hafidh swed
Member
- Apr 9, 2014
- 45
- 3
vijana wengi wa tanzania hawana wanalolijua kuhusu siasa wanapelekwa tu na wachache waliosoma.
Hivi kwanini tusi washawishi Watanzania tuungane Tanzania Nzima Kudai Katiba mpya?
Tuungane kuidai Katiba mpya
Kutaka mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya Uchaguz ni fikra za kichama zaidi kwa sababu kuna mambo mengi ambayo sisi wananchi tunataka yabadilike na kusema kweli hili la Muungano na serikali 3 ni sehemu ndogo sana ya matakwa yetu ukifuatilia rasimu ya katiba.Amani kwenu wazalendo wenzangu:
Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.
Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.
Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.
Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.
Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
Kutaka mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya Uchaguz ni fikra za kichama zaidi kwa sababu kuna mambo mengi ambayo sisi wananchi tunataka yabadilike na kusema kweli hili la Muungano na serikali 3 ni sehemu ndogo sana ya matakwa yetu ukifuatilia rasimu ya katiba.
Kuiondoa CCM madarakani kupitia Katiba hii ni hofu mbaya sana ambayo inajenga uadui na ndipo tuliposimama kwa sababu CCM hawatakubali kubadilisha vipengele vya Katiba hii kwa minajiri hiyo, Na Katiba mpya ni kwa manufaa ya wananchi ambao wengi sii wanachama wa CCM, Chadema, wala NCCR na wanachokitaka ni katiba bora yenye uongozi bora. Uzalendo, uwajibikaji, uwazi na sifa zote zenye kuwapa haki kama raia huru wa nchi hii. katiba mpya yenye lengo la kuiondoa CCM pasipo Uwazi na uwajibikaji ni sawa na kubadilisha Ufalme ambao viongozi wengi wanautaka. Kila kiongozi anataka kuingia Ikulu kama kwamba ndiyo sababu ya kuitaka katiba mpya!
Nimewasikia wana siasa wengi wakitaka mabadiliko haya kwanza kwa sababu ya uchaguzi wa mwaka 2015 wakati ni wao ndio wametukwamisha hapa kutokana na siasa zao. Na vipi wananchi wategemee utawala mpya wenye kuwagharimu fedha nyingi, kodi kubwa, misamaha ya kodi kwa mashirika ya nje yenye kuhodhi asilimia 100. Vipi kuhusu sheria ya kuheshimu vyombo na taasisi za ushirika wa jumuiya za wakulima na wafanyakazi? haki za kumwondoa kiongozi katika madaraka anaposhindwa kutekeleza wajibu, haki ya wananchi kumshitaki kiongozi yeyote anaye fisadi kwa kutumia madaraka alokabidhiwa. Miiko na maadili ya Uongozi, Na sheria kuwa msingi wa kutoa haki kwa wananchi wote badala ya Uheshimiwa kuwa kinga dhidi ya sheria. Leo tunalia na Polisi chini ya CCM kesho tulie tena Polisi kuwa chini ya Chadema ikiwa sheria ni zile zile?
Amani kwenu wazalendo wenzangu:
Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.
Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.
Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.
Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.
Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
Katiba ya manyinyiemu imempeleka fulani msituni