Network ya Seacom Tanzania ipo down

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,145
716
Bandugu;

Kwa wale wanaotumia network ya Seacom (fiber opic cable ya baharini) Tanzania, inasemekana kuwa mitambo yao ipo chini.

Hii imewaathiri watumiaji wengi wanaopata access ya Internet kwa kupitia makampuni ya simu nchini Tanzania.

Hivyo basi JF kwa watumiaji wa mtandao wa simu Tanzania itakua haipatikani.

Hii ni mara ya pili kwa network ya kampuni ya Seacom kuathirika namna hii.

Kama unamtafuta mtu aliyepo Tanzania na ni mtumiaji wa huduma hii na unamtafuta pia kwa njia ya internet atakua hapokei EMAIL wala kuwa na uwezo wa kujibu.

Haijajulikana mitambo itatengemaa saa ngapi. Hii imeanza mnamo mida ya saa nne asubuhi kwa saa za Tanzania.

MODS ujumbe ukifika mnaweza kuhamisha na kuiweka kwenye Tech.

Mjumbe hauwawi.

Fairplayer
 
Mimi mmojawapo tangu muda wa saa 4 na nusu asubuhi ngoma imekata - ni hatari kama hauna alternative link, nataka ku switch VSAT kwa muda huu. Nasikia hapo UK ndo kwenye tatizo...
 
Yaani haya madude sijui ni mashikoro si TZ wala KE maana nami niko na link na mtu wa kenya remote access kuna kitu twakifanya mzeee net iko ups & down al the time. sasa nadhani kama sio vitendea kazi duni vya SCom hapa kwa nchi zetu huku tutaishia kusema ni UK na kwingineko. Je tujiurize kwetu hapa TZ SCOM inafikaje DODOMA, ARUSHA, MWANZA, MBEYA na kwingineko au ndio watatumia ile Fiber Optic cable ya TANESCO ya miaka mingii??
 
Back
Top Bottom