Nelson Mandela; Julius Nyerere and Jakaya Kikwete

mkuu, kichuguu na mlima inaweza kufananishwa.....kichuguu ni kidogo na mlima ni mkubwa.......hiyo hapo juu ni kama ile michezo ya kutoa kitu kisichofanana.....yaani unapewa group lenye vitu vitatu, chumvi, sukari na vocha ya LUKU halafu unaambiwa utoe kitu ambacho hakitakiwi kuwepo kwenye hilo group.

hapo umenena mkuu, yaani huyu JK wa Msando hafananii kabisa, kama zingekuwa hesabu za probability anapata 0.00000000001 aproaches to zero kumfananisha na hawa wazee wetu mahiri.
 
Msando unataka watu wale burn tu hapa JF huwatakii mema kwa thread yako hii.

Unamlinganisha JK ambae hajui kwa nini nchi yake ni masikini na anafurahia bembea ughaibuni huku wananchi wake wanateseka? Nyerere na Mandela their great u cant compare with huyu raisi wenu.
 
Kamanda, hawa watu wote wameshikilia nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi. Kwa nini hawfanani? Mbona wote wamechaguliwa kwa kura kamanda?
 
King nimesoma post yako nimecheka sana! Ngoja tu niwe mkweli, huyu jamaa na Mandela na Nyerere ni kulinganisha Dar na Singida au Rukwa!!

Jana nilikuwa naangalia the Story and Life of Madiba ndipo nikaandika post!! Kwa kweli nilipata hasira sana ingawaje pia nilikuwa nafurahia kuangalia kwa mara nyingine maisha ya Mzee mandela. For some reason ukiangalia unapata sababu ya kureview maisha yako na kujiuliza nini mchango wako katika maisha!!

Nashukuru kwa kunihadharisha nisije nikachangia watu wakla ban humu ndani kwa kuwatia hasira!:laugh:
 
duh, Somoche umeua kabisa!! Lipuli na Man U ni sawa ulinganishe na Liverpool na ZimaniMoto!! Naamini bado unaikumbuka!

Nakubaliana na wewe kwamba huwezi kuwafananisha simply kwa sababu wote wanacheza mpira. Swali la msingi ni wanacheza mpira vipi, wana malengo gani ya kucheza, wanachezea ligi ipi!!

Hapa JK lazima ajiulize sana. Inakuwaje hawa viongozi wengine wanaacha legacy yeye anaacha sijui nini!! :roll:
 
RealMan,

Kutokana na mawazo ya wengi nalazimika kuwaomba radhi waungwana! Kwa mara ya kwanza hata Mwiba amempisha Mkwere!! Niletegemea hata Genius ate thanks na yeye amepisha! DUH! Kweli Mkwere habebeki!! Ngoja nimpotezee!!

Ila naamini kama angekuwa mtu wa kujifunza angejaribu kufuata angalau nyao za hawa wazee kidogo! Sijui siku atakapokabidhi funguo za ikulu atajivunia mafanikio yapi!!
 
toa upupu huu ..huwezi kuziunganisha dot za hao jamaa wawili na kikwete

Heeee! kamanda, Mkwere amekosea wapi? Mbona ameteuliwa kuwa mpatanishi na anashauri viongozi wenzake wakubali matokeo ya kura jamani? Huyu bwana anaelekea kwa kina Mandela na Nyerere! Mpatanishi wa afrika!! Haahahaa!
 
wewe lengo lako ni kuharibu mood za wana jf. Utani huu ungesubiri uutole siku ya tarehe 01.04.2011 ambapo ingeonekana ni siku ya wajinga. Sio leo ,tafadhali sana.

Nasolwa, nimekoma. Huyu jamaa ukijaribu kumbeba nimegundua utajikuta unalazimika kuingia nyumbani saa kumi jioni maana raia wanaweza kuchoma moto!!

Kwa kauli moja naondoa jina la Mkwere kwenye hiyo list!! Kuanzia sasa isomeke hivi 'Nelson Mandela, Julius Nyerere na WanaJF!!
 
Ni utoro wa fikra kwa kujisahau au makusudi kumfananisha Kikwete na Mzee Mandela na Mwalimu...hata Hosni amepotoka mwishoni tu lakini alikubalika ndio maana kabaki miaka yote! Kikwete aombe miujiza kumaliza lala salama yake!
 
Kuna watu wa kuwalinganisha jamani, yaani umlinganishe Kikwete na Nyerere, hata yeye mwenyewe akisoma anaweza akaanguka kwa presha! Mhh!
 
Back
Top Bottom