Alama/ logo ya Nyoka katika fimbo kwenye mambo ya afya ina maana gani?

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
Naomba kufahamishwa kwa nini katika nembo za kada za afya(sina hakika kama ni zote) zina nyoka.Nyoka ni alama ya nini,anawakilisha nini na kwa nini nyoka isiwe chura au binadamu.Nakumbuka katika nembo ya pharmacy kuna nyoka na hata katika nembo ya Muhimbili kuna nyoka pia si chuo si hospitali.
Naomba kuelimishwa tafadhari.
1587982687564.png

1587982705583.png

1587982718484.png
 
yule sio nyoka, ila ni mnyoo.
Mnyoo huo hupatikana Guinea,
anaitwa Dracuncula.
Mnyoo huyu akikuingia mguuni, hana dawa, huwezi kumuua.
Kumtoa ni shughuli pevu.

....Na mimi niliwahi kuelezwa hivyo kuwa ni Drancuculus Medinensis, ambaye huishi kwenye maeneo yenye maji, na huambikiza kupitia mayai yake ambapo baadae mnyoo huo hutotolewa na kukaa chini ya ngozi , mara nyingi hushambulia miguu. Hufanya kidonda na kumtoa watu hutumia kijiti, kumviringisha mnyoo ktk kijiti na kumvutia nje, kama anavyoonekana kwenye nembo ya Muhimbili.But, wapo wenye mawazo tofauti kuwa nyoka amekuwa akitjwa katika simulizi za kale kama kiumbe ambae alikuwa akisaidia katika tiba......
 
yule sio nyoka, ila ni mnyoo.
Mnyoo huo hupatikana Guinea,
anaitwa Dracuncula.
Mnyoo huyu akikuingia mguuni, hana dawa, huwezi kumuua.
Kumtoa ni shughuli pevu.

Nimeongea na mfamasia mmoja hapa ametoa maelezo yafuatayo.
1. Nyoka anamaanisha kwamba dawa ni sumu japo ukiitumia vizuri zitakutibu
2. Pia anasema kuwa watu wa zamani walikuwa wakiamini kuwa kama mate ya nyoka yakitumika vizuri yanaweza kuwa dawa, hivyo inaaminika kuwa nyoka ni miongoni mwa vitu vya kwanza kufanyiwa uchunguzi katika jitihada za kugundua dawa mpya
3. Alama ya nyoka inaashiria uangalifu kwa mtumiaji wa dawa, mtumiaji wa dawa anapaswa kuwa muangalifu.

Ofcourse, nimaelezo mazuri lakini sidhani kama yanaelezea kila kitu.Lets say yes kwa pharmacy,tunasema nini kwa kada zingine za afya.

Ingawa sihitaji kubishana, lakini ile picha katika nembo ya muhimbili naamini ni nyoka, unless huyo mnyoo anafanana sana na nyoka. Lets say huyo mnyoo unaemsema ndiye aliyopo katika nembo ya muhimbili, bado swali litabaki pale pale anaashiria nini na kwa nini awekwe yeye.
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo. nafikiri Nyoka inaonyesha kuwa alama ya uponyaji kutokana na Torati Ya Musa wakati wana Israel walipomuasi Mungu safarini jangwani. Mungu aliwatumia nyoka wadogo wadogo wenye sumu wakawa wanawauma Waisrael na kufa.

Musa Akawaombea kwa Mwenyezi ambaye kwa kutaka waonyeshe imani Aliwashushia Nyoka wa mfano aliyetungikwa juu na kuwaamuru kuwa mtu yeyote ili aokoke na wale nyoka wadogo wenyesumu basi atazame yule nyoka mkubwa aliyetundikwa. Kwa wale waliokuwa na imani waliokoka kwa kumtazama yule nyoka aliyetundikwa mtini.

Kwa hivyo ukiweza kufuata huo mfano wa nyoka kwenye vituo vya afya utapona. Nyoka ni symbol tu ya uponyaji kufuatana na maandiko hayo ya torati
 
Nimeongea na mfamasia mmoja hapa ametoa maelezo yafuatayo.
1.Nyoka anamaanisha kwamba dawa ni sumu japo ukiitumia vizuri zitakutibu
2.Pia anasema kuwa watu wa zamani walikuwa wakiamini kuwa kama mate ya nyoka yakitumika vizuri yanaweza kuwa dawa,hivyo inaaminika kuwa nyoka ni miongoni mwa vitu vya kwanza kufanyiwa uchunguzi katika jitihada za kugundua dawa mpya
3.Alama ya nyoka inaashiria uangalifu kwa mtumiaji wa dawa,mtumiaji wa dawa anapaswa kuwa muangalifu.

Ofcourse,nimaelezo mazuri lakini sidhani kama yanaelezea kila kitu.Lets say yes kwa pharmacy,tunasema nini kwa kada zingine za afya.

Ingawa sihitaji kubishana,lakini ile picha katika nembo ya muhimbili naamini ni nyoka,unless huyo mnyoo anafanana sana na nyoka.Lets say huyo mnyoo unaemsema ndiye aliyopo katika nembo ya muhimbili,bado swali litabaki pale pale anaashiria nini,na kwa nini awekwe yeye.

Njoo kwenye point yako ili tujadili vizuri, inaonekana kuna kitu umekisia na hauna uhakika nacho kwa hiyo jibu lolote litakalotoka hapa bila kugusa hicho kitu hauwezi kuridhika nalo

Just be open na tupo ukijuacho au ulichokisia kuhusu nyoka na mambo ya tiba au na imani yoyote
 
njoo kwenye point yako ili tujadili vizuri, inaonekana kuna kitu umekisia na hauna uhakika nacho kwa hiyo jibu lolote litakalotoka hapa bila kugusa hicho kitu hauwezi kuridhika nalo
just be open na tupo ukijuacho au ulichokisia kuhusu nyoka na mambo ya tiba au na imani yoyote

Wengi tunafahamu ubaya wa nyoka. Kwa mtazamo wangu, nyoka anapotumika kama nembo katika sehemu yoyote, si ishara nzuri. Hii inanifanya niamini kwamba ile nembo ya Muhimbili haina alama ya nyoka bali ni mnyoo.

Nyoka pia katika swala la imani ni ishara ya shetani. Nani akubali kuweka 'shetani' katika nembo au kazi yake ikiwa si mtu wa shetani??

Hebu tuchunguze ambapo alama hizi zinatumika... wanashughulika na nini?? Kupiga ramli..., nk
 
njoo kwenye point yako ili tujadili vizuri, inaonekana kuna kitu umekisia na hauna uhakika nacho kwa hiyo jibu lolote litakalotoka hapa bila kugusa hicho kitu hauwezi kuridhika nalo
just be open na tupo ukijuacho au ulichokisia kuhusu nyoka na mambo ya tiba au na imani yoyote

To be honest sijasikia chochote na wala sihitaji kusikia chochote ili kuridhika, ninacho amini mimi, ni lazima palikuwa na sababu ya hao walioweka alama ya nyoka katika nembo kufanya hivyo walivyofanya.

Pia naamini hiyo sababu itakuwa na historia fulani kama alivyojaribu kuelezea muheshimiwa hapo juu. Sasa nachojaribu kuomba kueleweshwa hapa ni mahusiano ya nyoka na tiba ila pia nisingependa kukaririshwa.

Na sidhani kama maelezo yale yale yanaweza kuelezea uwepo wa nyoka katika nembo ya Muhimbili pia yakafafanua uwepowa nyoka katika nembo ya pharmacy.

Kuna mtu aliniuliza nikakosa jibu nami nimekuja hapa kisimani mnieleweshe.
 
Katibukata,

Unajua umenikumbusha, hata matunge anatumia alama ya nyoka. Ninavyojua mimi Matunge hapigi ramli. Unaweza ukagesi ni kwa nini na yeye aliamua kutumia nyoka na si kingine.
 
Huyo nyoka na fimbo vina malelezo tofauti kama ukiongea na watu tofauti. Naambatanisha maelezo ambayo yanakubalika na wengi. Nimeyaacha kwa kiingereza ili nisopotoshe maana hapa chini.

The rod of Asclepius (sometimes also spelled Asklepios or Aesculapius), also known as the asklepian, is an ancient symbol associated with astrology, the Greek god Asclepius and with healing. It consists of a serpent entwined around a staff. The name of the symbol derives from its early and widespread association with Asclepius, the son of Apollo, who was a practitioner of medicine in ancient Greek mythology. His attributes, the snake and the staff, sometimes depicted separately in antiquity, are combined in this symbol. The Rod of Asclepius also represents the constellation Ophiuchus (or Ophiuchus Serpentarius), the thirteenth sign of the sidereal zodiac

The serpent and the staff appear to have been separate symbols that were combined at some point in the development of the Asclepian cult. The significance of the serpent has been interpreted in many ways; sometimes the shedding of skin and renewal is emphasized as symbolizing rejuvenation, while other assessments center on the serpent as a symbol that unites and expresses the dual nature of the work of the physician, who deals with life and death, sickness and health.

The ambiguity of the serpent as a symbol, and the contradictions it is thought to represent, reflect the ambiguity of the use of drugs, which can help or harm, as reflected in the meaning of the term pharmakon, which meant "drug", "medicine" and "poison" in ancient Greek; we know that today antidotes and vaccines are often compounded from precisely the thing that caused the poisoning or illness.

Products deriving from the bodies of snakes were known to have medicinal properties in ancient times, and in ancient Greece, at least some were aware that snake venom that might be fatal if it entered the bloodstream could often be imbibed. Snake venom appears to have been 'prescribed' in some cases as a form of therapy.


Willy
 
Huyo symbol ya nyoka inaonekana sehemu karibu zote zinatoa huduma za afya Hata kwenye logo ya WHO symbol ya nyoka ipo
 
Interesting question Che Kalizozele. I don't remember seeing that symbol; I should be more observant.
 
yule sio nyoka, ila ni mnyoo.
Mnyoo huo hupatikana Guinea,
anaitwa Dracuncula.
Mnyoo huyu akikuingia mguuni, hana dawa, huwezi kumuua.
Kumtoa ni shughuli pevu.

Asante kwa maelezo ya kitaalam,

Unajua haya mabo aliyaanzisha Sheikh Yahya kwenye kipindi chake cha uganga na ulozi channel ten, akaongelea ile michoro ya nyoka huku akitoa tafsiri yake pamoja na majina ya taasisi zinazotumia nembo ile ya nyoka. Sasa hapa tuepuke tafsiri za "kiganga" (kishirikina).
 
Asante Will nakumbuka maelezo kama haya alishawahi kutoa Yahya Hussein yule mtabiri, pia aliwahi kueleza kwa nini kufia za maaskofu na papa zina umbo kama kichwa cha samaki.
 
Naomba kufahamishwa kwa nini katika nembo za kada za afya(sina hakika kama ni zote) zina nyoka.Nyoka ni alama ya nini,anawakilisha nini na kwa nini nyoka isiwe chura au binadamu.Nakumbuka katika nembo ya pharmacy kuna nyoka na hata katika nembo ya Muhimbili kuna nyoka pia si chuo si hospitali.
Naomba kuelimishwa tafadhari.


Huyo ni nyoka si mnyoo.mnyoo kwa umbile lake huwezi kutambua kichwani ni wap mkiani wap.sasa ukitizama kwa makini huyo anaetumika kama alama ya tiba utagundua kichwa na mkia.pia kichwa cha huo unaodaiwa kuwa mnyoo una ulimi ulio waz na umegawanyika kama wa nyoka.

Ukweli ni kwamba huo sio mnyoo bali ni alama maalumu inayomuwakilisha mmoja wa miungu ya kigiriki ya kale aliyeaminika kuwa mungu wa tiba.kumbuka kuwa wagiriki wa kale wana mchongo mkubwa kwenye mambo ya sayansi ya Tiba n.k.

Kwa maana hiyo maneno na nembo nyingi ktk mambo tiba yana asili ya kiyunani na kirumi.hizi nembo za miungu ya kale haziishii tu kwenye mambo ya tiba bali zimetapakaa ktk taasis mbalimbali dunia.mf.Tai anaepatikana ktk nembo mbalimbali za taifa la maarekan pamoja na taasisi zake humuwakilisha mungu wa kipani wa msri ya kale osiris
 
Habari, nimekuwa nikijiuliza maswal juu ya hi logo inayo onesha nyoka amejikunja katka kijiti ama fimbo kwanini inatumia na mambo yahusuyo matibabu ama dawa, nimejaribu pia kuangalia baadh ya hospital za kidin na binafsi zikiwa na nembo hii naomba mwenye kufahamu maana ya hii atufungue macho, natanguliza shukrani kwenu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom