NEC: Tutamtangaza mshindi halali Igunga

charity beggins at home, sidhani kama watakuwa wazalendo wakawa fair katika kutangaza
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemtaka Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Protas Magayane, kuhakikisha anatangaza matokeo halisi ya uchaguzi huo bila kuingiliwa, kushurutishwa wala kutishwa na chama cha siasa, taasisi au mtu yeyote mwenye mamlaka ya juu serikalini ili kuepusha machafuko.

Mwenyekiti wa muda wa NEC, Profesa Amon Chaligha, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba wangependa kuona hali ya amani inaendelea kuwepo jimboni humo hata baada ya uchaguzi na namna pekee ya kuidumisha ni kutangaza matokeo sahihi na ya kweli.



Angalau wamegundua kuwa kutotangaza matokeo halali kunaleta machafuko na kuvuruga amani.

Kama anamaanisha anachokisema then we're safe! If otherwise then there are two things involved. Watu wa igunga hawatakuwa na mwakilish wanayemtaka na wakaikubali hali hiyo au wakaikataa. Wakiikubali we're safe!

Wakiikataa, there are two things involved. Wataingia mtaani kupinga matokeo na kuilaani tume au watakaa kimya. Wakikaa kimya we're safe.

Wakiingia mtaani, only one thing involved. Machafuko yatatotea na watu watakufa. This is for real and they've to take care!


Angalizo langu si tu kutangaza matokeo halali, bali kuyatangaza kwa wakati muafaka. Swala la kuchelewesha matokeo hasa maeneo uliposhinda upinzani imeonesha kuwa inaamsha hasira za wananchi na kusababisha amani kuvunjika. Mawakala wanajumlisha kura zao kwenye vituo, then kwenye kata na hatimae jimbo. Mapema wanakuwa wameshajua matokeo ya jumla. Tume inashindwa nini kufanya hivyo na kutangaza matokeo mapema?

Nawaomba sana wazingatie hilo ili kuepusha vurugu.
 
Back
Top Bottom