Neno Fupi La Usiku Huu; Upepo!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Neno upepo limesikika sana katika siku mbili tatu hizi. Duniani hakuna upepo mbaya. Ukimwona mwanadamu anarudishwa nyuma na hata kuangushwa na upepo, basi, ujue amekinzana nao.


Kuna upepo unavuma, ni dunia nzima. Kuna wanaojaribu kukinzana nao. Watashindwa. Maana, upepo una sifa moja kubwa; kujikusanya. Na upepo ukijikusanya ukawa mwingi, basi, hugeuka kimbunga. Na kimbunga kingine ni cha zilizilahi, kinasomba kila kinachokutana nacho.


Wanadamu tujifunze kutoka kwa ndege. Siku zote, ndege haruki na kuianza safari ndefu kabla hajaupima upepo. Na upepo una mkia. Ndege huruka kwa kuufuata mkia wa upepo, hivyo basi, anaendana na upepo. Na mwelekeo wa upepo ukibadilika njiani, basi, ndege anaweza kukatisha safari yake. Atapiga kambi hata juma zima mahali pasipo kwake. Atasubiri hadi pale mwelekeo wa upepo utakapobadilika tena. Ataendelea na safari yake.

Tuna safari tumeianza. Wengi wameshajiandaa na safari. Kuna ambao hawako tayari. Muda wa kuianza safari umekaribia sana. Inavyoonekana sasa, tutaondoka na kuwaacha. Itasikitisha sana, maana, nao ni wenzetu.


Wanadamu tunakumbushwa sana umuhimu wa kusoma alama za nyakati. Lakini, lililo muhimu pia, ni kusoma ishara za mabadiliko ya mwelekeo wa upepo.


Ndio, mawimbi ya bahari yameanza kujikusanya. Kuna pepo zinavuma zikija upande wetu. Zinakuja na kimbunga kikali.

Je, ni lini tutarajie kimbunga hicho kutufikia?
Jibu: Mtaziona ishara…
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku huu. Alamsiki.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
"Ni upepo tu, utatulia".

Washauri wasome alama za nyakati, ingawa bado wanajipa matumaini kwamba watanzania bado ni bendera fuata upepo!

Pamoja na hayo, kusoma alama za nyakati kunahitaji hekima uelewa na unyenyekevu. Watu wenye mamlaka huwa si wepesi wa kusoma alama za nyakati kwa kuwa huamini kwamba wanaweza kutumia mamlaka yao kulazimisha nyakati ziwe ndivyo sivyo!

Kila la heri CCM, wabunge wake na serikali yake.
 
thanks bro, - nasoma maon yako mengi hata katika magazine unazo andika- why cant u be an activist? i hope u will save us moree
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom