Neno La Leo: Wiki Ya Maji Na Helikopta Arumeru!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Nchi yetu inaingia gharama zisizo za lazima kama ambazo nchi inaingia kwa sasa kwa wagombea, vyama na hata Serikali kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo.

Tumeona hata helikopta zenye gharama nyingi zikiruka kilomita nyingi angani eti kwenye harakati za kusaka kura kwenye chaguzi ndogo huku wananchi wengi wa jimbo husika wakitembea kilomita nyingi kusaka maji ya kunywa na kupikia.

Wiki kama hii ya Maji inayoendelea sasa ilipaswa kuwa wiki ya kuomboleza uhaba wa maji unaochangiwa pia na matumizi mabaya ya rasilimali za wananchi kama haya ya kuendesha chaguzi ndogo kule Arumeru Mashariki.

Na hili ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa
 
Unapokua na mwandishi wa habari anayeshindwa kutofautisha kati ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi na mipango/miradi ya maendeleo ni janga kwa taifa.

Ndugu Mjengwa unatoa wapi ujasiri wa kufananisha vitu hivi viwili wakati hata kwa akili ya kawaida haviendani?
Fikiria zaidi ya urefu wa pua yako.
 
Asiwape shida tunajua siasa zake........ jinsi anavyotumika
Ninacho kiona hapa ni kwamba Hoja ya maggid ina falsafa kubwa iliyo wazidi uwezo kuielewa
 
Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba bei ya mafuta ya ndege(helkopta) ipo chini ukilinganisha na bei ya petrol na diesel so kutumia helkopta ni kusave matumizi
 
Ninacho kiona hapa ni kwamba Hoja ya maggid ina falsafa kubwa iliyo wazidi uwezo kuielewa
Kuna falsafa gani hapo??

Kwanza aiambie serikali hii iache tabia ya 'KUAZIMISHA'

Nchi ya kuazimisha.............unaazimisha nini wakati hujafanya chochote!!

Argue during planning and not spending!!!...........during budgeting nyote mnakaa kimya, wakati zikianza kuliwa ndo mnashtuka usingizini...
 
Leo ndoo ya maji kata ya mabibo, jimbo la ubungo tunanunua sh 1000, chini ya kamanda Mnyika.
 
Back
Top Bottom