Neno La Leo: Mizan Al Haq!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,


Mizan al haq ina maana ya mizani ni haki. Asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Mkulima anategemea mzani ili uamue uzito halisi wa ujazo wa mazao yake.


Lakini, ni mzani ndio umechangia kumdidimiza mkulima wa Tanzania. Wafanyabiashara wengi wenye kutumia mizani katika kununua mazao ya mkulima wamekuwa wakifanya hila na mizani hiyo, hivyo, mara nyingi katika kilo mia moja za mkulima, kilo kumi au hata zaidi huliwa na mzani. Mkulima anadhulumiwa.


Ona mfano huu, miaka ya sabini Tanzania ilikuwa ikisifika kwa kuuza pamba bora duniani. Nchi ilipata mapato ya fedha za kigeni, na mkulima akanufaika pia. Lakini, wakulima wa pamba walipogundua kuwa wenye mizani wanawafanyia hila na kuwadhulumu kilo zao, basi, nao wakaanza kutia maji pamba yao ili uzito uongezeke, na wakati mwingine walichanganya na mchanga. Matokeo yake, pamba ya Tanzania ikakosa ubora, na soko pia. Nchi inakosa mapato, na mkulima pia.


Swali, tume ya kudhibiti mizani inafanya nini? Maana, mizan al haq- mizani ni haki. Kama mizani haitoi haki tunafanyaje?


Maggid Mjengwa
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.com
 
Back
Top Bottom