Neno "Bongo", Nini maana yake na asili yake?

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,314
2,635
Kwakweli kiswahili kinazidi kupaa.

Zamani mtu alikuwa akisafiri kwenda Dar alitumia msemo naenda BONGO. Hivi sasa hata mtu anaeishi nje ya Dar anasema yeye mbongo pengine anamaanisha yeye M-TZ.

Maswali yangu;

Je, bongo maana yake ni Dar au Tanzania?

Inahusiana nini Dar au Tanzania?

Pia nitafurahi kama mtanijuza hili jina lilianza kufahamika lini na nani mwanzilishi.

Jamani wanaJF,

Naomba mnieleweshe kuhusu hili jina la BONGO. Nimekuwa nalisikia siku nyingi sasa na pengine kuunganishwa na maneno mengine kama BONGO FLAVOR , kwetu BONGO , KI-BONGOBONGO Na kadhalika.

Natanguliza shukrani
 
kaka hiii nimisimu mfano neno bongo maana yake akili kwa hiyo watu waliona kuwa wakazi wa dar wana uelevu wa mambo mengi hivyo wakaamua kupaita bongo

Hapana.Ilitokana na ukweli kwamba hapo awali na pengine sasa kuishi Dar ilikuwa utumie akili fulani ya ujanja,kichwa vinginevyo ungeshindwa.
 
Bongo ofice ya mtu ipo mfukoni hata visa ya USA unaipata chini ya mti.Hakuna kinachoshindikana.
BONGO=USWAHILI.
 
Bongo Dar es Salaam ndo mpango mzima.
Wa ughaibuni wanatuharibia maana. Waache mara moja kabla sijawapiga ban.
 
Kwa kawaida ukiwa ndani ya Tz bongo inamaanisha Dar, ila kutokana na kuwa ki historia wengi waishio nje ya Dar wakiwa nje ya Tz bado wanashukia Dar halafu ndo waende huko mikoani ndo hapo mgongano wa lugha ukatokea na ikiwa mtu akiwa nje ya Tz anakuwa Mbongo kwani akiwa anarudi Tz anarudi Dar kwanza halafu ndo aende aendako, pia imetokana na idadi kubwa ya waishio nje ya Tz (hususan Ulaya ma Amerika kuwa ni wa Tz wanaoishi Dar.

Kwa lugha nyingine ni kuwa ukiwa ndani ya Tanzania inabidi uishi Dar kuhitimu kuwa Mbongo, na ukiwa nje ya Tanzania unahitimu mojakwa moja kuwa mbongo, hadi urudi Tz na kama huishi Dar unakuwa si Mbongo tena!
 
Bongo ilitokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya watu dar walikuwa wajasiriamali hivyo bila akili za ziada mambo hayendi.mambo mengi hata nyeti yalipatikana kupitia ofisini za mfukoni.
 
zamani nlisikia dar wakipaita dizim(dsm) hili la bongo likaja kwa ugum wa maisha ndan ya jiji la Dar. Bongo=akili. Ili uweze kuishi huko bongo(Dar) maisha yalivyo lazima bongo(akili) itumike zaidi.
Mzizima=Bandari salama=Dar-es-salaam=Dar=Dsm=Dizim=Bongo.
 
lilitoholewa kutokana na neno ubongo ndipo lakapatikana neno Bongo. Maana yake ili uishi Dar lazima kutumia ubongo (akili) sana tofauti na mikoani. Baadaye maisha ya Watz wote hata wa mikoani yamekuwa magumu hivyo Tz kwa ujumla sasa hivi inaitwa Bongo. l
 
Jamani wana jf naomba mnieleweshe kuhusu hili jina la BONGO nimekuwa nalisikia siku nyingi sasa na pegine kuunganishwa na maneno mengine kama BONGO FLAVOR , kwetu BONGO , KI-BONGOBONGO Nakadhalika -- natanguliza shukran
 
Hili neno Bongo linatafsiriwa tofauti.Mfano ukiwaTanzania ukisema nipo Bongo maana yake uko DAR.

Mtu aliyeko Arusha au Mwanza mara nyingi hasemi niko Bongo ila watu ambao wako nje ya nchi mara nyingi mtu atasema narudi Bongo, maana yake narudi Tanzania.

So hilo neno lina maana tofauti inategemea uko sehemu gani ya hii Dunia.
 
lilitoholewa kutokana na neno ubongo ndipo lakapatikana neno Bongo. Maana yake ili uishi Dar lazima kutumia ubongo (akili) sana tofauti na mikoani. Baadaye maisha ya Watz wote hata wa mikoani yamekuwa magumu hivyo Tz kwa ujumla sasa hivi inaitwa Bongo. l

jaluo, nimenda ufafanuzi,
 
Bongo lina maana ya wakazi wanatumia akili nyingi sana kukabiliana na maisha ya jijini Dar(enzi zile) sasa neno hili linatumiaka karibu miji yote jinsi mambo yalivyokuwa magumu kimaisha
Tujikumbushe waziri mkuu mstaafu jina nimeisahau kwa wenye data plz tukumbushane- aliwai kulipinga ili neno Bongo kwa nguvu zote lisitamkwe jijini Dar
 
Ukiwa ndani ya tanzania bongo unamaanisha dsm,,, but ukiwa nje ya tanzania bongo unamaanisha tanzania nzima,,

Maana ukiwa unarudi nyumban tanzania imezoeleka kusemwa unashuka bongo...

Na ukweli bongo ni bongo kweli maana ndege ikianza kuzunguka bahari tu kuset direction for landing jk nyerere unaanza kuona mji ulivyojengwa kiujanja ujanja bila kufata ramani na unajua nimeingia Bongo maana ni ujanja ujanja kila kitu ramani haieleweki eleweki vurugu vurugu
 
Bongo=AKILI...kuishi DSM ilimlazimu/inamlazimu m2 kuishi kiujanjaujanja, ku2100 mbinu mbadala kuendesha maisha ya kila cku. "mission town" lakini baada ya hali ya maisha kuwa ngumu wa2 wote Tz mijini na vijijini, kuanzia mkulima, mfanyakazi na hata mfanyabiashara inambidi kuishi kiujanjaujanja, kutumia bongo kuendesha maisha...neno bongo lilianza kutumika miaka ya 1984. Wakati huo unapanda treni pale moshi saa 10 jioni nakufika bongo saa 4 asbh cku inayofuata!
 
Bongo=AKILI...kuishi DSM ilimlazimu/inamlazimu m2 kuishi kiujanjaujanja, ku2100 mbinu mbadala kuendesha maisha ya kila cku. "mission town" lakini baada ya hali ya maisha kuwa ngumu wa2 wote Tz mijini na vijijini, kuanzia mkulima, mfanyakazi na hata mfanyabiashara inambidi kuishi kiujanjaujanja, kutumia bongo kuendesha maisha...neno bongo lilianza kutumika miaka ya 1984. Wakati huo unapanda treni pale moshi saa 10 jioni nakufika bongo saa 4 asbh cku inayofuata!
Ni kabla ya hapo mkuu. Baada ya vita vya Kagera 1978/9 hali ya uchumi ilisambaratika na maisha kuelekea kuwa magumu. Wakati huo Nyerere alituahidi mambo yatanyooka ndani ya kipindi cha miezi 18 na tukatakiwa "tufunge mikanda". Hali ilizidi kuwa mbaya na mwanzoni wa 80´s msemo wa "jua kali" na "bongo" ndipo ulipoanza kushamiri. Yaani jamaa anakuuliza vipi mambo? na wewe unajibu mambo jua kali (yaani ni kusota). Bongo ilitokana na swala la kutumia ubongo ili kusavaiv mjini. Na hapo ndipo Dsm ilipogeuka kuwa bongo. Bongo jua kali. Baadaye na hadi sasa bongo inamaanisha TZ kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom