Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,233
Unlike other political posts kama Uwaziri n.k hii post ni ya utendaji. Kama kweli ni mtendaji mzuri kama wengi wanavyodai hapa muda si mrefu tutaanza kuona matunda yake. That said...
NHC ni mojawapo ya Mashirika machache yaliyo past expire date ambayo bado yanatukumbusha siasa za Ujamaa. Sababu hatuko tena kwenye Ujamaa kwa vitendo, basi ni vema tukaachana nalo. Tukijiuliza hili shirika linamnufaisha nani kwa sasa hakuna mwenye jibu...Badala yake warekebishe mfumo mzima wa ujenzi Tanzania. Wafanye haya na mengine...
1. Harakisha Tin Number/ Social Security/National Insurance Number kwa kila raia.
2. Tuweke mfumo mzuri mikopo kwenye Mabenki,
3. Ondoa/Punguza Kodi kwenye malighafi na mashine za Ujenzi,
4. Weka misingi mizuri ya vibali na usimamizi wake kwenye ujenzi,
5. ....
6. ....
Sit back and watch, Wananchi wakijenga nyumba zao wenyewe tena kwa ufanisi.
Huwezi kufanya number mbili kama huna namba 1. Na hilo ndio linatuumiza sana.