Neno 'dear'

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,769
2,544
hili neno la kingereza lina utata katika matumizi. maana yake hasa ni nini? kwenye barua utakuta Drea sir/madam. tunaambiwa dear ni mpenzi, so tuseme mpenzi kwenye barua rasmi? maana yake hasa ni ipi? naombeni jibu
 
hili neno linatumika siku hizi na wanawake wa uswahilini kwenye kuchuna mabuzi..

ukiona mwanamke wa kiswahili anakuita dear ujue unachunwa....

take care.
 
hili neno la kingereza lina utata katika matumizi. Maana yake hasa ni nini? Kwenye barua utakuta drea sir/madam. Tunaambiwa dear ni mpenzi, so tuseme mpenzi kwenye barua rasmi? Maana yake hasa ni ipi? Naombeni jibu

mhh.
 
hili neno linatumika siku hizi na wanawake wa uswahilini kwenye kuchuna mabuzi..

ukiona mwanamke wa kiswahili anakuita dear ujue unachunwa....

take care.

Du ..Mkuu Boss hapa umeniacha hoi... yawezekana ushaumizwa kama sisi wengine eeh?
 
hili neno la kingereza lina utata katika matumizi. maana yake hasa ni nini? kwenye barua utakuta Drea sir/madam. tunaambiwa dear ni mpenzi, so tuseme mpenzi kwenye barua rasmi? maana yake hasa ni ipi? naombeni jibu

Dear Mziwanda! Nafikiri ni neno la msisitizo linaloumba mahusiano mazuri si lazima iwe mapenzi
 
hili neno linatumika siku hizi na wanawake wa uswahilini kwenye kuchuna mabuzi..

ukiona mwanamke wa kiswahili anakuita dear ujue unachunwa....

take care.

hahaaa...wa kizungu je?
 
mshakaji kuna baadhi ya maneno huwezi kupata maana halisi hususan unapo litafsiri toka lugha moja kwenda nyingine, Dear ni neno la heshima na si la mapenzi thats why hata kwenye barua muhimu kama za kikazi una andika Dear sir/madam.
 
basi tukubali kuwa kibongobongo tunalitumia vibaya
 
ni kama kiambishi awali kinachojenga nia njema kwamfano kama ninataka kukueleza jambo ninapoanza na neno dear ni ishara kuwa maneno yanayufuata ni maneno mema yasiyo na uadui au ufitini,,..kinyume chake ni enemy (adui) . kwahiyo ninapoandika barua kwa kuanza na dear , manake utarajie yaliyomo ktk hiyo barua yote ambayo si ufitini, uadui au ugonvi . hiyo ndiyo maana halisi, kila unayemtakia mema na unaona ni mwema kwako ni sawa tu ukimwita dear - habari ndo hiyo
 
dear kiswahili sahih ni mpendwa, short and clea, mpendwa can be any body, dad, mum, sis, bro, mention whoever
 
Dear Mziwanda! Nafikiri ni neno la msisitizo linaloumba mahusiano mazuri si lazima iwe mapenzi

Ndivyo ilivyo mkuu, lakini waswahili walishaharibu kabisa hili neno!! Msichana wa kiswahili akikuita dear, basi jiandae!!!
 
Neno Dear halina maana ya mpenzi tu, dear kwa kiswahili ni mpendwa ila waswahili tumeshajiwekea kuwa ni mpenzi. Unaweza kumwita mtu yeyote unaempenda Dear.
 
Matumizi ya maneno mengi kwa sasa yameharibiwa kwa makusudi au kwa kutokujua, Hili neno ni mojawapo wa maneno mengi, kimsingi unaweza kumuita mtu yeyote yule Dear, hata Mungu. Kama wengine walivyosema hapo juu ukimwita msichana au mwanamke yeyote yule dear wazo lake la kwanza ni mahusiano ya kimapenzi, hata wavulana/wanaume nao pia. Hasa wale waliokuwa marafiki (Normal friendship) wa opposite sex mmoja akimwita hivyo mwenzake utasikiwa wa upande wa pili akisema kumbe fulani ananitaka mie sikujua leo kaaniita dear, n.k. Ukitaka kuona ngumi za mwaka marafiki wa kiume mmoja wao amwite mwenzake dear uone. Na katika jamii zetu za kiafrika mtoto wa kiume amwite hivyo dada au hata mama yake au wa kike amwite hivyo kaka au baba yake utasikia watu wanasema fulani simwelewielewi na fulani siku hizi n.k.

Ndio maana nimejaribu kutafuta haya matumizi machache ya neno hilo:
A. Adjective: dear (dearer, dearest)
1.Dearly loved
2. With or in a close or intimate relationship
e.g "my sisters and brothers are near and dear"
3.Earnest
e.g "one's dearest wish"
4.Having a high price
e.g "much too dear for my pocketbook"
B. Noun: dear
1.A beloved person; used as terms of endearment
2.A sweet innocent mild-mannered person (especially a child)
C. Adverb: dear
1. With affection
2. At a great cost
e.g "this cost him dear"
D. Interjection: dear
1. Used to express shock, dismay, disappointment, sympathy, etc.

Kwa mifano hiyo hapo juu unaweza kuamua kulitumia neno hilo kwa usahihi au kuendeleza maana potofu juu ya neno hilo.

Heshima mbele wazee.
 
hili neno la kingereza lina utata katika matumizi. maana yake hasa ni nini? kwenye barua utakuta Drea sir/madam. tunaambiwa dear ni mpenzi, so tuseme mpenzi kwenye barua rasmi? maana yake hasa ni ipi? naombeni jibu
Kwenye barua hutumika kama mpendwa na si mpenzi!!
 
hili neno la kingereza lina utata katika matumizi. maana yake hasa ni nini? kwenye barua utakuta Drea sir/madam. tunaambiwa dear ni mpenzi, so tuseme mpenzi kwenye barua rasmi? maana yake hasa ni ipi? naombeni jibu

Umesema vema. Neno la kiingereza 'dear' lina 'utata' (i.e. lina maana zaidi ya moja!). Kwenye kiingereza neno 'dear' linaweza kutumika kama kivumishi (adjective), interjection, jina(noun) au adverb (kielezo).

Kama alivyodadavua Creative Thinker hapo juu, neno 'dear':

Likitumika kama kivumishi (adjective), linaweza kuwa na maana zifuatazo:

  • ‘mbaya' (i.e. severe, sore – mfano: ".. in our dear peril")
  • ‘enye thamani' (highly valued – Mfano "dear friend") – kwenye barua za kiofisi nadhani linabeba maana hii.
  • ‘enye kupendwa' (affectionate, fond)
  • ‘aghali' (expensive – mfano: mangoes are very dear just now)
Pia linatumika kama kielezo (‘adverb') kumaanisha ‘sana' au ‘kiasi kikubwa' (mfano: "The effort would cost them dear").

Linatumika kama jina (noun), linaweza kuwa na maana ya: Mwenye kupendwa/mpenzi (a loved one – sweetheart!) au Mtu anaependeka (a lovable person).

Pia, neno dear linatumika kuonesha kukerwa, kushangazwa nk (interjections or exclamations) – mfano: "Oh, dear! Does it hurt?", "Dear me! That's a surprise!"
 
Umesema vema. Neno la kiingereza 'dear' lina 'utata' (i.e. lina maana zaidi ya moja!). Kwenye kiingereza neno 'dear' linaweza kutumika kama kivumishi (adjective), interjection, jina(noun) au adverb (kielezo).

Kama alivyodadavua Creative Thinker hapo juu, neno 'dear':

Likitumika kama kivumishi (adjective), linaweza kuwa na maana zifuatazo:

  • ‘mbaya’ (i.e. severe, sore – mfano: “.. in our dear peril”)
  • ‘enye thamani’ (highly valued – Mfano “dear friend”) – kwenye barua za kiofisi nadhani linabeba maana hii.
  • ‘enye kupendwa’ (affectionate, fond)
  • ‘aghali’ (expensive – mfano: mangoes are very dear just now)
Pia linatumika kama kielezo (‘adverb’) kumaanisha ‘sana’ au ‘kiasi kikubwa’ (mfano: “The effort would cost them dear”).

Linatumika kama jina (noun), linaweza kuwa na maana ya: Mwenye kupendwa/mpenzi (a loved one – sweetheart!) au Mtu anaependeka (a lovable person).

Pia, neno dear linatumika kuonesha kukerwa, kushangazwa nk (interjections or exclamations) – mfano: “Oh, dear! Does it hurt?”, “Dear me! That’s a surprise!”

Ndugu ninakushukru kwa kurahisisha maelezo ya neno dear, nilikosa muda wa kuyarahisisha hasa kwa lugha inayoeleweka kama hiyo hapo juu, Thanks. Mpaka hapo najua watu wataelewa zaidi na zaidi lini, wapi, wakati gani na kwa nani kulitumia neno hilo ili kuondoa utata usiokuwa na lazima.

Heshima yako mkuu.
 
nafikiri maana yake ni mpenzi / mpendwa kumbuka rafiki yako wa kiume anaweza kuwa mpenzi wako! yaani ni mtu umpendae. Mfano bibilia inaposema wapenzi pendaneni haimaanishi mtu mke na mume ila humaanisha watu wote
 
Matumizi ya maneno mengi kwa sasa yameharibiwa kwa makusudi au kwa kutokujua, Hili neno ni mojawapo wa maneno mengi, kimsingi unaweza kumuita mtu yeyote yule Dear, hata Mungu. Kama wengine walivyosema hapo juu ukimwita msichana au mwanamke yeyote yule dear wazo lake la kwanza ni mahusiano ya kimapenzi, hata wavulana/wanaume nao pia. Hasa wale waliokuwa marafiki (Normal friendship) wa opposite sex mmoja akimwita hivyo mwenzake utasikiwa wa upande wa pili akisema kumbe fulani ananitaka mie sikujua leo kaaniita dear, n.k. Ukitaka kuona ngumi za mwaka marafiki wa kiume mmoja wao amwite mwenzake dear uone. Na katika jamii zetu za kiafrika mtoto wa kiume amwite hivyo dada au hata mama yake au wa kike amwite hivyo kaka au baba yake utasikia watu wanasema fulani simwelewielewi na fulani siku hizi n.k.

Ndio maana nimejaribu kutafuta haya matumizi machache ya neno hilo:
A. Adjective: dear (dearer, dearest)
1.Dearly loved
2. With or in a close or intimate relationship
e.g "my sisters and brothers are near and dear"
3.Earnest
e.g "one's dearest wish"
4.Having a high price
e.g "much too dear for my pocketbook"
B. Noun: dear
1.A beloved person; used as terms of endearment
2.A sweet innocent mild-mannered person (especially a child)
C. Adverb: dear
1. With affection
2. At a great cost
e.g "this cost him dear"
D. Interjection: dear
1. Used to express shock, dismay, disappointment, sympathy, etc.

Kwa mifano hiyo hapo juu unaweza kuamua kulitumia neno hilo kwa usahihi au kuendeleza maana potofu juu ya neno hilo.

Heshima mbele wazee.

thank u dear!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom