New atcl you cant compare with precission

Mimi binafsi nilishachoshwa na monopoly ya Precisionair. Ticket zao ni ghali na ku cancel safari za ndege mara kwa mara. Mnaosema ATC haifai kuwepo, subirini Qatar Airways ikianza safari zake za ndani mwezi ujao ndipo mtaona utamu wa competition.
 
Jamani tuwape moyo wenzetu siyo kila kitu kibaya.Tuwape na mbinu za kuboresha huduma zao.Sio kuwa demoralize kila siku jamani

Shirika la ndege ATCL haliwezi kuimalika as long as Eng. Chambo na mtu anaitwa Kirenga watakuwepo pale wizara ya uchukuzi kwani hawa wawili wapo pale to frustrate every move ya kutaka kulifufua shirika hili na ni vizuri Mwakyembe akalielewa hili tatizo na kulishuhulikia mapema iwezekanavyo hata kama Chambo analinga kuwa Kikiwete ni ndugu yake na yupo pale kuhahakikisha kuwa wanajenga bandali Bagamoyo!!
 
Kuna kitu inaitwa national carrier ambayo ikiendeshwa vyema kama kenya airways au uganda airways ndo utaelewa kwa nini serikali imekuwa ikijitahidi kufufua atc. Its a pride and a prestige to have your own national carrier bearing your precious flag in international airspaces my dear. Tuisupport jamani atc

ATC is a pride to who? Is it a pride to the people who cannot clean water in Dar es Salaam? To the parents who do not seem to undestand why their children do not have a semblance of a class? Why cant we compare this to a father or mother who is always well dressed to preserve the integrity and pride of the family while the children have nothing to eat or wear?

I know that non-investment in ATC alone will never solve Tanzania's problems but there are many ATC-like projects in Tanzania. If we get rid of them we will surely save something.

I am more mad with ATC because I have witnessed the many times it has been raised from the ground only to fail again, from the days of Julius Nyerere. I can't even remember how many times this Corporation has been resurrected by our goverment.

Talk about Pride, who doesn't know that Cathay Pacific is a de facto airleine of Hong Kong although it is not government owned? I long to see a Cathay Pacific like airline in Tanzania!
 
Watz wengi naamini kama siyo ushabiki wa kijinga ni kurogwa tu,Precision hivi sasa zaidi ya asilimia 49 ni mali ya Watz ni vema pia kusuppor huko pia maana hisa zimeuzwa kwenye soko la hisa na wananchi wengi wamenunua hisa hizo.N jambo la kushangaza kuendelea kupiga madongo shirika ambalo ni mali ya WaTz wenyewe.Mie naamin ATCL ni jambo la muda na kwamba kukua kwake au kufa kwake kunategemea utashi binafsi wa viongozi wetu kupunguza ufisadi na wizi katika shirika.Nakumba muda fulani Kiwete alikuwa anakwenda Geita mgodini na kuzindua barabara ya Geita-Usagara na alikodi ndege ya Precision yeye na wajumbe wake na sisi kwenye uwanja tulichelewa karibu masaa mawili kwa kusubiria ndege hiyo.Na kwa kuwa ni shirika binafsi lazima serikali ililipa gharama zote kwa PA .Lakini kama leo hii Kikwete atataka kusafirina ATCL baada ya kuimarika malipo yanweza kufanyika baada ya muda mrefu au mwishowe kuwa madeni sugu kama inavyoonekana kwa mashirika kama Tanesco,dawasco n.k.Ni ushauri wangu tuunge mkono mashirika yote na kusiwepo fitina za hapa na pale.Kwa uzoefu wa kusafiri na Precision wakati ATCL ikiwepo wakati wa Mataka naamini PA deserves appreciation than what few members pretend on this forum.
 
Shirika la ndege ATCL haliwezi kuimalika as long as Eng. Chambo na mtu anaitwa Kirenga watakuwepo pale wizara ya uchukuzi kwani hawa wawili wapo pale to frustrate every move ya kutaka kulifufua shirika hili na ni vizuri Mwakyembe akalielewa hili tatizo na kulishuhulikia mapema iwezekanavyo hata kama Chambo analinga kuwa Kikiwete ni ndugu yake na yupo pale kuhahakikisha kuwa wanajenga bandali Bagamoyo!!
nami nitakuwa na imani nalo siku top positions zitakapotangazwa/kupewa watu walio huru bila influence ya siasa na ushikaji!
 
