Nenda Sumaye, Usiogope! Chomoa mchanga wa chini katika kifusi cha mchanga!

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Kwa malumbano yalivyokuwa kati ya Sumaye na viongozi wa CCM ni wazi kuwa game inasogea karibu kabisa na mahali pa ama sumaye ama CCM mmoja anahitaji ondoka mpisha mwingine. Na tayari Sumaye anaweza ingia katika akumbukumbu vyema kama atatangaza hadharani kuwa anajitoa CCM rasmi na kujiunga na wapiganaji akina Mbowe na asigombee uongozi wowote.

CCM watapiga kelele sana kuwa nataka madaraka il haitosaidia kwani hatogombea uongozi wa juu wowote zaidi ya kuwa mzee wa chama.

Kwa muonekano wa haraka CCM hawatakuwa na busara za kujibu vyema maswali yatakayoibuka mara sumaye atakavyoondoka.Hii itawapa ujasiri sana wana CCM wengi wasioridhika na hali, na baadaye patakuwa na avalanche ya defectors. Mwisho who knows CCM inaweza kufa overnight bila damu kama tulivyopata uhuru wa kwanza. Pengine damu pekee itakuwa ya walio uwawa na polisi.

Mh. Sumaye nasema nenda, tangaza nia ya kuachana na Siasa uchwara kama alivyosema Rostam. Ila tofauti ikiwa wewe haupo ktk List ya aibu, na wewe si tuu unaachana na siasa uchwara bali chama uchwara chenye siasa za Hovyo. Utakuwa umelitendea mema na haki taifa hili, na utakumbukwa kwa hilo. Usigeuke nyuma utakuwa jiwe la chumvi na kujiweka ktk hatari ya kutokuwa salama. Kwa sasa ni salama kuwa CHADEMA kwani tayari kila mtu anawaangalia kwa makini wasiku-Mwangosi au Mwakyembe.

Mhe. Sumaye lianzishe tuone CCM nyumba ya mchanga inavyoporomoka kama mchanga ndani ya edifice. Na hapataihitajika tena mtu wa kuishambulia bali itaendelea momonyoka hadi kuisha kwa ulichoanzisha. Hii ndio zawadi yenye fahari kuliko huo urais, na hata kama CHADEMA watapenda kukusimamisha baada ya miaka kadhaa bado utakuwa na heshima kubwa katika historia ya nchi hii. Make it big, with big publicity na ikibidi hata with a big party. Then kapumzike baada ya jibu moja kwa Nape. Utakuwa umefunga mikia kwa utambi na kuwapiga moto huku wakiwa katika shamba la ufisadi, udini, ukanda, undugu, urafiki na ukabila.

Sumaye ukirudi nyuma kama Sitta hutakuwa na amani tena, utaogopa kivuli chako, utaogopa majani yakikugusa, utaogopa kila kitu kihusucho usalama wako. Ni bora kuondoka kwa mbwembwe kubwa instantly halafu uwape majibu ukiwa sehemu salama huku ukipata juice na heshima.
 
CCm ni chama cha hovyo sana na hatari sana kwa dunia ya leo yenye fikra huru.

Sumaye hawezi kuwa salama huko na sidhani kama ahahitaji tena hela sasa zaidi ya heshima. Anaweza pata heshima kwa power au kwa kutenda jema. Power haina gurantee sana ya kukupa heshima. Mfano mmoja ni rais aliyepo, ana madaraka ila hana kuheshimika.
 
Kamwe Sumaye hawezi kuondoka CCM viongozi wengi waandamizi walio madarakani na wastaafu wanang'ang'ania kubaki CCM sio kwa sababu wanaipenda sana hapana ni kwa kuwa wanajua wakiondoka maslahi yao yatakuwa hatarini na pia maovu waliyoyatenda wakiwa madarakani yatawekwa wazi!

Mfano mzuri Nimrod Mkono alichimba mkwara kuwa jina lake lilikikatwa patachimbika, Limekatwa na kaambiwa kama anataka kuondoka njia nyeupe, ameondoka? Si amegeuka na kusema anakubali matokeo na hakuwahi kutishia chama?

