Elections 2010 Neno moja la dr. Slaa linaweza kubadilisha nchi

kwanza niwapongeze wana JF popote mlipo. Nimejaribu kufuatilia thread nyingi katika forum hii na nimegudua kuwa watanzania wengi wanasubili nini Dr. Slaa atasema ili watekeleze. Hii inaonesha ni namna gani watanzania walifanya maamuzi ambayo hayakupewa thamani.

Tumwombee kwa Mungu Dr. Slaa awe na hekima kuu ili aweze kuivusha nchi hii katika vuguvugu hili ambapo hata aliyetangazwa kuwa mshindi hana furaha na urais wake maana wananchi hawamuungi mkono!

Utaona thread zinasema ... Tunangojea Dr. Slaa atamke, tutekeleze. watz wana imani kubwa naye

JAMANI DONT REDUCE JF TO GARBAGE.
NINA WASI WASI BAADA YA WALIOTUHUMIWA KUWAIBIA KURA WATANZANIA SASA WANAANZISHA MIJADALA YENYE MWELEKO WA UCHOCHEZI WA KUMPINGA RAIS ALIYEAPISHWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILI KUPATA BASIS YA KUIFUNGA JF.

KATIKA MADA YAKO UNADAI KUWA "
Nimejaribu kufuatilia thread nyingi katika forum hii na nimegudua kuwa watanzania wengi wanasubili nini Dr. Slaa atasema ili watekeleze" WHAT IS THE RELATIONSHIP BETWEEN IDADI YA WANAJF NA WATANZANIA WENGI ULIODAI WANASUBIRI KAULI YA DR SLAA?

UMEENDELEA KATIA MADA YAKO KUWA "
ambapo hata aliyetangazwa kuwa mshindi hana furaha na urais wake maana wananchi hawamuungi mkono!" HUU NI OUT RIGHT UCHOCHEZI WENYE NIA YA KUWAINGIZA WENGINE MKENGE. NAOMBA USHAHIDI KUWA WANANCHI WA TANZANIA HAWAMUUNGI ALIYETANGAZWA NA KUWA MSHINDI; NA KWA KUWA ULIKUWA UNAMAKE REFEENCE KWENYE UCHAGUZI MKUU NA DR SLAA BILA SHAKA UNAMLENGA MHE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE. VILE VILE TUPE USHAHIDI NA UTUELEZE VIPIMO VYAKO VYA KUBIANI FURAHA YA MTU?

 
hayo uyasemayo ni ya kweli sehemu nyingi amebatizwa jina la; 'kamanda". Neno lake linasubiriwa kwa shauku kubwa kila upande. Tumuombee kwa mungu aendelee kumpa busara ili aweze kuvusha nchi yetu katika kipindi hiki kigumu.

acha kuwashabikia watu wenye malengo yao baada ya kutuibia kura zetu, unaweza kutuambia wapi na wapi wanakosubiri neno lake?
 
Hivi vijana wa KITANZANIA,, mtaacha lini kujidanganya na kuishi kwa ndoto?????
nchi haiwezi kukombolewa na vijana wajinga ambao hawataki kuamini ukweli, wanaishi kwa kujipa matumaini hewa, hawajiamini na hawataki kuukubali ukweli na pindi wakiukubali wanataka kuupindisha kwa makusudi.
HUYO BABU YENU SLAA, anajuta ni kwa nini aligombea URAIS, anajua alishindwa na hata viongozi wa chama chake wamemuacha peke yake athibitishe uendawazimu wake(jaribu kumpelekea microphone kiongozi yeyote wa chadema uone atakavyokimbia).
mnasikitisha sana vijana wa kitanzania........
mtabaki kuwa watumwa wa CCM katika nchi yenu
mtabaki kulamba viatu vya wanasiasa uchwara wa chadema mpaka pale kitakapotoweka katika ramani ya nchi
mtabaki mkiuota ukombozi wa nchi huku mkidhani hiyo kazi inatakiwa kufanywa na watu fulani na sio ninyi
mtabaki kuwa wapiga soga vijiweni, wavivu wa kufikiri na msio na utashi wa kuamua.
mtabaki kufikiria kwa kutumia magazeti na wala sio kwa kuzifikirisha bongo zenu
utashi wenu utaongozwa na imani za kidini (dini za kikoloni) na sio uwezo wa akili zenu kuchanganua mambo
hamtaacha kulalamika,hamtaacha kujidanganya, hamtaacha kujipa matumaini hewa,hamtaacha kuamini watu wasioaminika,hamtaacha kukabidhi hatma yenu mikononi mwa wanasiasa, hamtaacha kusujudia na kuabudu wasiostahili na HAMTAKUWA NA UWEZO WA KUUKABILI UKWELI NA HIVYO KUTOKUWA TAYARI KUPAMBANA NAO kwani vijana wengi wa kitanzania hususan wasomi ni COWARDS.

Inaonekana wewe una matusi sana.

Kwa sababu umekwisha kutuambia kwamba sisi ni waoga nakupa ahadi moja tu kwamba nitakula sahani moja na wewe mpaka umeze kauri zako zote.

Ni Ndoto gani ambayo tumejiviriga nayo na kuifanya dira ya maisha yetu??

Tunajidanganya vipi? Ni vema utoe mfano wa kueleweka.

Tumesoma, kama ambavyo mwenyewe umesema. Tunafanya kazi na kuingiza vipato halali tunachambua matukio ya kisiasa kwa kutumia vigezo vya Uelewa wetu. Tunapima Ukweli na Ulongo katika mzani wa Haki bila kuwa Biased.
Hapo kosa letu ni nini, KUSOMA au kuelimika??

Kuhusu kuupindisha ukweli kwa makusudi. Toa mfano moja namna tuupindishavyo ukweli? Toa Tukio halisi ambalo linasuport usemi wako.

Mimi na Wewe siyo nafsi ya Dr Slaa.

Habari za kujuta kugombea Urais ndo kwanza nazisikia kwako.

Ni Dr Slaa aliyekuambia kwamba anajuta au wewe unadhani anajuta? Au mmejadiriana KICHAMA?

Ukitaka kujua Habari za Dr Slaa unamwuliza DR Slaa siyo MH Mnyika.

Kweli sisi tunasikitisha sana kumlamba miguu kama siyo Nyayo Mwanasiasa Dr Slaa bila yeye kutupatia Kofia TShirt za Yanga wala nini. Huu ni ujinga kumlamba mtu miguu wakati hana Fedha wala mgawo wowote wa kifisadi na hana uwezo wa kutuhonga U DC.

Hata hivyo nina swali. Ni vipi tunamlamba miguu Dr Slaa?

Ni Kweli Tutabaki kuwa Watumwa wa CCM katika nchi yetu.
Nafurahi sana hata wewe mwenyewe bila kushawishiwa na Kibaraka yoyote wa CHADEMA unakubali kwamba CCM chama cha Wakulima na Wafanyakazi kina Watumwa nchini Tanzania na wengi wao ni Vijana wasomi.
Hapo mimi sina la kuongeza. Last Time niliposoma Historia ya Dunia, niliona utumwa ni jambo linalopigiwa kelel sana na halina nafasi mahali popote duniani.Je CCM wako tayari muda ukifika wa watumwa kuwekwa Huru??


Umesema Tutabakia Kulamba Viatu vya Wanasiasa Uchwara wa CHADEMA mpaka kitakapotoweka.
Hivi umejiuliza swali kwa nini tunalamba viatu bila kupewa chochote?
Kwa nini tunashindwa kulamba viatu vya Viongozi wa CCM wanaogawa fedha mbuzi kila uchaguzi ukija na kuishia mara wakichaguliwa?
Sasa kama tunalamba viatu watu wasio kuwa na Dola?
Hujilizi nini kitatokea siku wakishika Dola?


Hili la kuota Ukombozi na kudhani kwamba kazi ya kuleta ukombozi ni yawatu fulani, ni jambo ambalo limeniingia sana. Nakuahidi kwamba nitalifanyia kazi. Nashukuru kwa ushauri wako mzuri. kweli ni ujinga wa hali ya juu kuwa na Elimu ya Shahada ya Chuo kikuu na kuachia watu wazembe na wenye mawazo duni kujipenyeza katika siasa na kutuongoza katikamfumo wa uchumi wa kuzimu.

Tulipokuwa vyuoni tulikuwa tukitumia vichwa vyetu kufikiri hadi tukahitimu. Kwa changamoto yako yenye mguso, vijana tutaacha uvivu na nakurejea ari yenu ya zamani na kujiingiza ipasavyo katika siasa.


Kuhusu Utashi wa kuongozwa na Dini za Kikoloni hilo sijui kama nimekuelewa sana.