Kwa kweli management hii ni ya kupongezwa.Hongera zao ila wajpange walipe deni
 
Nachukua nafasi hii kuipongeza Management ya ATCL na Serikali kwa ujumla kufufua Shirika letu la Ndege ATCL.
Mimi ni frequent customer wa Precission but I have never got satisfied with their service. Jana nimepanda ATCL kwa kweli nimekuwa satisfied.

1. Bei ni nzuri sana inatofautiana na PW kwa almost 150% - I know those are introductory rates but I am sure they will shoot to 100%

2. Chakula safi - Huwezi linganisha na yale ma sandwich ya precission wanayotoa mwaka wa tano sasa

3. Aina ya ndege - Ni ndege mpya aina Boeng na siyo ATR wala Caravan

4. Service - Crews are matured and not these dotcoms stuff

Big ATCL big up Government but we need consistence

age dont matter cha msingi ni high quality customer service, hata hivyo vile vibinti vya PW vinatakiwa customer service training.
 
Kama wameipruvu big up! Ila cjui kama idadi ya ndege inalingana na wafanyakazi.na yale mambo yao ya ANY TIME CANCELLED (ATC) vp bado wanayo ama wanazingatia muda siku hizi?
 
Tuachane na kuponda kila kitu wakati huko nyuma tulikuwa tunalalamika kutokana na kuzidi kuangamia kwa shirika la ndege la Tanzania, huo sio ukomavu. Karibu mataifa mengi duniani yana shirika la ndege moja la kuaminika au zadi ya shirika moja. Hii ni kutokana na kwamba viwanja vikuu vya ndege humilikiwa na serikali, na hivyo kuwepo na shirika linalofanya viwanja vya ndege kuwa na uhai zaidi na papo kuliingizia taifa pesa badala ya kutegemea mashirika ya ndege ya nje ya nchi ambayo yapora pesa za nje kwa kuzitakatisha kihalali kutokana na mfumo wetu wa kuliyumbisha shirika la Ndege Tanzania ambalo siku za nyuma lilikuwa linakua kwa kasi ya ajabu hasa katika awamu ya kwanza.

Huduma bora na wahudumu makini ni njia mojawapo ya kuwa kivutio katika usafiri wa anga. Kwa nafasi kadhaa nilizosafiri nimeshuhudia mashirika mengi ya ndege za Ulaya hupenda kuwaweka wahudumu vijana zaidi kama kivutio kwa wateja, lakini tatizo utaona wasichana warembo hao wako kama urimbo kusahau wateja wengine na kuyumbia zaidi kwa wanaowakenulia meno yao na kuonyesha kuvutiwa na uwepo wao.

Mashirika ya ndege ya Marekani wahudumu wa ndani ya ndege ni matured ambao unaona wako makini sana na kazi yao, na hawana kitu kingine cha kuhangaika na mvuto wa mteja (abiria) fulani, ila utendaji wao, wajibu wao unaowafanya wawepo katika kazi hiyo. Zote ni mbinu nzuri ila kwa njia mbalimbali, nani ameweza zaidi katika hao wanaosafiri kwa ndege mara nyingi wanalo jibu.

Mashirika mengi ya Ulaya pombe ndani ya ndege ni mtindo mmoja, kuna wanaomaliza safari na kuteremka uwanjwa wa ndege wakiwa under influence, tofauti na ndege za Marekani marufuku pombe ndani ya ndege au ndege za uarabuni marufuku alcohol ndani ya ndege.

Kukodi ndege kwa mashirika mengi ni jambo la kawaida kutokana na gharama kubwa ya kununua ndege mpya, na pengine ndege mpya kuchukua muda mrefu kuipata kutokana na kwamba makampuni ambayo yana - assemble ndege si kwa mtindo wa magari kuwepo kwenye parking lot kusubiri wateja, bali ni kwa order tu ya wateja, na hivyo kuchukua muda kukamilika na wakati huduma inahitajika. Kuna mashirika mengi ya ndege ambayo huenda yamepoteza baadhi ya route zao na hivyo ndege zao kuwekwa kwenye list kubwa ya waiting, ni bora kukokdisha na ni nafasi nzuri kwa mashirika ambayo yanahitaji ndege za papo kwa papo kukodi ndege zao. Kwa nafasi shirika linapojaribu kusetirika kwa kutumia ndege za kukodi watakuwa na mkakati wa kuagiza ndege zao mpya.

