Ndugu Zangu,
PARADOX ni ile hali ya maelezo kupingana yenyewe. Kutokuwepo na lojiki ya jambo zima. Haujapita mwezi tangu pale Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijitokeza hadharani na kuunga mkono hudumna ya tiba ya Babu wa Loliondo ikiwemo madai ya Babu mwenyewe, kuwa dawa yake inatibu UKIMWI mbali ya maradhi mengine mengi.
Ni heri Pinda angekaa kimya, maana, Juni mwaka huu Umoja wa Mataifa unaadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya UKIMWI. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alikuwa Kenya majuzi kuzindua mwanzo wa maadhimisho hayo ambayo kidunia yatafanyika Kenya.
Na leo Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kuzindua Mkakati wa Taifa wa Kinga ya UKIMWI (2009-2012), pamoja na Mpango Kazi kuhusu Jinsia na UKIMWI (2010-2012).
Tunaambiwa, kuwa uzinduzi huo unafanyika ikiwa ni moja ya sehemu ya ushiriki wa ugeni wa Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia UKIMWI (UNAIDS) Bw. Michel Sidibe.
Tunaambiwa pia, kuwa wakuu hao wa Umoja wa Mataifa wako nchini kwa ziara ya siku mbili kuongeza hamasa kwa nchi za Afrika kutilia mkazo zaidi kinga ya UKIMWI ili kupunguza maambukizo mapya hadi kufikia sufuri hasa wa kizazi kipya, ifikapo miaka mitano ijayo, pamoja na kuhakikisha kuwa vifo vitokanavyo na UKIMWI navyo vinapungua.
Ukweli ni huu, kuwa kwa Serikali yetu kushadidia tiba ya Babu wa Loliondo kabla hata haijathibitishwa kitaalamu kuwa inatibu UKIMWI inachangia katika kuongeza maambukizi mapya ya UKIMWI, maana, kuna Watanzania leo walioaminishwa kuwa tiba ya UKIMWI imeshapatikana. Wanaendeleza ngono zembe, si kuna Kikombe Cha Babu!.
Mbaya zaidi, Serikali kupitia Wizara ya Afya haijaweka msisitizo kwa wanaotumia ARV's kuendelea kutumia dawa zao hata baada ya kikombe cha Babu. Hili ni pigo kubwa katika mapambano yetu dhidi ya UKIMWI.
Kwetu Watanzania hiki kinabaki kuwa kizungumkuti, a paradox! Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid
Iringa,
Jumatatu, April 4, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo