NEC ya dharura Dodoma kishindo gani?

Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.

Nahisi atawaeleza nchi imemshida amwage manyanga
 
Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.

jamani nisaidieni sina habari kuna crisis ya kikatiba CCM inayohitaji dharura ila naamini jamaa anaweza tiwa aibu na wenzake waliomsaliti nahisi kama timu haiko ktk stence nzuri
 
Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.

Jk anajua watz hawatafanya lolote na ndio maana anaendelea na ishu zenye msingi kwake na chama tawala. Isasikitisha ila ndivyo tulivyo.
 
kama kweli wewe una elimu ya chuo kikuu utakubaliana nami kwamba GPA haina mahusiano makubwa na mafanikio katika utendaji. Zipo GPA za kweli, za chupi, za kuiba mtihani, za kuchungulia karatasi ya mtihani kwa mtahiniwa mwingine. Ni heri ukapata GPA ya 2.4 lakini ikawa halali. Wangapi wana GPA nzuri lakini wameshindwa pia kuonyesha ufanisi katika maeneo ya kazi zao?
Lakini hawagombei Uraisi wa nchi Mkuu! Watu walionywa wasikimbilie Ikulu hawakuzingatia maana ya maneno yale. Matokeo yake ndiyo haya kuzimia jukwaani!
 
Hakuna jipya litakalojadiliwa pale. Ni ushamba huo, hakuna habari ya katiba ya ccm. Tunajua wanataka kuwatisha wabunge kuhusiana na misimamo yao kwenye mambo yanayolisumbua taifa letu. Tunafahamu pia kuwa hakutakuwa na waandishi wa habari katika kikao hicho. Kwa hiyo yote atakayoyasema nape hatutayaamini.

CCM haina dila wala mwelekeo wa kuikomboa Tanzania katika matatizo yaliyopo.

Umejuaje huo ni unafiki au mjukuu wa shekh Yahya?kosoeni kwa ukweli sio ukiona mada unataka uchangie upate sifa tu.
 
Mkutano huu umeitishwa ili kuwaadabisha wabunge walioonesha kumdharau Rais wao, hata wengine kupendekeza kuwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani nae!!
 
Tatizo kubwa kwa jk kwa sasa si madaktari bali ni uchaguzi wa ccm ambako kuna kampeni ya kumtoa uenyekiti. Anabadili katiba ya ccm ili zoezi hilo liwe gumu. Hayo ya madaktari na wengineo kwa sasa hayana priority kwake
 
mambo magumu kwa JK kwanini asitatue tatizo mmoja hadi jingine kwani sasa ni wakati mgumu kuliko wakati wowote.Lakini mtoto akitaka wembe mpe
 
Kuna viongozi wataotolewa nishai. We subiri utaja niambia.

LABDA si huyu JK tunaemwona ambaye akiri yake inajua yeye ndiye bosi wa watanzania waliompa kura wakati ukweli ni watanzania ndiyo mabosi wake. hivyo kwa mtazamo wake huo ambao unamfanya hajari kitu chochote kinachohusu Watanzania usitegemee lolote
 
Mkutano huu umeitishwa ili kuwaadabisha wabunge walioonesha kumdharau Rais wao, hata wengine kupendekeza kuwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani nae!!

Inawezekana kwani hadi leo hii, Wabunge wa CCM hawapo juu ya chama bali chama kipo juu wa wabunge wa CCM.
 
Ndugu wana JF,
Habari nilizozinasa hivi punde ni kwamba, mheshimiwa Rais Kikwete ameahirisha ghafla ziara yake ya kikazi katika nchi za Nordic (Denmark, Norway, Sweden, Finland) na Uholanzi, ambayo ilitakiwa aianze wiki ijayo. Sababu zilizotolewa na serikali ni kwamba JK ameahirisha ziara hiyo ili kutatua mzozo wa ndani ya chama chake ambao unafukuta sasa, ukizingatia kwamba mwaka huu chama chake kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu...

Kwahiyo raisi anaweza kuahirisha ziara kwaajili ya chama/ kukiwa na emergence issue kwenye chama na hawezi kuhairisha safari/ziara kukiwa na emergence issue inayowagusa watanzania ? (refer mafuriko, mgomo wa madaktari etc)
 
Watu wanakufa mahospitalini bila huduma, yeye anang'ang'ana na katiba ya ccm! Hivi huyu ni rais wa Tanzania au rais wa ccm?

We acha tu ndugu yangu!! Huyu Kikwete anastaajabisha sana. Kuna mgomo wa madaktari nchini kwa wiki mbili sasa ambao unasababisha Watanzania kukosa huduma muhimu ya matibabu na wengine hata kufa, yeye badala ya kuweka kipaumbele katika mgomo huu ili kuumaliza haraka yeye yuko busy na kikao cha magamba!! Sijui kinamshinda nini kama Rais wa nchi kwenda kukutana na Madaktari ili kumaliza mgomo huu. Dr Slaa hakukosea kabisa alipotoa kauli kwamba, "Kumchagua Kikwete katika uchaguzi huu ni janga kubwa kwa Taifa letu."
 
Timing mbovu kujadili katiba ya ccm . utafunikwa na mambo ya migomo na katiba ya nchi.

Lakini cha kushangaza kingine kama ni katiba ya CCM kwa nini kiwe dharula kwa nini kisiwe wenye time table na schedule ya mwaka ya mwenyekiti na chama . Je mwenyekti na kikosi kazi chake waanafanya kazi kwa style ya zimamoto. Week by week.
Good observation. Hilo suala la katiba halina udharura wowote, kwa nini ameliitishia NEC ya dharura? Kuna dharura zilizopo, lakini amenyamaza kimya
 
Wanakutana ila hawana jipya, labda kama watajadili walivyochinja nyumbu na nyati kwenye sherehe za CCM 35, na kujadili walivyowatelekeza watu waliowasomba kutoka vijijini.
Tungetarajia watoe hadharani majina ya MAGAMBA lakini hakuna wa kuthubutu wote wanaogopana.
Labda kama wataongelea namna ya kupata mgombea ARUMERU.
 
Jamani kwanini mnaojiita Great thinkers mnapenda kubuni mambo au kuwa wataalamu wa kupiga ramli.

JK na wana CCM wana kikao chao cha dharula na ni vizuri kuwa na subra kupata agenda za kikao chao na sio kupiga ramli kujua wanataka kuongea nini.

Kumbukeni nao ni wasomi na wana mengi sana ya kuzungumza hususan usalama na hali ya nchi yenu, mikakati na maendeleo ya kampeni za ubunge arumeru na uwakilishi uzini na mengi mengineyo.

Wapeni pumzi wajinafasi na chama chaokatika vikao vyao sio kuwabanabana kwa kila kitu.
Kinachokera si kikao chao...... wafanye kikao hata mwaka mzima, the issue ni PRIORITY ya nini kifanyike wakati upi...... KWA MFANO, THE BAD TIMING ALIYOIFANYA ni kuhusu posho za wabunge katika kipindi hiki cha madai ya posho za madaktari
 
Back
Top Bottom