Neno fasaha ni lipi kati ya hairisha na ahirisha?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Nimekuwa naona vyombo vya habari hasa Magazeti wakitumia neno "Hairisha" likimaanisha (kwa kiingereza) postpone. Wataalam wa Kiswahili naomba mnisaidie neno fasaha ni Hairisha au Ahirisha?

Utakuta Gazeti limeandikwa (kwa mfano) " mkutano umehairishwa". kwa jinsi ninavyo fahamu, ingekuwa " Mkutano Umeahirishwa".

Msaada tafadhali.
 
Sina uhakika wa kutosha lakini nadhani neno sahihi ni "ahirisha" kama kuna wadadavuzi wa lugha nadhani watatuweka sawa maana naona kama bado tunaongea kwa kuhisia tuu.
 
Neno fasaha ni "Ahirisha" na si "Hairisha". Kuna watu wengi tu hata humu JF wana shida na matumizi ya "h". Pale ambapo inapaswa kuwepo wanaitoa, na pale ambapo haipaswi kuwepo wanaiweka. Ndipo unapokutana na madudu haya ya "hairisha".
 
Hii inatokana na lafudhi ya watu wakutoka mikoa fulani huweka h endapo a ni ya kwanza na wengine huifuta h k.m hamna huwa amna.

Sahihi ni ahirisha. Kinachokera unakuta huandikwa hivyo kwenye magazeti kama vile hakuna proof reader, labda tu awe na tatizo hilo. Tuenzi lugha yetu kwa kuandika kwa usanifu
 
Hii inatokana na lafudhi ya watu wakutoka mikoa fulani huweka h endapo a ni ya kwanza na wengine huifuta h k.m hamna huwa amna.
sahihi ni ahirisha. Kinachokera unakuta huandikwa hivyo kwenye magazeti kama vile hakuna proof reader, labda tu awe na tatizo hilo. Tuenzi lugha yetu kwa kuandika kwa usanifu

Hata neno budi. kianzio chake sahihi ni sina budi lakini wengi wetu hutamka nina budi.
 
Jibaba:
Katika muktadha huu, hebu angalia makala ya Bwana Stephen Maina ambaye ni mpekuaji wa hali ya juu wa makosa, mategu na madudu ya Kiswahili! Maoni yake yanapatikana kwa kawaida kwenye gazeti la Mwananchi Tanzania.

Mimi naendelea kupata elimu ya kuridhishsa sana nikisoma taarifa zake kuhusu namna watu mbalimbali wanavyotumia Kiswahili vibaya au kiuzembe.

Anakaribisha mawasiliano. Yuko simuni: 716694240
 
Marijani: Tafadhali nielezee jinsi ulivyoumba neno hili la "wadadavuzi". Linanipendeza lakini siwezi kulikubali bila ya maarifa mengine kuhusu hadhi yake ya neno jipya ... ? Asante.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom