Neno "Bongo", Nini maana yake na asili yake?

​Hivi bongo kuna wanaume kweli???maana nchi inaburuzwa na watu wako kimya kama vile kila kitu kiko sawa....
 
Ina depend upo wapi .ukiwa Tanzania nje ya Dar na unasema naenda bongo maana ni Dar .ila ukiwa nje ya Tz ukisema naenda bongo maanayake ni Tz
 
Ni kweli MTU aliyekuwa akitoka mkoani kwenda Dar alikuwa akisema anaenda bongo. Kwa hiyo bongo ni dar kwa enzi hizo! Kwa sasa nchi nzima inaitwa bongo kwa kuwa % kubwa ya watu wanaendesha maisha kiujanja-ujanja.

Hii nchi kwa sasa bila bongo utaona rangi zote!
 
Jamani wana jf naomba mnieleweshe kuhusu hili jina la BONGO nimekuwa nalisikia siku nyingi sasa na pegine kuunganishwa na maneno mengine kama BONGO FLAVOR , kwetu BONGO , KI-BONGOBONGO Nakadhalika -- natanguliza shukran
Bongo mjomba maana yake ni ujanjaujanja tu watu wanatumia ubongo tu kuishi hayo mengine sijui bongo Flavour na mengineyo ni vionjo tU
 
Hivyo ujanjaujanja uwongo uwongo na utapeli ndiyo bongo aaahaa nimeelewa sasa
majina huumba wenyewe wanasema. Masuala ya muda bongo siyo mambo yanayozingatiwa sana ukiambiwa saa 2 ujue ni saa 4
angalia hata id za watu hapa zimekaa kibongobongo mfn mzushi Mauza uza
 
Last edited by a moderator:
Bongo dar es salaam akili kumkichwa ukizubaa umeachwa ohoo ilo neno lina maana kubwa sana yn ukiitwa we mbongo ww mtu hatari wakalamwazi tunawaita mbuli ku mlomo
 
HILI NENO AMETUACHIA ALIYEKUWA RAISI WA GABON, OMARI BONGO. ALIPOZURU TANZANIA KWA ZIARA YA KISERKALI. ALIKAA CK NYINGI KIASI HAPA JIJINI DSM. KUTOKANA NA KULIPENDA JIJI LETU, AKASEMA DAR ES SALAAM NI JIJI LANGU, YAANI JIJI LA BONGO. IKAWA NI KAMA UTANI MAGAZETI YAKAANDIKA DSM NI JIJI LA BONGO. YAANI DSM NI JIJI LA RAIS WA GABON, OMARI BONGO. HIYO NI MWANZONI MWA MIAKA YA 90.
 
Back
Top Bottom