Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Wakati ambapo Watanzania wakijiandaa na Ufunguzi wa IT & Communication Summit , Nchini Kenya wiki hii Kumefunguliwa kituo cha TEKNOHAMA ambapo wadau mbalimbali wa Fani hiyo wanaweza kwenda kutumia vifaa vya vituo hivyo kwa ajili ya kazi zao mbalimbali haswa kwa wanafunzi ambao wanahitaji kufunza zaidi na wale wanaopenda kujiajiri wenyewe mradi huu uko chini ya Ushahidi.com Hii ni hatua nzuri sana kwa Kenya na afrika mashariki kwa ujumla .
Pia Kampuni kadhaa za mawasiliano ya mtandao yameahidi kusaidia katika kuhakikisha kituo hicho kinapata huduma ya mawasiliano bure kwa siku zao zote za kazi .
Uganda napo serikali ya nchi hiyo itaanza kuwapa ardhi bure wadau wa TEKNOHAMA lakini hii itafanyika kwa wale wenye miradi inayoeleweka ya kibiashara ambayo inaweza kusaidia jamii za sehemu ambapo mdau husika yupo haswa vijijini na sehemu zingine ambapo teknologia hii iko nyuma kidogo hii itakuwa changamoto sana kwa wadau mbalimbali wan chi hiyo kuja na mawazo miradi na mambo mengine kwa faida ya jamii zao .
Mambo hayo yakiwa yanaendelea kwenye nchi za wenzetu tena jirani zetu kuna mambo ambayo sisi kama watanzania yatupasa kujiuliza mipango yetu ya TEKNOHAMA mpaka sasa hivi inaendeleaje je yale ambayo yalipendekezwa miaka 5 iliyopita yamefikia malengo au kutekelezwa hata kidogo tu tunaweza kuona nyota njema ikingaa mbele zetu ?
Kwa kuanzia tunaweza kuangalia upya kama TCRA Taasisi inayohusika na mawasiliano nchini kwa ujumla kama imeweza kufikia malengo yake iliyojiwekea na kama bado inafaida kwetu kama taifa au kuwe na taasisi nyingine mama iliyohuru katika utendaji wake wa kazi mbalimbali zinazohusu mawasiliano , kwa kweli Hii Taasisi ni ya kuangalia kwa macho makali , lazima ifanyiwe mabadiliko ili iwe ya kisasa iweze kuendana na wakati wa sasa kwenye Sekta ya Mawasiliano Kuna hitajika platform Mpya ya kuendesha mfumo mzima wa mawasiliano Nchini
Imeonekana Umeme kuwa Tatizo sugu sana katika utendaji wa Masuala mengi ya TEKNOHAMA , hapa ninapoandika hii barua fupi niko Katikati ya Jiji zaidi ya Nusu ya Jiji lote la DSM halina umeme kwa masaa 4 sasa na hali hii imekwepo toka mwaka jana hii ina maana shuguli nyingi za teknohama haziwezi kuendelea kama ilivyo labda kwa wale wenye uwezo wa kuwa na vifaa vya kuzalishia umeme lakini hii inaweza pia ngumu kwa wale wasiokuwa na uwezo .
Kitu cha mwisho ni kwa wadau mbalimbali kufikria sasa kuwa na Contents zinazohusu mambo yetu kwenye wavuti zao suala hili limeonekana kuwa gumu kwa wengi wetu lakini naamini siku zijazo kunaweza kuwa na mabadiliko makubwa tukiamua kuwa na contents zetu .
Na ushirikiano kati ya watu wa TEKNOHAMA Umekuwa hafifu sana wengi hawaaminiani - Hili siwezi kuliongelea kwa mapana lakini nawaomba wana TEKNOHAMA tuzidishe ushirikiano wa kazi za kila siku ili tusogeze taifa hili Mbele ,Lakini kutokuwepo Taasisi ya kutambua wataalamu mbalimbali kwenye TEKNOHAMA imechangia sana suala hili .