NEC yapuliza Kipenga Uchaguzi mdogo Arusha Mjini na Handeni mkoani Tanga

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Wakati naperuzi katika mitandao ya kijamii nimekutana na hii habari ya uchaguzi Mkuu, nimeona nishare pamoja na waja jukwaa.

===========================




wenyekiti-wa-Tume-ya-Taifa-ya-Uchaguzi-Jaji-Mstaafu-Damian-Lubuva-kulia-akizungumza-na-waandishi-wa-habari-hawapo-pichani-750x350.jpg


TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa Majimbo ya Arusha Mjini na Handeni mkoani Tanga na kwamba utakaofanyika Disemba 13, mwaka huu baada ya kuahirishwa kufuatia kufariki kwa wagombea Ubunge katika majimbo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Disemba 6, 2015, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema taratibu zitakazotumika katika uchaguzi huo ni zile zile zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Aidha, amefafanua kwmaba mara baada ya kupiga kura, kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na vyama vyote vya siasa nchini na vilivyoingia kushiriki uchaguzi mkuu na kuridhiwa na Mahakama wapiga kura wanatakiwa kuondoka vituoni na kuendelea na shughuli zao.

"Msimamo wa Tume ni kuwa haujabadilika kama tulivyokubaliana kipindi kile na vyama vya siasa kwamaana huu ndio ulikuwa pia msimamo wa Mahakama kwamba sheria hairuhusu watu kubaki kwenye vituo vya kupigia kura"alifafanua Jaji Lubuva.

"Sijui sasa wanaotaka kubaki wanatafuta nini, kwanza, utawazuia wanapotaka kwenda kupiga kura, sasa tunawaomba tafadhali sana, wananchi wakishapiga kura waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida ili baadae warudi kuangalia matokeo" aliongeza.

Suala la kukaa mita 200
liliibua mvutano wa muda mrefu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka huu, ambapo Msajili wa Vyama Vya siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi, alipokuwa anazungumzia suala hilo alisema si jambo dogo na ni jambo kubwa ambalo lisingechukuliwa kwa busara lingeweza kuleta machafuko.....

Soma zaidi =>
NEC yatangaza Siku ya kufanyika Uchaguzi Arusha Mjini na Handeni mkoani Tanga

 
Back
Top Bottom