Elections 2010 NEC: Unganisheni RATIBA yenu na ya mama Salma

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Hii ni mara ya pili Mama Salma Kikwete anaingilia mikutano(msafara) wa mgombea urais wa Chadema Dr. Slaa.

Mara ya kwanza ni wakati ratiba ya mikutano ya Slaa ilikuwa inaonyesha angekuwa Mbulu mjini siku hiyo karibu vurugu zitokee kwa kugombea uwanja. Safari hii makundi hayo yote yamekutana mkoani Mara sehemu ya Mwibara. Mara ya tatu nafikiri ngumi zinaweza kutokea.

Je ina maana Mama Kikwete hana ratiba ya mikutano iliyotolewa na NEC, kama anayo kwanini amepanga kila unapokuwa msafara wa Slaa na yeye yupo. Ni nani basi anayeingilia ratiba ya mwingine, nasema hivi kwa sababu kuna siku fujo zinaweza kutokea kama ilivyokuwa Mbulu mjini.

Kama ratiba ya NEC inajulikana na Tanzania ni kubwa kwanini basi makundi hayo yasipangwe sehemu tofauti. Kama haiwezekani kuyatofautisha naomba NEC iingize ratiba ya safari za Salma kwenye ratiba yao ya kampeni za vyama na WAMA kiwe kama chama cha siasa ili kuepusha mwingiliano na vyama vingine, wakati mwingine inakera.
 
Huu ni uchokozi wa wazi dhidi ya Dr. Slaa na kampeni zake halali..tired with this country..yaani kila kitu ni shagalabagala, hatuna utaratibu unaoeleweka hata siku moja ijayo kwa Mungu. NEC imekuwa teaser bull!
 
Wanaheria wa Chadema fanyeni hima kumburuta mahakamani huyu illeterate!!!!!!!!

Kabla hawjaleta mambo ya keny..
 
Tunaweza kusema hii ni choko choko au kuna kitu kinatafutwa (an accident waiting to happen) ili kiwe breaking point ya kutafuta huruma kwa watu wait and see.
 
Kaka wanatafuta sababu hao, wafanywe mbaya walala mike, JANA SI UMEONA TBC WANASEMA CHADEMA WANAFANYA FUJO!
Ndio naona wanatafuta sababu ya kumzui Slaa asigombe , kwani vurugu zikitokea ndio hivyo tena mtu kuumizwa, maana mama anatembea na mabodo gadi, wapo tayari kurusha lisasi (risasi) au kuwaonyesha kwamba Chadema ni watu wa fujo.
Hivyo ni vizuri chadema wakaliweka wazi hii kitu kwa wananchi na hiyo Shingo (NEC)
 
Back
Top Bottom