Neno La Leo: Baba Mobutu; Tikala libela, lokuta monene!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,

WAKONGO wa Kinshasa na kwengineko wanaujua wimbo huu; ”Papaa Mobutu ee, lokuta monene, oy'akanisaka, MPR ekokufaha, wayahaa, Tata Marechal, tikala libela, tata Mobutuee, tikala libela, ...!”

Makala yangu ya juma lililopita imepekelea baadhi ya wasomaji wangu, na hususan vijana, kutaka kufahamu zaidi habari za Joseph Mobutu. Kuna aliyeniandikia akisema; kwa anavyoiangalia jamii yetu hii, kuna anaoyojifunza kutoka kwa yaliyomkuta Mobutu.

Mobutu ni kielelezo kizuri cha hulka za watala wengi wa bara letu.
Na Afrika utazionaje dalili za Chama cha siasa kinachokufa? Jibu; ni pale ’Kiongozi Mkuu’ anapoanza kujitenga na umma, kwa kauli na matendo. Kuna wenzake wachache pia ndani ya Chama watakaokuwa na hulka hiyo. Chama cha siasa huonekana kuwa mbali na watu. Hakikidhi matakwa ,mahitaji na matarajio, si tu ya wanachama wake, bali ya umma. Afrika chama cha siasa hutekwa kirahisi na wachache.

Je, Mobutu huyu ni nani? Joseph Desire Mobutu. Baadae akaja kujiita, Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga. Inasemwa, kuwa Sese Seko ina maana ya milele, na Nkuku Ngbendu wa Za Banga ina maana ya mtu anayepita na kuacha nyuma yake alama za moto . Naam. Ni Mobutu wa milele na anayeacha alama za moto nyuma yake!

Joseph Mobutu alizaliwa mwaka 1930 na alifia uhamishoni, Rabat, Morocco, mwaka 1997. Kwa matendo yake alipokuwa madarakani, Mobutu aliishia kuzikwa kama njiti ya kibiriti katika makaburi ya ughaibuni. Mazishi yake yaliudhuriwa na watu wachache sana. Hayakufanana na ufahari aliojijengea alipokuwa hai na mwenye madaraka.

Kule Kongo Mobutu alishasikia kilio cha Wakongo cha kutaka mabadiliko, akapuuzia. Wakongo katika mitaa ya Kinshasa, Lubumbashi, Kisangani na kwingineko walianza kunong’ona, kuwa MPR, inakaribia kufa. MPR- Popular Movement Of The Revolution- kilikuwa ni Chama kilichoanzishwa na Mobutu na wenzake mwaka 1967. Hatimaye Wakongo wakaacha kunong’ona, wakawa wakiongea kwa sauti mitaani, sokoni na kwenye vilabu vya pombe, kuwa, “MPR inakufa!”

Katika hali ya kujinusuru, Mobutu akawanunua hata wasanii ili wamuimbe yeye na Chama chake. Hiyo hapo juu ni moja ya nyimbo za kumtukuza Mobutu na Chama chake. Tafsiri yake; ” Baba Mobutu, utakaa udumu, wanasema sana , kuwa MPR itakufa, haiwezekani! Naam. Leo tunaona, kuwa Mobutu hakukaa akadumu, MPR imekufa, imewezekana! Na ndivyo wahenga wetu wanavyotwambia; ” Kila lenye mwanzo lina mwisho”. Na hilo ni Neno La Leo.

( Hii ni sehemu ya makala yangu, Raia Mwema, leo Jumatano)

Maggid
Iringa
Jumatano, Aprili 20, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
0788 111 765
 
Nauona ujumbe huu ni kama 'barua ya Mapenzi' kwa Wanaojivua Magamba kama wanaamini kwamba anayekuambia ukweli na kukuonyesha ulipoanguka/unapokosea anakutakia Mema. Nimeangalia kwenye ITV kilichokua kinaendelea Dodoma wakati NEC ya CCM ilipokua 'inajivua Magamba' waliimba ule wimbo unao hamasisha kujiamini katika mapambano unaosema... " Nani ajuaye....ni Mwenye? Aje Simba mtu..." Ni yale yale ya Mabotu kama asemavyo mtoa 'neno la Leo'.
 
