Elections 2010 NEC/wasimamizi wa majimbo mtiini mungu

Lusambara

Member
Oct 31, 2010
38
9
Kwa kweli si jambo la kufurahisha, kazi imefanyika kwa AMANI harafu hawa jamaa wanataka kuanzisha fujo. Nina maswali machache hapa wana JF tujiulize.

1- Nini maana yake kila kituo kubandika matokeo ya kura zilizopigwa? Mimi ninavyojua, hata kabla ya wao kutoa matokeo rasmi, tayari umma unajua nani kapita kwa kukusanya matokeo toka vituo vyote. Kazi ya Msimamizi ni kuziweka pamoja ili kupata matokeo ya JUMLA TU.

2- Kila chama cha siasa kina wakala anayeaminika, nini maana yake kugomea kusaini matokeo? Ina maana hukiamini chama ambacho kimekuwekea Wakala? Msajili wa vyama alisema, " Hakikisheni munaweka mawakala ambao ni bora na muwaamini, na nyinyi wananchi mrudi nyumbani kwani wao muliowaweka watasimamia ipasavyo" tumewaweka na tumewaamini sasa mbona HAWATUPI RAHA ZETU JAMANI?

3- Mh. L. Makame alisema " MATOKEO YATATANGAZWA HATA KAMA MGOMBEA ATAKAA KUKUBALIANA NA MATOKEO HAYO" Ina maana alikusudia MKUKI UWE UPINZANI TU? Ninavyoaamini mimi ni kwamba kama ingekuwa upinzani unagoma, matokeo yagetangazwa mara moja. NASEMA TENA WASIMAMIZI NA NEC MUONGOPENI MUNGU. TAIFA NA KILA MMOJA AMEMLILIA MUNGU ILI IWEPO AMANI, MACHOZI YETU MUNGU AMESIKIA MSILETE YA KWENU.

LAKINI kumbukeni RAIS WETU, DR SLAA ALISEMA WAKATI WA MDAHALO " Kama fujo zitatokea basi wenye kuzisababisha itakuwa ni CCM kwani ndio wenye dola" Alitabiri hivyo na sasa inaweza kuwa hivyo.

Kila Mmoja alipo amuombe Mungu, ili asiwepo wa kuwaza tofauti na NGUVU YA UMMA ILIYOAMUA IWE HIVYO.
 
Back
Top Bottom