Neno shemeji lina maana gani?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Nashindwa kujua maana hasa ya neno SHEMEJI.
Nasikia watu wakiitana shemeji shemeji.
Sipati maana halisi la neno hili shemeji kwani hata watu walioonana kwa mara ya kwanza, hawasiti kuitana shemeji.
Shemeji ni nani WANA-LUGHA?
 
Shemeji ni mtu aliye na udugu wa damu wa kikaka ama kidada na mwanandoa mwenzio.
Yaani mfano ni Kaka ama Dada wa Mkeo ni Shemejio vilevile kwa Mwanamke ni Kaka ama Dada wa Mumewe (japo mara nyingine Dada wa Mume huitwa Wifi likiwa na maana hiyohiyo ya Shemeji ila ni maalum tu kwa wanawake wenyewe, mwanaume haitwi wifi katika hali yoyote ile). Siku hizi pia watu wamekuwa wakitumia neno shemeji kwa mtu wa kabila jingine aliyeolewa/owa na mtu wa kabila lake, imekuwa ikitumika.
 
MAHMOUD
Mbona watu wanaoitana shemeji wala hawana undugu wowote?
Hujawahi kusikia watu wa namna hii?
 
MAHMOUD
Mbona watu wanaoitana shemeji wala hawana undugu wowote?
Hujawahi kusikia watu wa namna hii?

Mkuu Exaud, jamii za kitanzania zinaishi kama ndugu. Mfano mimi na wewe kama tunafanya kazi pamoja, tunasoma pamoja, tunaishi mtaa mmoja, ama ni marafiki, basi tunakuwa kama ndugu hivyo mkeo namuita shemeji. Na hata wasichana wakiwa marafiki, hujiona kama ndugu, hivyo mme wa rafiki yake humuita shemeji japo si ndugu. Vilevile hata kama nafanya kazi na binti ambaye kaolewa, ama nasoma naye lakini hatuna undugu, mme wake nitamuita shemeji.

Shemeji kwa Mme ni ndugu wa Mke wenye cheo cha dada, kaka ama binamu. Na vile vile kwa Mke ni ndugu wa Mme wenye cheo cha kaka na mabinamu wanaume, ikija ndugu wa mme ambao ni wadada na mabinamu ambao ni wasichana jina shemeji hugeuka na kuwa Wifi.
 
MAHMOUD
Mbona watu wanaoitana shemeji wala hawana undugu wowote?
Hujawahi kusikia watu wa namna hii?

EXAUD ni vizuri unaposoma post ya mtu akaisoma hadi mwisho, yaelekea maneno yangu ya mstari wa mwisho yalikupitia kushoto. hayo hapo chini.

Siku hizi pia watu wamekuwa wakitumia neno shemeji kwa mtu wa kabila jingine aliyeolewa/owa na mtu wa kabila lake, imekuwa ikitumika.
 
Mkuu Exaud, jamii za kitanzania zinaishi kama ndugu. Mfano mimi na wewe kama tunafanya kazi pamoja, tunasoma pamoja, tunaishi mtaa mmoja, ama ni marafiki, basi tunakuwa kama ndugu hivyo mkeo namuita shemeji. Na hata wasichana wakiwa marafiki, hujiona kama ndugu, hivyo mme wa rafiki yake humuita shemeji japo si ndugu. Vilevile hata kama nafanya kazi na binti ambaye kaolewa, ama nasoma naye lakini hatuna undugu, mme wake nitamuita shemeji.

Shemeji kwa Mme ni ndugu wa Mke wenye cheo cha dada, kaka ama binamu. Na vile vile kwa Mke ni ndugu wa Mme wenye cheo cha kaka na mabinamu wanaume, ikija ndugu wa mme ambao ni wadada na mabinamu ambao ni wasichana jina shemeji hugeuka na kuwa Wifi.

Watanzania tumezidi kukwepa ukweli. Badala ya kumwita mke wa rafiki yako jina lake (mfano Mary) au mke wako kumwita rafiki yako wa jina (mfano Jumanne) tunaendekeza mambo ya kuitana shemeji pasipo sababu. Kwa hiyo watoto wanakuwa na baba wadogo na auntie wasio hesabika. Matokeo yake watu hao wanatumia hizo nafasi kufanya maasi kama kutongoza shemeji zao au kunajisi watoto. Mimi napenda watoto wangu wamwite rafiki yangu kwa jina lake mfano Mr Petro au Mama Petro. Shemeji ibaki kwa ndugu wa mke kwa upande wangu au ndugu zangu kwa mke wangu. Kwa maana hiyo watoto watajua shangazi, wajomba, baba/mama wadogo zao ni akina nani. Shida inakuwa pale ambapo ndugu anakuwa na uhusiano wa mbali ambao unahitaji kama dakika 5 kuulezea. Ila watu wa muhimu wabaki hao niliowataja!
 
Watanzania tumezidi kukwepa ukweli. Badala ya kumwita mke wa rafiki yako jina lake ........tunaendekeza mambo ya kuitana shemeji . . . Shemeji ibaki kwa ndugu wa mke kwa upande wangu au ndugu zangu kwa mke wangu......Shida inakuwa pale ambapo ndugu anakuwa na uhusiano wa mbali ambao unahitaji kama dakika 5 kuulezea.

DARK,
Mawazo yako ni changamoto kubwa sana.
Inamaanisha tumeshapoteza maana ya shemeji kwa lugha ya kiswahili.
Sijui wa JF wengine wanamchango gani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom