neno moja ndani ya katiba.Mh Zitto angeweka acauntability(uwajibikaji),wew e je?

.Daniel.

Member
Oct 19, 2011
21
8
wakuu tukiwa tunaelekea kwenye katiba mpya napendekeza lifuatalo;
tuweke maneno tunayoamini kuwa ni ya msingi kwenye katiba mpya kwa ajili ya tafakari zaidi
bones are made before the flesh and the flesh before the skin.

kwa kuwa JF have great thinkers nategemea bones are going to be made.nalianzisha kwa kuanza na mifano,kama ifuatavyo;

Mh Zitto alipokuwa anahitimisha hoja ya kamati ya kudumu ya bunge ya mashirika ya uma alisema;
kama kuna neno moja ambalo lingetakiwa kuwa kwenye katiba basi neno hilo ni 'Acauntability'(uwajibikaji)


wewe unasemaje? siyo lazima liwe neno hata sentensi unaweza kuweka ila epuka maneno mengi,sema tatizo na ufumbuzi.
mfano:kutokana na serikali kuu kuonekana kuwa mbali na jamii,CHADEMA tunapendekeza serikali za majimbo-Mh Mbowe.

mimi napendekeza lifuatalo;
neno ningeweka 'haki'.
kwa kuwa mahakama ndiyo chombo cha kutoa haki na kwa kuwa haki ndiyo msingi wa amani ni lazima mahakama zetu ziwe huru ili ziweze kutenda haki; napendekeza mapato ya serikali yagawanywe na yaainishwe in percentage kwenye katiba kwa mihimili yote mitatu (bunge,mahakama na serikali)

wewe unapendekeza nini? kwa ajili ya kutatua tatizo gani? tupe maoni yako tuyatafakari kwa maslahi ya taifa.
Karibu.
 
Back
Top Bottom