Pamoja na uwepo wa baadhi ya mashirika Tanzania yanayohudumia usafiri wa anga, huduma yao huwezi kuilinganisha na shirika letu la ndege la Tanzania ambalo ndilo linaloweza kubeba jukumu kubwa kwa huduma na ufanisi. Mashirika binafsi yapo kwa masilahi binafsi na mashirika ya umma yapo kwa manufaa ya umma. Ndio maana mashirika mengi makubwa ya ndege ni yale yenye share kubwa na serikali za nchi na hupata unafuu kutokana na punguzo ya gharama za uegeshaji kutokana na kuwa na share hali kadhalika kivuli cha mkono wa chombo cha umma. Tusishanga mashirika binafsi kuwa na nauli kubwa tofauti na shirika la umma.

Ukisafiri nchi mbalimbali duniani utakuta kila nchi na kila kiwanja cha kimataifa kuhodhiwa na shirika la ndege la nchi kuwa kama kiwanja cha nyumbani. Hivyo nasi hatuna budi kuwa na mtazamo huo kwa vile tunao uwanja ambao hautufaidii moja kwa moja wananchi kama hatuna shirika la ndege la kitaifa. Tuwe na mtazamo wa kitafia na manufaa ya umma na taifa badala ya kuwa na mwono wa kuona tu mradi tuna ndege ziwe za shirika la umma au binafsi. Tusiwe wakandiaji tu wa kila kitu, pale wanapoonyesha dalili ya kuanza na kujipanga upya tuwatie moyo hiyo inaweza kuwa hamasa ya kujituma kufanya vizuri zaidi.

Mwezi mmoja uliopita pale Mtaa wa Samora nilikuwa natafuta ofisi ya Swiss Air, nikaamua kwenda pale ATC House nikijua wanajua iliko watanielekeza. Nilipofika pale ATC House iliniuma sana kuona jengo kubwa ambalo enzi hizo lilikuwa fahari ya shirika letu leo limebaki tupu, kwa wakati huo niliona wahudumu wawili pale ofisini na security officer, wakati enzi hizo ukifika pale palikuwa na uhai. Nawashukuru waninisaidia kunielekeza ilipo ofisi ya Swiss Air.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yape mpeni, Jana nimerudi na ATCL kutoka Mwanza Asubuhi, Service yao ni nzuri sana, na wanajua wanacho kifanya, Usafi, Crew Wenyewe wasafi sana, na Wana huduma nzuri sana.

Kweli mkuu hata mimi niliruka nao j5 nimewakubali wako juu international standard waendelee hivyohivyo wasiterereke tena
 
Watz wengi naamini kama siyo ushabiki wa kijinga ni kurogwa tu,Precision hivi sasa zaidi ya asilimia 49 ni mali ya Watz ni vema pia kusuppor huko pia maana hisa zimeuzwa kwenye soko la hisa na wananchi wengi wamenunua hisa hizo.N jambo la kushangaza kuendelea kupiga madongo shirika ambalo ni mali ya WaTz wenyewe.Mie naamin ATCL ni jambo la muda na kwamba kukua kwake au kufa kwake kunategemea utashi binafsi wa viongozi wetu kupunguza ufisadi na wizi katika shirika.Nakumba muda fulani Kiwete alikuwa anakwenda Geita mgodini na kuzindua barabara ya Geita-Usagara na alikodi ndege ya Precision yeye na wajumbe wake na sisi kwenye uwanja tulichelewa karibu masaa mawili kwa kusubiria ndege hiyo.Na kwa kuwa ni shirika binafsi lazima serikali ililipa gharama zote kwa PA .Lakini kama leo hii Kikwete atataka kusafirina ATCL baada ya kuimarika malipo yanweza kufanyika baada ya muda mrefu au mwishowe kuwa madeni sugu kama inavyoonekana kwa mashirika kama Tanesco,dawasco n.k.Ni ushauri wangu tuunge mkono mashirika yote na kusiwepo fitina za hapa na pale.Kwa uzoefu wa kusafiri na Precision wakati ATCL ikiwepo wakati wa Mataka naamini PA deserves appreciation than what few members pretend on this forum.

Hata NSSF na TANESCO ni mali ya watania pia.Wanafaidikaje na haya mashirika kama sio kichaka cha kuwaibia wananchi?. Nani anamaamuzi kwenye haya mashirika likiwemo hilo unasema tunamiliki 49%!!!!...Funguka !!
 
Tuachane na kuponda kila kitu wakati huko nyuma tulikuwa tunalalamika kutokana na kuzidi kuangamia kwa shirika la ndege la Tanzania, huo sio ukomavu. Karibu mataifa mengi duniani yana shirika la ndege moja la kuaminika au zadi ya shirika moja. Hii ni kutokana na kwamba viwanja vikuu vya ndege humilikiwa na serikali, na hivyo kuwepo na shirika linalofanya viwanja vya ndege kuwa na uhai zaidi na papo kuliingizia taifa pesa badala ya kutegemea mashirika ya ndege ya nje ya nchi ambayo yapora pesa za nje kwa kuzitakatisha kihalali kutokana na mfumo wetu wa kuliyumbisha shirika la Ndege Tanzania ambalo siku za nyuma lilikuwa linakua kwa kasi ya ajabu hasa katika awamu ya kwanza.

Huduma bora na wahudumu makini ni njia mojawapo ya kuwa kivutio katika usafiri wa anga. Kwa nafasi kadhaa nilizosafiri nimeshuhudia mashirika mengi ya ndege za Ulaya hupenda kuwaweka wahudumu vijana zaidi kama kivutio kwa wateja, lakini tatizo utaona wasichana warembo hao wako kama urimbo kusahau wateja wengine na kuyumbia zaidi kwa wanaowakenulia meno yao na kuonyesha kuvutiwa na uwepo wao.

Mashirika ya ndege ya Marekani wahudumu wa ndani ya ndege ni matured ambao unaona wako makini sana na kazi yao, na hawana kitu kingine cha kuhangaika na mvuto wa mteja (abiria) fulani, ila utendaji wao, wajibu wao unaowafanya wawepo katika kazi hiyo. Zote ni mbinu nzuri ila kwa njia mbalimbali, nani ameweza zaidi katika hao wanaosafiri kwa ndege mara nyingi wanalo jibu.

Mashirika mengi ya Ulaya pombe ndani ya ndege ni mtindo mmoja, kuna wanaomaliza safari na kuteremka uwanjwa wa ndege wakiwa under influence, tofauti na ndege za Marekani marufuku pombe ndani ya ndege au ndege za uarabuni marufuku alcohol ndani ya ndege.

Kukodi ndege kwa mashirika mengi ni jambo la kawaida kutokana na gharama kubwa ya kununua ndege mpya, na pengine ndege mpya kuchukua muda mrefu kuipata kutokana na kwamba makampuni ambayo yana - assemble ndege si kwa mtindo wa magari kuwepo kwenye parking lot kusubiri wateja, bali ni kwa order tu ya wateja, na hivyo kuchukua muda kukamilika na wakati huduma inahitajika. Kuna mashirika mengi ya ndege ambayo huenda yamepoteza baadhi ya route zao na hivyo ndege zao kuwekwa kwenye list kubwa ya waiting, ni bora kukokdisha na ni nafasi nzuri kwa mashirika ambayo yanahitaji ndege za papo kwa papo kukodi ndege zao. Kwa nafasi shirika linapojaribu kusetirika kwa kutumia ndege za kukodi watakuwa na mkakati wa kuagiza ndege zao mpya.

Pamoja na uwepo wa baadhi ya mashirika Tanzania yanayohudumia usafiri wa anga, huduma yao huwezi kuilinganisha na shirika letu la ndege la Tanzania ambalo ndilo linaloweza kubeba jukumu kubwa kwa huduma na ufanisi. Mashirika binafsi yapo kwa masilahi binafsi na mashirika ya umma yapo kwa manufaa ya umma. Ndio maana mashirika mengi makubwa ya ndege ni yale yenye share kubwa na serikali za nchi na hupata unafuu kutokana na punguzo ya gharama za uegeshaji kutokana na kuwa na share hali kadhalika kivuli cha mkono wa chombo cha umma. Tusishanga mashirika binafsi kuwa na nauli kubwa tofauti na shirika la umma.