Uislamu uliletwa na Wakoloni wa KIARABU kutoka UARABUNI.
Ukristo uliletwa na Wakoloni wa Kijerumani na Kiingereza kutoka Ulaya.

Sisi siku zote tulikuwa na Matambiko ya Jadi ndiyo dini yetu asilia haikuletwa na mtu yeyote tuliianzisha wenyewe.

Ina maana unatushauri kujenga Imani kwa Dini zetu za Asili za Matambiko?
Au ulikuwa na maana moja kati ya dini hizo mbili Uislamu na Ukristo ni ya KIKOLONI???

MH Kikwete ni muislamu Dini hiyo ililetwa na Wakoloni MH Dr Slaa ni Mkristo Dini hiyo ililetwa na Mkoloni wote wana imani katika dini za kikoloni. Mimi ni mKristo dini yangu ililetwa na Mkoloni.Watanzaia asilimia 75 wanaamini dini zilizo letwa na wakoloni hapo kweli sikuelewi.


Naomba uelezee vizuri suala hili la Dini za wakoloni.


Yule MwanaSayansi Gwiji Albert Einsten alisema wazi kwamba"Imagination Is Better Than Knowledge"
Leo tunasafiri kwa ndege kwa sababu Akina Wright Brothers waliwahi kuota na kujipa matumaini kwamba kitu kizito zaidi hewa kinaweza kuruka na kusafiri angani.
Watu wanaamini kwamba wanaweza kusafiri na kuanzisha Koloni Sayari ya Masi, wanaamini kwa sababu wanaimagine hivyo.

Tunaishi kwa matumaini,tunaishi kwa matumaini kwamba Taswila tuzijengazo akilini mwetu juu ya kujenga upya nchi Yetu Tanzania katika mwelekeo wa kutuondoa hapa kama taifa na kutupeleka kule kama taifa ni Darubini ituonyeshayo visivyoonekana kwa macho na visivyogusika kwa mikono lakini viwezavyo kutafsiriwa kwa vitendo na kufanywa vitu halisi.

Ukomo wa shughuli yeyote afanyayo mwanadamu huhitimishwa na mipaka yake ya Taswila azijengazo akilini mwake.


Hapa ninaandika kwa kutafsiri sehemu ya taswira kutoka katika ubongo au akili yangu.

Wewe pia umeandika maneno yote haya kwa kutafsiri katika maandishi sehemu ya Taswira zilizomo ubongoni au akilini mwako.

Maandishi yetu wote hapa yamo ndani ya mipaka ya Taswira zijengwazo akilini mwetu.

Ufinyu au wembamba wa hoja si uwezo wa kushindwa kuandika herufi bali ni ufupi wa masafa ya kujenga Taswira akilini.

Uzuri au Ubaya wa kitu hautokani na kitu kilichopo mbele yetu kionekanacho kwa ucchi wa macho yetu bali ni tafsiri itolewayo na Taswira zilizomo akilini mwetu.
Ndiyo maana kuna watu wengi Tanzania wanaamini WIZI ni jambo ZURI pia ni Jambo lenye kuleta na kutia ushawishi wa maendeleo.

Wakati huohuo kuna kundi la Watanzania wengine wanauona wizi ni jambo BAYA lenye KUDHURUMU HAKI na kuleta MIFARAKANO isiyo ya lazima, Pia wanauona wizi kuwa ni KOSA LA JINAIkadri ya uwezo wao wa kutafsiri katiba ya nchi na sheria za nchi.

Uzuri upo hapa JF utajionea mwenyewe jinsi utakavyo gubikwa na kugubika Taswira zenye Masafa marefu katika Short Wave Band.

MH NOTRADAMME naomba unisamehe sana kwa huu mzalendo wa Daily NEWS, haikuwa nia yangu kukuchosha kwa upumbavu.
 
Hana lolote wala chochote. Hii ni forum maalum ya Chadema na kila anepingana na Padre Dr wa Kikatoliki Slaa basi anafungiwa.

Ameangukia pua sasa anaugulia.
[/B]

hivi una tatizo gani na ukatoliki.inaongelewa siasa unaingiza dini.tabia hii ni chafu sana ,wa2 wenye mawazo mgando kama wewe muyapeleke pale mtaa wa msimbazi au buguruni.wake up! naamini we ni msomi huna cha kudiscuss zaidi ya Ukatoliki wa Dr slaa.unaboa !!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom