Elections 2010 NEC yafuta watu milioni 1.5 daftari la wapigakura

RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,367
1,519
Habari ndiyo hiyo wanaJF, inabidi kuwa makini na hizo kura 1.5 Milioni si haba isije ikawa ndo mchezo ule wa jadi kwa upende fulani.

Source: IPP Media


 
Lakini umeona sababu zilizowekwa 1) wamefariki 2)wamehama vituo 3)Hawakukidhi masharti nk. wasiwasi wangu ni kuwa wamefutwa ndio tuamini lakini kura zao zinaweza kutumiwa. Au siyo Mfaume wa Wafaume. Wanafunzi vyuo vikuu wenyewe hawafiki hata laki mbili.
 
Dua la kuku......! marehemu nao ni wanafuzi wa UDSM?.........tuacheni kufuru kwa ajenda zetu za kisiasa!
 
Lakini umeona sababu zilizowekwa 1) wamefariki 2)wamehama vituo 3)Hawakukidhi masharti nk. wasiwasi wangu ni kuwa wamefutwa ndio tuamini lakini kura zao zinaweza kutumiwa. Au siyo Mfaume wa Wafaume. Wanafunzi vyuo vikuu wenyewe hawafiki hata laki mbili.

UDSM watakuwa mojawapo
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu lazima mkapige kura na msipopiga sio kwa sababu shauri mmezuiwa. Tafuta nauli panda basi kapige kura kituo ulichojiandikisha. Wakenya walipanda ndege na mabasi kurudi kwao kwenda kupiga kura ya Ndio ama La ya Katiba yao. Huo ndio mwamko wa kisiasa, na uzalendo. Acheni kulalama wakati nauli ya kupanda mabasi ni hela ya simu au saluni tu kwa mwezi. Hata kama mnaona hamjatendewa haki, basi pambana ili ile haki yako uipate. Ujasiri umeenda wapi?
 
watanzania wanaongezeka kwa asili mia 2.5-3.o%. katika muda wa miaka 5, ni wazi wapiga kura wangeongezeka, sio kupungua. kwa kawaida ongezeko huwa ni "net", yaani baada ya kutoa walio kufa nk. sasa maelezo ya nec kwamba wapiga kura wamepungua ni moja ya maajabu ya dunia

macinkus
 
2005 NEC ilijaza mamluki sasa wameona watastukiwa wamewatimua.....watu 1.5m ni nusu ya DSM...it does not make sense ata all...we need to merge hii NEC na yule msajili kuwa na taasisi moja....na iwe independent from the executive please....
 
Mimi kinachonipa wasiwasi ni hayo majina yaliyofutwa, tutajuaje kama kweli yamefutwa wakati tume ya uchaguzi siyo huru? Je kwa kuwa nahaki ya kuelezwa na tume, hayo majina nikisema tayari yameshapigiwa kura za urais nitakuwa nakosea? Kama ni kosa basi NEC itahakikishaje kuwa hao waliobaki wote watatapiga? kura
Mimi nahisi kuna mchezo usio wa kizalendo unachezwa na NEC hapa. Ngojeni tusubiri mwisho wake.
 
Habari ndiyo hiyo wanaJF, inabidi kuwa makini na hizo kura 1.5 Milioni si haba isije ikawa ndo mchezo ule wa jadi kwa upende fulani.

Source: IPP Media



Mhhh I really doubt this isije wakawa wamefuta na jina langu :becky::becky::becky:au kama ulivyosema RedDevil isije ikawa ndo mchezo ule wa jadi kwa upande fulani maana wanavyohaha sasa hivi utafikiri wamedondosha pini kwenye chumba chenye giza
 
Muppets in a failed Muppet Show...........and that Kiravu is talking like a politician while he isn't....biggest muppet
 
yalikuwa mangapi, wamefuta 1.5, wameongeza mangapi, je kuna breakdown ya wilaya au mikoa?
taarifa inapatikana wapi?
je waliohama wametoa taarifa kwa utaratibu gani?
 
Back
Top Bottom