Ukisafiri nchi mbalimbali duniani utakuta kila nchi na kila kiwanja cha kimataifa kuhodhiwa na shirika la ndege la nchi kuwa kama kiwanja cha nyumbani. Hivyo nasi hatuna budi kuwa na mtazamo huo kwa vile tunao uwanja ambao hautufaidii moja kwa moja wananchi kama hatuna shirika la ndege la kitaifa. Tuwe na mtazamo wa kitafia na manufaa ya umma na taifa badala ya kuwa na mwono wa kuona tu mradi tuna ndege ziwe za shirika la umma au binafsi. Tusiwe wakandiaji tu wa kila kitu, pale wanapoonyesha dalili ya kuanza na kujipanga upya tuwatie moyo hiyo inaweza kuwa hamasa ya kujituma kufanya vizuri zaidi.

Mwezi mmoja uliopita pale Mtaa wa Samora nilikuwa natafuta ofisi ya Swiss Air, nikaamua kwenda pale ATC House nikijua wanajua iliko watanielekeza. Nilipofika pale ATC House iliniuma sana kuona jengo kubwa ambalo enzi hizo lilikuwa fahari ya shirika letu leo limebaki tupu, kwa wakati huo niliona wahudumu wawili pale ofisini na security officer, wakati enzi hizo ukifika pale palikuwa na uhai. Nawashukuru waninisaidia kunielekeza ilipo ofisi ya Swiss Air.

Ufafanuzi wa maana sana Candid Scope,nakupongeza.Huwa tunatabia ambayo inashangaza sana hatuwezi kuwa tunalalamika tu hata pale tunapopewa habari ambazo zinamwelekeo wa kutatua tatizo.Biashara ni matangazo,kama kweli sisi ni wazalendo tujifikirie uzalende wetu ni kwa nchi ipi.Inashangaza kuona watu hawana mawazo chanya kwa mali zetu(zikiwa bado mikononi mwetu),zikishindwa kuendesheka wajanja wakizigawa kwa wageni tunaanza kupiga kelele kana kwamba tu wazalendo zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Precision air woboreshe huduma za vyakula kwene ndege zao sijui ni ubahili au nin wakati nauli ziko juu ile mbaya, Big up ATCL kazeni buti.
 
Kwani kutoka Mwanza Dar to and fro kwa 540, PW na ATCL nani anatukandamiza kwa bei?
 
Kwa kweli mimi sioni sababu kabisa ya kulitetea sana shirika la ndege la ATC ambalo limekuwa ni shimo lisilojaa. Ni mzigo kwa taifa letu. Hili shirika halijawahi kufanya vizuri hata kidogo. Kila wakati limekuwa kama nguo anayopewa mtoto asiyejiweza, ambayo inanunuliwa mpya halafu inavaliwa na kupendeza pale mwanzo na mwishoni inachakaa na kubakia tambala bovu ambalo halishoneki. Inatupwa halafu inabidi utafute pesa ya kununua nyingine. Hili shirika halijawahi kusimama peke yake. Kila wakati ni lazima serikali itupe pesa huko., tokea kuvunjika kwa EAA.

Watu wanazungumzia ufanisi wa ATC sijui ni lini liliwahi kuwa na ufanisi. Kuna wakati ATC ilimaanisha Any Time Cancellation. Kwa hiyo sikuelewi vizuri Candid Scope unaposema huduma za mashirika binafsi huwezi kuzilinganisha na zile za ATC. Shirika hili limeliza watu wengi sana lakini kuna watu wanalipenda kama mtoto mkiwa. Watu wanalipenda kwa vile ni la taifa. Ni sawa na kuwa na bendera ya taifa.

Inabidi tuelewe vilevile kuwa kudorora kwa huduma na nauli kubwa inayotozwa na mashirika ya binafsi inatokana na kuwa na monopoly. Kuingia kwa ATC kutafanya mashirika haya kupunguza nauli na kuboresha huduma zao. Kwa ATC itabidi waende "in the opposite direction" ili wakutane katikati, waongeze nauli na kupunguza huduma fulani fulani.

Kama kweli serikali inataka iwe na shirika zuri la ndege basi inabidi ilianzishe halafu liandikishwe kwenye soko la hisa watu walinunue. Hili nalo ni swala la kwenda nalo kwa umakini kwani tunao mfano TOL.
 
Back
Top Bottom