Neti za olyset ni bomu!

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
3,587
4,323
Hivi karibuni jamaa yangu alikwenda dukani kununua neti ya olyset inayosifika kwa ubora wa kukinga mbu,akalipa sh 8000 akapewa neti ya olyset iliyofungwa kwenye mfuko wa nailoni wenye nembo ya tanzania( mama wajawazito na wenyewe watoto wachanga wanalipa sh 500 tu!)
neti za olyset wanasema zina dawa ya kujikinga na mbu kwa miaka 5 kwa maana kwamba mbu hatui kwenye hiyo neti ya olyset.
Baaba ya kuitumia kwa kipindi cha wiki 1 alishangaa kuona mbu wanatua katika neti hiyo na kufanya mashambulizi kama kawaida na pia ajabu kubwa ni kuwa mbu walipenya katika matundu ya hiyo neti na kuingia ndani ya neti.
Sasa swali linakuja je hii vita ya malaria ni porojo tu au kuna usanii ndani yake??
Kwanini neti zinazosifiwa na taasisi za afya hapa nchini ziwe feki kiutendaji?
Hivi waliotoa pesa za msaada kwenye huu mradi kama raisi bush au raisi clinton au bill gates wakiambiwa hivyo watatufikiria vipi sisi watanzania?watu wanaosaidiwa lakini hawataki kujisaidia wenyewe.
Hii misaada tunayopewa toka kupatikana uhuru nchi hii ingetumika ipasavyo si tungekuwa mbali sana kipindi hiki ?
 
Hii si vita ni ulaji wa kimataifa, na uzuri viongozi wetu ni mambumbumbu kwa hiyo wametoa eneo la ujaji. I submit
 
Hata hivyo sio mbu wote wanasababisha malaria. Ni mbu jike wa kabila ya Anopheles ndio anakunywa damu, kwa hivyo mbu dume anaweza kukufanyia kelele kwenye masikio lakini hana madhara.

Ile dawa inaua mbu wanaosababisha malaria tu. Au wataalamu nimekosea?
 
hapa nafikiri inakimbiza kwa mda tu kwani nakumbuka mimenunua 6000 nanilipoweka mwezi wa kwanza sikuona mbu kabisa walikimbia wote kwa kiasi kikubwa kweli kuhusu kupenya labda afungi vzuri jamani
 
Back
Top Bottom