NEC yabariki kampeni za Chadema Maswa kusitishwa
Na Joseph Mwendapole
30th October 2010
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imebariki uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga ya kusimamisha kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mkurugenzi wa Nec, Rajab Kiravu, alisema jana kuwa NEC ilipitia kwa makini uamuzi uliochukuliwa na kamati hiyo na imeridhika kuwa hatua iliyochukuliwa ni sahihi.
"Kamati ya Maadili ya kitaifa imeridhika na hatua iliyochukuliwa baada ya kupitia kwa makini mwenendo wa shauri lile hivyo NEC imekubali chama hicho kisifanye kampeni zozote ndani ya jimbo lile," alisema.
Vile vile, Kiravu alisema Nec imepokea rasmi malalamiko ya CCM dhidi ya Chadema kutokana na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Temeke, Dickson Amos, kumkashifu mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa mkutano wa kampeni Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Kiravu alisema ingawa siku zimekwisha NEC itajadili malalamiko hayo ya CCM kwa kina na kisha itatoa majibu kwa chama hicho.
Akizungumzia matokeo ya urais, Kiravu alisema yatakuwa yakitangazwa kwa umma kadri yatakavyokuwa yakiletwa kutoka majimboni na baada ya majimbo yote kuwasilisha matokeo yatajumlishwa na kutangazwa.
CHANZO: NIPASHE