Ndugu Zangu,

WAKONGO wa Kinshasa na kwengineko wanaujua wimbo huu; "Papaa Mobutu ee, lokuta monene, oy'akanisaka, MPR ekokufaha, wayahaa, Tata Marechal, tikala libela, tata Mobutuee, tikala libela, ...!"

Makala yangu ya juma lililopita imepekelea baadhi ya wasomaji wangu, na hususan vijana, kutaka kufahamu zaidi habari za Joseph Mobutu. Kuna aliyeniandikia akisema; kwa anavyoiangalia jamii yetu hii, kuna anaoyojifunza kutoka kwa yaliyomkuta Mobutu.

Mobutu ni kielelezo kizuri cha hulka za watala wengi wa bara letu.
Na Afrika utazionaje dalili za Chama cha siasa kinachokufa? Jibu; ni pale 'Kiongozi Mkuu' anapoanza kujitenga na umma, kwa kauli na matendo. Kuna wenzake wachache pia ndani ya Chama watakaokuwa na hulka hiyo. Chama cha siasa huonekana kuwa mbali na watu. Hakikidhi matakwa ,mahitaji na matarajio, si tu ya wanachama wake, bali ya umma. Afrika chama cha siasa hutekwa kirahisi na wachache.

Je, Mobutu huyu ni nani? Joseph Desire Mobutu. Baadae akaja kujiita, Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga. Inasemwa, kuwa Sese Seko ina maana ya milele, na Nkuku Ngbendu wa Za Banga ina maana ya mtu anayepita na kuacha nyuma yake alama za moto . Naam. Ni Mobutu wa milele na anayeacha alama za moto nyuma yake!

Joseph Mobutu alizaliwa mwaka 1930 na alifia uhamishoni, Rabat, Morocco, mwaka 1997. Kwa matendo yake alipokuwa madarakani, Mobutu aliishia kuzikwa kama njiti ya kibiriti katika makaburi ya ughaibuni. Mazishi yake yaliudhuriwa na watu wachache sana. Hayakufanana na ufahari aliojijengea alipokuwa hai na mwenye madaraka.

Kule Kongo Mobutu alishasikia kilio cha Wakongo cha kutaka mabadiliko, akapuuzia. Wakongo katika mitaa ya Kinshasa, Lubumbashi, Kisangani na kwingineko walianza kunong'ona, kuwa MPR, inakaribia kufa. MPR- Popular Movement Of The Revolution- kilikuwa ni Chama kilichoanzishwa na Mobutu na wenzake mwaka 1967. Hatimaye Wakongo wakaacha kunong'ona, wakawa wakiongea kwa sauti mitaani, sokoni na kwenye vilabu vya pombe, kuwa, "MPR inakufa!"

Katika hali ya kujinusuru, Mobutu akawanunua hata wasanii ili wamuimbe yeye na Chama chake. Hiyo hapo juu ni moja ya nyimbo za kumtukuza Mobutu na Chama chake. Tafsiri yake; " Baba Mobutu, utakaa udumu, wanasema sana , kuwa MPR itakufa, haiwezekani! Naam. Leo tunaona, kuwa Mobutu hakukaa akadumu, MPR imekufa, imewezekana! Na ndivyo wahenga wetu wanavyotwambia; " Kila lenye mwanzo lina mwisho". Na hilo ni Neno La Leo.

( Hii ni sehemu ya makala yangu, Raia Mwema, leo Jumatano)

Maggid
Iringa
Jumatano, Aprili 20, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
0788 111 765
Hii imenikumbusha Chama cha Magamba jinsi kinavyokuwa kinapigiwa debe na wanamuziki
 
Back
Top Bottom