifa za vyombo vya habari zilizomnukuu Mwenyekiti wao akizungumzia Dowans wakati kamati haikuwa na maamuzi kuhusiana na kampuni hiyo.

Miongoni mwao ni Makamu Mwenyekiti wa Zitto, Mbunge wa Mbarali, Esterina Kilasi, ambaye alinukuliwa wiki hii akisema kwamba kamati haikuwa na maamuzi yoyote kuhusiana na Dowans.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo aliliambia Raia Mwema kwamba wajumbe wengi waliozungumzia suala la mitambo walibainisha kwamba Tanesco ni lazima inunue mitambo mipya na izingatie sheria.

"Baada ya Tanesco kuzungumzia dhamira yake ya kutaka kununua mitambo ya Dowans, tuliwaambia kwamba suala la kununua ama kutonunua ni suala la kiutendaji linalotakiwa kuzingatia sheria, ubora wa kitu kinachotakiwa kununuliwa na taratibu zifuatwe na tuliwasisitizia kwamba kazi ya Kamati na Bunge ni kusimamia," alisema Mbunge huyo.

Mbunge huyo ambaye alikataa kutajwa jina kwa kuwa si msemaji wa Kamati, alisema waliwaeleza Tanesco waziwazi kwamba kitendo chao cha kufika katika Kamati kutaka mpango wao wa kununua mitambo upate baraka, hakikua sahihi.

"Tulisikiliza nia ya shirika dhidi ya mitambo hiyo lakini hatukubariki ununuzi huo. Uamuzi wa kamati ni kuishauri Serikali kununua mitambo mipya kwa ajili ya tahadhari na kukabiliana na tatizo la umeme linaloweza kujitokeza kama Tanesco walivyoonya, lakini kwa kuzingatia ubora, sheria, kanuni na taratibu za manunuzi," alisema.

Mbali ya Zitto na Kilasi, wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Felister Bura, Diana Chilolo, Raphael Chegeni, Bahati Abeid, Emmanuel Luhahula, James Musalika, Peter Serukamba, Juma Njwayo, Tatu Ntimizi, Hafidh Ali Tahir, Elisa Mollel, Zaynab Vullu, Mwanawetu Zarafi, Mwadini Abass Jecha na Shally Raymond.

Mbali ya kutoa ushauri kwa Serikali, Kamati ya Zitto ilipendekeza kuwapo kwa kikao cha pamoja na kamati ya Nishati na Madini, maombi ambayo yalikataliwa na Spika Sitta, ambaye alibainisha wazi kwamba hakukuwa na sababu ya kikao hicho baada ya Kamati ya Nishati na Madini, inayoshughulikia sekta hiyo, uamuzi ambao unaelezwa kukubalika na kamati zote.

Tayari Tanesco wamekwishasitisha mpango wao wa kununua mitambo ya Dowans, lakini kwa taarifa ambayo ilitoa kitisho kwa wananchi kwamba kutakuwa na tatizo kubwa la umeme litakaloathiri sekta nyingi za huduma na uzalishaji.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa na Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Idris Rashid iliibua mjadala mpya wa kumtaka ajiuzulu kutokana na kutowajibika na kuutisha umma.

Katika tamko lake Dk. Rashid alisema: "Tanesco inatangaza rasmi kujitoa kwenye nia yake ya kununua mitambo hii. Ni imani yetu kwamba tumekwisha kujieleza na kujenga hoja za kutosha, na wananchi wa Tanzania, watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, hospitali hazitoi huduma, viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu tulishindwa kufanya maamuzi".

Sakata la Dowans limeibua mjadala mkali nap engine mgawanyiko wa wazi uliotokana na kauli za kukinzana kati ya wabunge wa kamati mbili ya POAC na ile ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM), William Shellukindo, anayesaidiwa na mwanasiasa machachari, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe tofauti ambazo zimejitokeza zaidi katika vyombo vya habari.

Shellukindo na Mwakyembe wote walionyesha kushitushwa kwao na taarifa za kamati ya Zitto kujihusisha na masuala ya kisera badala ya kupitia hesabu huku wakihusisha hatua hiyo na mikakati ya kisiasa.

Dk. Mwakyembe ndiye aliyesema kwamba upo uwezekano wa suala hilo kutumika kama sehemu ya kampeni za kisiasa za Chadema ambako Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wake, lakini Zitto akanukuliwa akisema suala hilo halina chembe ya siasa mbali ya maslahi ya Taifa.

Baada ya kauli za wabunge hao, Spika Sitta alifunga mjadala kwa kuishauri serikali kuachana na ununuzi wa mitambo ya Dowans kwa kuwa hauna maslahi kwa Taifa.
 
Mimi nasubiri mwali wa MMKJ maana sina comment kwa nchi iliyooza kama ya kwetu ambayo wezi(mafisadi) wanaiba pesa zetu wakati tunaona na wanawekewa kinga bila kushitakiwa
 
Jamani tujiulize unajua unapokwenda kukopa pesa hasa ukiwa na dhamana kama hizi ni mitambo na spare parts ambazo value yake inaweza kuisha kadri muda unapokwenda ni vigumu sana mabunki kukuamini mpaka awepo mdhamini anayeeleweka.

Je serikali haikujiweka kama mdhamini wa Dowans wakati anaenda kukopa pesa hizi benki?

kama ilidhamini itakuwa ni big loss kwa nchi yetu maana hawa jamaa watayaacha majenereta yao na serikali ikadaiwa kwani ni mdhamini (kama kweli alidhamini)

Na zaidi ya hapo, hivi hakuna Personal Guarantees za Ma-Director? na kama Zipo na akina nani Hao???
 
Back
Top Bottom