Neno La Leo: Kuna Tofauti Ya Mjinga Na Mpumbavu!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,

KUNA tofauti ya mjinga na mpumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; ” Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”. Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.

Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndio maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?

Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid
Iringa,
Jumanne, Machi 22, 2011
http://mjengwa.blogspot.com
 
hamna kitu humu. yale yale tu niliyofundishwa na marehemu bibi.

ngoja nichek mabandiko mengine.
 
Ndugu Zangu,

KUNA tofauti ya mjinga na mpumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; " Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza". Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.

Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndio maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?

Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; " Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!" Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid
Iringa,
Jumanne, Machi 22, 2011
http://mjengwa.blogspot.com

He! kumbe upo!! Kwani faidika na kampeni za ccm 2010 tayari imeisha..!? Nilikuwa napita tu.
 
Mkuu unaweza kuwa unarekebisha title zako?

Maana haingii akilini ukisema NENO LA LEO

NINI MAANA YA NENO LA LEO?
 
Kings, asante sana.

Neno La Leo Ni Neno tu. Neno huru. Nimelitoa leo. Nawe umetoa Neno lako, leo, nalo ni Neno La Leo. Tutafakari Neno, basi!
 
Majjid nasikia CCM wamekulipa mafao yako kwa kuwapigia kampeni vizuri na ninasikia wewe ndiyo uliyehamasisha vijana kinondoni waandamane kuunga mkono hotuba ya rais, sawa fanya vyovyote lakini kumbuka CDM tupo kwa ajili ya kuuwa wadudu wanaoruka na wanaotambaa,maana yangu tunapiga CCM, CUF pamoja na viroboto wengine
 
Mpumbavu Ni Mpumbavu Tu awe amesoma au hajasoma....same applies kwa Mjinga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom