Elections 2010 NEC yabadili matokeo ya Vunjo yasema ilikosea

Na swali lingine la kujiuliza ..Je kwa marekebisho hayo, haiwezi kuathiri namba ya wabunge wa viti maalum? sababu namba yao inatokana na namba ya kura za Ubunge. Kutokana na marekebisho hayo CCM imepoteza zaidi ya kura 6,000 na CDM imeongeza zaidi ya kura 600 za ubunge..!
 
huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote. NEC haikulijua hilo. nakumbuka NEC walisema tena kwa kujiamini kuwa KABLA HATUJATANGAZA MATOKEO TUME INAYAHAKIKI KWANZA japo haikutuambia how lakini ajabu hayo yaliyohakikiwa yamemzidishia mgombea wa CCM kura 6000. kwa nini wasiwajibishwe? kwa nn wasijiuzulu
 
Hawa jamaa ni ZERO Plus! Nadhani Hesabu walikuwa wanaikacha wakizani ukiwa mwanasheria huhitaji hesabu.......

Hakuna jinsi ya KUKWEPA HESABU HAPA DUNIANI LABDA UFE, LAZIMA ITAKUUMBUWA SIKU MOJA. Sasa imewaumbua hawa wazee!

Hivi boss wa Nec lazima awe mwenye profession ya sheria, mbona havina uhusiano?

Hatutaki sasa tunataka Mtu mwenye proffesional ya numbers,statistics and computing to manage uchaguzi.
Mtu mwenye profession hii atasaidia kupush hata electronic voting na ku train watu kuwa na uwezo wa kutumia computa applications za uchaguzi!
Hawa wazee hata MS EXCEL ndo wameiona siku ya kuhesabu kura wakati ipo toka 1985 ungetegemea nini!
Hivi mkurungezi(KIDEVU) naye ana profession gani eti? Huwa namwona akiropokaropoka kama asiyekuwa na profession yoyote!
 
Luteni,

Asante kwa masahihisho. Nafikiri kura halali ni zile baada ya kuondoa kura zilizoharibika, hivyo huenda total kwasasa iko sawa.

Kinachoshangaza, ilikuwaje hakuna chama kilicholalamikia matokeo hayo? Nakala na matokeo vituoni kila chama kinakuwa nazo, inaelekea vyama havikuwa makini kuhakikisha wanajumlisha kura zote toka kwa mawakala wao ili kujiridhisha.

Hapo ni tatizo maana kama kuna udhaifu kama huo, mkurugenzi wa uchaguzi anaweza kutangaza matokeo yake ambayo hayaendani na ukweli vituoni na wahusika wasijue ukweli wake.
Mtanzania

NEC imesema kura halali kwa sasa baada ya marekebisho ni 53,914 hii ina maana baada ya kutoa zilizoharibika lakini ukijumlisha walizopata wagombea wote total ni 55,677 . Huwezi kutangazwa umeshinda kwa kura fulani halafu waseme hawajatoa zilizoharibika it is nonsense.

Kwa maana yako unataka kutuambia zilizoharibika ambazo siyo halali ziongezwe kwa mgombea yupi? does it make sense. Au kwa lugha nyingine the difference 55,677 - 53,914 = 1,763 ziongezwe wapi wakati wao wameshasema kura halali ni 53,914, ina maana hizo 1,763 walizopewa wagombea hazikuwa halali. Wasitake kutufanya hatujui hesabu.
 
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.

Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.

Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano

Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)

Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.

Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.

My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika huwa hazifanikiwi na mara nyingi hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.

Wanajamvi hii tume haifai hata kidogo kwanini isivunjwe iundwe tume huru ya uchaguzi ?.
 
Tunahitaji tume huru iundwe kuchunguza zoezi zima la kuhesabu kura. Tume wamepata wapi mamlaka ya kubadili matokeo waliyokwishatangaza? pengine tunahitaji wahasibu kuwepo ndani ya tume. simple arithmetics wanashindwa. huenda wote walipata F za basic mathematics
 
Kama kawaida tena natena! Tanzania uozo hautuishi jamani hii tume inakula pesa ya watanzania kwa kufanya uozo! tunaishi kwa ubahatishaji tu!:A S angry:
 
Kweli wao CCM wana pesa sisi Chadema tuna Mungu..

Naona ameshaanza kujichanganya bado ya JK pia watakuwa walikosea pia...
 
Mkuu Mtanzania, Swali la Kujiuliza ni nani Aliywashtua NEC kwamba Matokeo waliyotangaza hayakuwa Sahihi? Na Je kama Uchakachuaji huo Ungempa Ushindi jamaa wa CCM je NEC wangekuwa tayari kurekebisha kasoro? Je Nani mwenye Makosa? NEC au Msimamizi wa Uchaguzi?

Je Makosa haya yamefanyika kwenye Majombo mangapi? NEC wakipelekwa majibu sahihi katika majimbo yanayolalamikiwa kama Arumeru Magharibi, Segerea, Kilombero itakuwa tayari kutangaza Takwimu Halisi hata kama hawawezi kutengua Uteuzi wa Mbunge Husika?

Credibility ya NEC Iko wapi?

Mkuu na wewe umepata Phd juzi juzi, au ni kama ya mkuu wa kaya....:smile-big:
 
Mie nadhani tusiende mbali sana kwenye uhuru wa tume. Kwanza tupate watu makini wa kusimamia ukweli. Iwekwe tume ya wasema kweli hata bila uhuru, wengi duniani hawapo huru lakini wanasimamia ukweli. Watu wanaoweza kujumlisha na kutoa waunganishwe kwenye hao wakweli. Tukimaliza hapo twende kupigania uhuru kamili wa tume. "Incremental approach"
 
:A S-smoking: walivuta kubwa:A S-devil1:wakawa hivyo:director:wakatangaza hivi:israel:akashinda huyo:sorry:wakaomba:sleep:tulikuwa tume:director:tumetangaza upya kashinda aliyekuwa:lock1:sasa ivi utna:gossip:aaaah pumbavu huu si ujinga:doh:...........naomba kwa anayeweza kuanzisha mada ya kura za wazi waliomuunga mkono,DOKITA JK na waliomuunga mkono DOCTOR W S.
 
Luteni,

Sidhani kama NEC kwa kufanya masahihisho wametengua matokeo ya uchaguzi. Ila kama tofauti ya hizo kura ingemfanya mtu mwingine na sio Mrema awe mshindi, hapo ndipo pangelikuwa na kazi kubwa.

Mimi sio mwanasheria, lakini nafikiri ingelitokea hivyo NEC wenyewe wangeliweza kwenda mahakamani kuomba itengue matokeo hayo.
Kutengua matokeo maana yake nini, hadi aliyekuwa wa kwanza awe wa pili nafikiri hapana, kubadilisha maksi au kura za mtu kutoka A kwenda B ni kutengua hata kama ataendelea kushikilia nafasi ile ile. Hapa tunaona kama hawajatengua kwa vile kura zilizotenguliwa hazikubadili position ya mtu lakini kisheria wametengua matokeo .
 
Mtanzania

NEC imesema kura halali kwa sasa baada ya marekebisho ni 53,914 hii ina maana baada ya kutoa zilizoharibika lakini ukijumlisha walizopata wagombea wote total ni 55,677 . Huwezi kutangazwa umeshinda kwa kura fulani halafu waseme hawajatoa zilizoharibika it is nonsense.

Kwa maana yako unataka kutuambia zilizoharibika ambazo siyo halali ziongezwe kwa mgombea yupi? does it make sense. Au kwa lugha nyingine the difference 55,677 - 53,914 = 1,763 ziongezwe wapi wakati wao wameshasema kura halali ni 53,914, ina maana hizo 1,763 walizopewa wagombea hazikuwa halali. Wasitake kutufanya hatujui hesabu.

Luteni,

Nilikuwa sijajumlisha hizo kura, lakini kama namba walizopata wagombea ni sahihi basi taarifa nzima ina makosa.

Nakubaliana na wewe kura walizopata wagombea haziwezi kuwa nyingi kuliko kura halali.

Vyombo vyetu vingi haviko makini kabisa kwenye namba na ndio maana hata mikataba inatuletea matatizo.

Inaelekea hili tatizo la kila sehemu, kuanzia NEC, bungeni, vyama vya siasa nk. Ndio maana wajanja wanatumia hizo weaknesses kuchakachua.
 
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.

Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.

Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano

Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)

Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)

Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.

Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.

My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika huwa hazifanikiwi na mara nyingi hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.

source please
 
The first move ni kwa Chadema kutangaza maandamano makubwa kudemand Tume ijiuzulu, na lawyers wake wawasilishe kesi rasmi kama sio Court kuu pekee bali ICC kwa njama na kuharibu uchaguzi na demokrasia na kutishia amani na usalama wa watanzania wote.
 
Back
Top Bottom