Wengi wa viongozi ni sawa na Mkono, hata huyu Sitta anayepiga makelele ni kutisha tu hana lolote!
 
Hivi mkuu unaota? Ama? Sumaye aondoke halafu aache mizigo yake ccm? Kumbuka anachukua pensheni na marupurupu mengine ingawa ni ya serikali, lakini mmh. Sidhanii......
 
Hivi mtu anakichukia chama baada ya kukosa nafasi au vipi mimi sielewi kabisa siasa za kinafki za kibongo
 
Chadema sio chama cha kila makapi, kama anataka kujitoa CCM ajitoe aendelee na shuhuli zake za kilimo.
 
Sumaye hata afanye mazungumzo na Chadema, yeye sio mtaji lolote, sio mtaji chochote, na akihama CCM, atajihamia yeye kama yeye, hana wafuasi wowote wa kutishia usalama wa CCM!. Angetishia kuhama yule Mzee wa ....ndio CCM ingetingishika!.

Hata hivyo, sifa za kugombea urais kupitia CCM sio ujumbe wa NEC bali ni kwa mwana CCM yoyote mwenye sifa!, hivyo hata kama Sumaye amebwagwa ujumbe wa NEC na ki..da wake, kisa ki..da huyo pia katembea na Muzeiye, hiyo sio sababu ya yeye kuihama CCM!.

Kwa vile Sumaye hata kitu chochote cha maana zaidi tule tujumba alitotujenga kwa mikopo ya kifisadi ya NSSF, then hana jeuri yoyote ya kuihama CCM wakati tegemeo lake ni mafao ya kustaafu ambayo ni 80% ya current PM!. Japo hata akihama pensheni yake iko pale pale, bali masimango yatammaliza bure!.

Nawaomba niwape siri nzito nyie mnaodhani mnajua kumbe hamjui kitu!. Kwa Chadema, mtaji sio Sumaye, bali mtaji ni .......ndiye anayesubiriwa in case CCM hawamsimamisha!.

Take note, hivi mmeshawahi kuwasikia viongozi wa Chadema wakimlaumu jamaa fulani wa CCM?!.

Habari ndio hiyo!, nawaombeni msiniulize ni nani?!, wenye kuelewa wameelewa, nyie wengine, wenzangu na mimi tusioelewa, nawaombeni sana tusameheane tuu!.

P.
 
mkuu Pasco umenena vema, sumaye hana impact yoyote si cdm au ccm,ishu hapa ni mzee mamvi ndo habari ya mujini an effect kubwa sana akitoka magamban wanamagamba wahesabu chama chao is no more
 
Last edited by a moderator:
Kamwe Sumaye hawezi kuondoka CCM viongozi wengi waandamizi walio madarakani na wastaafu wanang'ang'ania kubaki CCM sio kwa sababu wanaipenda sana hapana ni kwa kuwa wanajua wakiondoka maslahi yao yatakuwa hatarini na pia maovu waliyoyatenda wakiwa madarakani yatawekwa wazi!

Mfano mzuri Nimrod Mkono alichimba mkwara kuwa jina lake lilikikatwa patachimbika, Limekatwa na kaambiwa kama anataka kuondoka njia nyeupe, ameondoka? Si amegeuka na kusema anakubali matokeo na hakuwahi kutishia chama?

Wengi wa viongozi ni sawa na Mkono, hata huyu Sitta anayepiga makelele ni kutisha tu hana lolote!
Mkuu Osokoni, nakuunga mkono, kuna mada fulani Mzee Mwanakijiji aliwahi kuuliza https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38155-wapiganaji-walioko-ccm-wanapigania-nini-hasa.html mimi katika mchango wangu, nilisema wanapigania matumbo yao!.
Swali ni jee ndani ya CCM, wanapigania nini?. Jibu langu la jumla ni kuwa wanapigania nafsi zao just for survival

Wapiganaji wa kweli ni wale ambao wako tayari to take risk kwa kusimama mbali na uvundo kuwathibitishia watanzania kuwa huku tuliko chama kimetekwa na mafisadi.

Wale kina Sumaye type, wanaopigania nafsi zao, mtawatambua kwa kutokubali kuriski nafasi zao ndani ya CCM ambako mafisadi wana upper hand. Kwa vile CCM ina wenyewe, na baadhi ya wenyewe hao ndio hao hao mafisadi na wengine wao ndio hao kina Sumaye, hapa ni mwendo wa mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama, maadamu wenye nguvu ni mafisadi, mwenye nguvu mpishe, hao kina Sumaye type watajikuta kuliko kuriski loosing, wakijua hawawezi kuwashinda, watatumia formular ya 'if you can't beat them, join them' watajiunga nao na wote wakuwa kwenye tenga moja la samaki, na wote watakuwa ndio wale wale.
Hata baada ya Sumaye ku loose, hayo mazungumzo na Chadema ni kiwewe tuu cha hasira za kushindwa!, akishatulia, atayakubali matokeo ya "if you can't beat them, join them"!, watajoin forces tayari kulinda status quo yao for 2015!.

P.
 
mkuu Pasco umenena vema, sumaye hana impact yoyote si cdm au ccm,ishu hapa ni mzee mamvi ndo habari ya mujini an effect kubwa sana akitoka magamban wanamagamba wahesabu chama chao is no more
Mkuu Ciello, hiyo ilikuwa zamani, kwa sasa he is a gone case, CCM wanasubiri tuu kutap followers wake, then kumtafutia honourable exit way!. Wanam dispose ili kumsafishia Membe!.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Msafiri kiboko (JK), kawaletea bajaji ambazo haziwezi kubeba hata tenga la nyanya ati zitumike kama Ambulance! Yaani akili za kuambiwa ameshindwa kuchanganya na zake!! Huku wilayani kwetu walileta hizo piki piki 4, halafu hakuna hata moja inayotembea.

Nikafanya udadis kujua kama watumiaji(wananchi na watoa huduma sipitali) kama wanazikubali, woote wanapinga hizo bajaji. Kali nilipouliza bei yake, nikaambiwa ni @18 million!! Uhuru=kazi ya TANU, Ufisadi= kazi ya CCM
 
Hayo ndio mambo ya CCM ila mambo kama haya yanatakiwa yasemwe tuu bila kutaja majina!. Hili la kutaja mpaka na majina ndilo limemcost Godbles Lema kupoteza ubunge wake pale Arusha, baada ya kumwaga hadharani, jinsi jamaa anavyo washughulikia hawa kina mama wa CC!.
Ha ha ha ha ha h h kumbe Lema alichana LIVE bila chenga, mmm mamvi noma, sasa makanisani anafataga nini!! Lol
 
Kamwe Sumaye hawezi kuondoka CCM viongozi wengi waandamizi walio madarakani na wastaafu wanang'ang'ania kubaki CCM sio kwa sababu wanaipenda sana hapana ni kwa kuwa wanajua wakiondoka maslahi yao yatakuwa hatarini na pia maovu waliyoyatenda wakiwa madarakani yatawekwa wazi!

Mfano mzuri Nimrod Mkono alichimba mkwara kuwa jina lake lilikikatwa patachimbika, Limekatwa na kaambiwa kama anataka kuondoka njia nyeupe, ameondoka? Si amegeuka na kusema anakubali matokeo na hakuwahi kutishia chama?

Wengi wa viongozi ni sawa na Mkono, hata huyu Sitta anayepiga makelele ni kutisha tu hana lolote!

Sumaye hawezi kuondoka ccm,vinginevyo atakuwa amenunua kesi na TRA kwenye vitega uchumi vyake vyote na marupurupu yake ya uwaziri mkuu watasitisha kwa nguvu!
 
Huyo Sumaye anazeeka vibaya.

Nakumbuka siku ameteuliwa waziri mkuu macho yalikuwa mekundu mapepe kibao haamini mahco yake. Leo amejiona na yeye anafaa kuwa rais pamoja na kumwagwa mwaka 2005.

Mwenyekiti alishawaambia waondoke wajiondoe wenyewe mapema lakini wengine kama hawa wenye uchu wa madaraka wanasubiri kwanza wapigwe chini ndio watafute pakushika!
 
Back
Top Bottom