New revelation, Dowans in huge debt

Nijuavyo kama una deni na umeweka assets zako kama collateral security, huwezi kuziuza mpaka mkubaliane na hizo bank au aliyekukopesha.

Inaonekana huko bank kuna aliyepewa 10% maana asset za thamani ya 90 billion inakuwaje colatteral security ya 100m USD?. Halafu walikuwa wanatumia assets zile zile kupata mikopo kwenye bank tofauti!

Yaani the whole operation was run by debt!. Nisawa na JF tukipewa tenda ile maana tunakopa na kununua mitambo. Biashara ipo na mlaji yupo(Tanesco).

Bonge la deal!

I like it!
 
Mkuu Nyambala,

Mwenye Dowans anajulikana ila tatizo ni kwamba yeye mwenye na mafisadi wenzake hawataki hajulikane! Mambo ya kipuuzi puuzi tu!

Sawa kabisa baba Enock - Lakini si wakuu wetu wanataka kutuaminisha kwamba hajulikani?

Anywayz haya mambo mpaka lini? Mkjj are u sure we are nearing the beginning of the end? Haya mambo yanatia sana kichefu chefu!!!!!!!!! Watanzania tunazugwa mchana kweupeeeeeeeeeee!!!! Sasa napata picha kwa nini Salva alikuwa mkali pale gazeti la mwananchi lilipogusia muungwana kupigia debe manunuzi hata sheria isipofuatwa!!!!
 
Hii c zitto tu amabaye hajui habari hii ila ni watanzania walio wengi.Nina imani ngeleja na Rashid wanaelewa vizuri saana na walitaka wakalipe madeni sisi tubaki na giza vilevile. Magazeti mengi huwa yanaandika neno sirikali kama serikali-hakika hili neno lina ukweli kwa asilimia kubwa saana. Ndugu zangu watanzania,tukiona watu wanashabikia kitu saana kama ilivyokuwa dowans na washirika wake bila kumsahau mc sherukamab ujue kuna kitu. Tunashukuru kwa hiyo taarifa wakuu,yetu macho na masikio bila kusahau kutembelea ovuti yetu makini itupayo ukweli wa mambo!!
 
These people knew they WERE dealing with PURE NUTS. They knew in this country you can do anything, virtually anything, and go out with an applause!

It was such a huge STINK they knew someone will be BLOWN out of proportions.

I'm sorry for the grass that have been caught between the elephants' war

Career shattered, poor me!!
 
Zitto yuko wapi alikuwa anatuletea apology ndeeeeeeeefu kumbe mambo yenyewe ndio haya? Kweli njaa mbaya wadau, au mnasemaje?
 
Mi nadhani na haya mabenki yetu haya nayo inabidi yamulikwe, maana naona yameshibana mno na mafisadi.
 
Lets refresh our memories:

a. Haya majenereta yalinunuliwa kwa fedha za nani na kwa kiasi gani na kwa udhamini wa nani?
 
Duh, kweli hii ishue kumbe ni zaidi ya watu kujiuzulu, kuna more to it than one can imagine! Tatizo letu ni kwamba nchi inaongozwa kimeshimeshi (kama walivyosema wakuu humu jamvini)! Tukisema ni njaa inakuwa kama tunawaonea sababu hii ni sijui hata tusemeje manake ni uchafu mtupu, tena nakumbuka maneno ya Hayati Baba wa Taifa, "HUU NI UNYANG'AU NYANG'AU TU"
 
mishemishe si kitoto.. Lakini this is good because from this will spawn a new age. Tuombe uzima tuu
 
Lets refresh our memories:

a. Haya majenereta yalinunuliwa kwa fedha za nani na kwa kiasi gani na kwa udhamini wa nani?

shida yangu kubwa ni hapo kwenye udhamini! inawezekana Serikali ilitoa udhamini hasa kuiwezesha dowans kukopa kwenye hizo bank.

uummh! kesi ya Ufaransa wanatudanganya tu!
 
Duh, sasa kombe limefunuliwa.

Hapa kama watu hawatakwenda Kisutu basi tumekwisha.

Ndio maana hata usajili wa haya makampuni haueleweki-eleweki. Wanatumia majina ya watu ambao hawawezi hata kuomba mkopo kwenye Bank za kawaida, ili wao ndio wahukumiwe endapo deal itabunburuka. Watu hawa ni hatari sana.

Sijui kwanini DPP hachukui hatua haraka. Au kapewa amri ya kukaa kimya?

Nadhani mambo yapo bayana kuliko hata ile ya Mramba. Yona na Mgonja. Mambo yanaonekana wazi kabisa. Wafunguliwe mashitaka, wakajitetee mahakani. BASI.
 
Sasa ninaanza kuelewa kwanini waliokuwa wakitetea ununuzi wa mitambo hiyo walikuwa hawataki kabisa kuulizwa swali la legal ownership ya hiyo mitambo, maana wangezama sana hayo yote yangejulikana na deal lingeonekana ni chafu tangu mwanzo na hata hao waliokuwa wakiwa-support wangeogopa.

Hoja yao ilikuwa ni kwamba tusiangalie mmiliki wa mitambo ama historia ya mitambo, bali tuangalie mahitaji yetu na kumbe tulikuwa tunauziwa mzoga wa mbuzi ulio kwenye gunia.

Sasa iko wazi kwanini TANESCO na serikali walikuwa wanataka support ya Bunge. Maana kama Bunge lingeridhia basi tungekuwa tumeliwa na huyo msimamizi wa serikali angekuwa hana nguvu ya kuihoji serikali maana angeonyeshwa documents zinazoliunganisha Bunge kwenye huo ununuzi haramu wa mitambo.
 
Ama kweli hii ni hatari!!!!!Ina maana Waziri na Nishati na Madini,pamoja na mkurugenzi wa TANESCO .alikuwa hana taarifa ya hizi.Sasa hakika usaniiiiiii umepita kipimo.Naomba hawa viongozi wamrudie mungu wao.
 
kama ni kwa wale wenzetu wenye nchi za barafu.. this is the proverbial "tip of an iceberg"..

Hebu tujikumbushe kidogo kitu yaliyopita kabla ya kuvunjwa kwa mkataba:-

On Dowans, Dr Rashid said the legal consultants traced the origins of the firm all the way to Costa Rica, where it was registered as having a capital of only USD 100 and had no references.

``Both these companies (Dowans and Richmond Development Company LLC) were dubious and were shrouded in mystery,`` he said.

Explaining why they had given Dowans Tanzania Limited up to August 1 to close shop, he said it was a gesture of politeness so that Dowans would get a chance to fold up and settle the claims of their employees.

Responding to a request to reveal the identity of people behind Richmond Development Company LLC, he said Tanesco was dealing with the managing director of Richmond, Mohammed Gire.

``The problem is that people know that Gire does not have the financial capacity to run such a business. There are a lot of questions as to how he was awarded this contract and who are the persons behind him…because he only owns an internet café,`` Dr Rashid said.

Pressed to name individuals who were transacting with Tanesco on behalf of Dowans, he named them as Henry Surtees, who was the company representative, and managing director Guy Picard, who rarely visited Tanesco. Both are foreigners.

On whether the impact of Dowans withdrawal from power generation would be felt by Tanesco, Dr Rashid said: ``Their absence won't be felt.``

He added that Downs Tanzania Limited were generating 100MW and now Tanesco had already installed another 100MW power generating plant of its own at Ubungo, Dar es Salaam.

Asked whether Tanesco was mulling over the possibility of purchasing the Dowans plant, he said the possibility was very slight as such an arrangement ``will not help this nation.``

He said Dowans were supposed to move all their equipment from the site now that the contract was no more.


Huyu Dr. Idris Rashidi akibanwa ataweza kutufunulia mengi kuhusu wamiliki wa Dowans na alishinikizwa na nani hii mitambo inunuliwe. Kuhusu Zitto mmh, nakumbuka wengine tulimwambia mapema kabisa ajitoe, lakini aliamua kutetea alichoita msimamo wake eti kwa maslahi ya Taifa.

Sasa mimi nina"appeal" kwa Mh. Zitto, mbunge wa Kigoma kupitia Chadema awe mwungwana na akubali alighafilika. Gari karibu linaondoka na asipoangalia ataachwa kwenye mataa !! Hakuna tena atakayeweza kuzuia yatakayojiri baada ya muda si mrefu.
 
Mkuu Nyambala,

Mwenye Dowans anajulikana ila tatizo ni kwamba yeye mwenye na mafisadi wenzake hawataki hajulikane! Mambo ya kipuuzi puuzi tu!



Jina la mmiliki wa Dowans halitajwi kwa sababu jina lenyewe ni matusi matupu na halitamkiki wala halina silabi. ":,*.`><,~`
Unaweza kutaja tendo la kujamiiana na mkeo kwa kilugha mbele ya mzazi wako?
Basi nakwambia ni rahisi kutaja neno hilo la kiujamiiana kwa kilugha mbele ya mzazi wako kuliko kutaja jina la mmilikiwa kampuni ya Dowans pale Tanzania.
 
Kamati ya Zitto walilijua hili? Kama jibu ni hapana, je wapo tayari kubadili msimamo wao?

Kamati ya Zitto? Leave the Kamati out of this. Wenzake wamemruka masikini!


IPP MEDIA
09 Mar 2009
By Simon Mhina


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Estherina Kilasi ambaye pia ni Mbunge wa Mbarali (CCM)...alisema maneno ambayo yamemkariri Mwenyekiti wao (Zitto Kabwe) yalikuwa maoni yake binafsi na wala sio ya kamati kwa vile hakuna hata kikao kimoja ambako walikubaliana na ombi la kununua mitambo hiyo.

``Wala hatujawahi kutoa ushauri wowote juu ya suala hilo, zaidi ya kuwaelekeza Tanesco walifikishe kwa kamati husika ya Nishati na Madini,``alisema

Akifafanua, alisema kilichotokea siku hiyo ni semina ambayo Tanesco waliiandaa na kuwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuwaelezea mipango ya kununua mitambo ya Dowans kwa kuwa wana kiasi cha Sh. bilioni 60 kwa ajili hiyo.

``Sisi tuliwahoji kama mnazo Sh Bilioni 60 mnashindwajwe kuongezea kidogo ili mnunue mitambo mipya? Vilevile tukawahoji hivi mambo haya mnayotuambia kwenye semina wameyapeleka kwa wahusika ambao ni Kamati ya Niashati inayoongozwa na William Shelukindo?,`` alisema Kilasi na kuongeza:

``Baada ya hapo tuliwashauri suala hilo walifikishe kwa wahusika (Kamati ya Madini) na hakuna hata mahali pamoja tulipolitolea uamuzi suala hilo kwa vile halituhusu.``

Mbunge huyo alisema kufuatia kauli za Zitto ambazo zimezua malumbano, na kuifanya Kamati yao ionekane ina `walakini` wanamsubiri kwa hamu arejee ili wamuweka kiti moto.

``Unajua baada ya semina ile mimi nilienda Zambia, huku nyuma ndo nikasikia malumbano, lakini baada ya kurejea nimewauliza wenzangu na hasa makatibu wanaoandika muhtasari, kama kuna kikao kingine kimeketi na kutoa uamuzi, lakini wakasema hapana. Sasa tunamsubiri Zito arejee safarini ili tumuulize kulikoni? ``Alisema.

 
Hebu tujikumbushe kidogo kitu yaliyopita kabla ya kuvunjwa kwa mkataba:-




Huyu Dr. Idris Rashidi akibanwa ataweza kutufunulia mengi kuhusu wamiliki wa Dowans na alishinikizwa na nani hii mitambo inunuliwe. Kuhusu Zitto mmh, nakumbuka wengine tulimwambia mapema kabisa ajitoe, lakini aliamua kutetea alichoita msimamo wake eti kwa maslahi ya Taifa.

Sasa mimi nina"appeal" kwa Mh. Zitto, mbunge wa Kigoma kupitia Chadema awe mwungwana na akubali alighafilika. Gari karibu linaondoka na asipoangalia ataachwa kwenye mataa !! Hakuna tena atakayeweza kuzuia yatakayojiri baada ya muda si mrefu.

I love JF......Long live JF....!

Mag3 many thanks kwa kutukumbusha comments za DR.Rashid wakati ule wa uvunjwaji wa mkataba na Dowans?

Kwa nini huyu jamaa tena juzi alitaka kula matapishi yake mwenyewe? alisema, Dowans ni kampuni ya kitapeli ambayo wamiliki wake hafamiki vizuri, pia akaendelea kudai uvunjwaji wa mkataba ule haungeathiri kwa vyovyote vile uzalishaji wa umeme.....! Sasa haya ya kutaka kununua mitambo ya wahuni aliyaletaje hapa na kushabikia? je, suala nchi kuingia gizani linakujaje hapa wakati alisema hatungefeel pengo la Dowans?

Kweli za mwizi arobaini!
 
Mwanakijiji nadhani unataka kusema lakini hutaki. Ngoja nikusaidie kidogo uendeleze::

Rostam na Lowassa wanakabiliwa na losses kubwa mno kutokana na mitambo ya dowans na loans zake zenye interest kubwa kwani walitegemea Lowassa kama Prime Minister angepush, sasa kuondolewa kwake kumeleta matatizo mengi mno kwani hata zile hela Manji alizorudisha kama portion ya Kagoda wao ndio walitoa.

Sasa hivi imebidi hata sheria zitake kupindwa through TCRA ili Rostam/Lowassa waweze kuweka collateral ownership yao ya Vodacom wapate foreign loans kwani bank nyumbani wamekataa kutoa loans. Nadhani wanahitaji about $30million.

Tulipokuwa tunakuja juu kuhusu Dowans kuna mengi nyuma yake na issue ndio kwanza zinaanza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom