Elections 2010 NEC na Uswahiliswahili wake

mchillo

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
500
224
Jana Taifa letu lilipitia hatua muhimu kabisa ambapo wananchi walifanya maamuzi ya kuchagua viongozi wao. Kuna mambo kadhaa yaliyonikera na yote yanatokana na utendaji mbovu wa Tume ya uchaguzi ambayo licha ya kusheheni watu kibao wanafanya mambo yao ki uswahiliswahili.
Hebu fikiria, tume iliyodumu kwa miaka zaidi ya 15 sasa imeshindwa kabisa kuandaa utaratibu ambapo kila Mtanzania angeweza kupigia kura popote ili kukamilisha haki yake ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa? Ni wananchi wangapi wameipoteza haki yao kwa kutokuwepo walikoandikishia kupiga kura kutokana na dharura za kibinadamu? Hukumu yao ni kunyimwa haki yao ya kuchagua kiongozi wampendae? Hivi nchi kama Mozambiki, Zimbabwe, hata Burundi na Rwanda wanatuzidi nini hadi wenzetu wawe na uwezo wa kupigia kura popote (Hata nje ya nchi yao)? Ni kweli kabisa timu nzima ya NEC imeshindwa ku-establish data base ya wapiga kura wote itakayotumika kuwathibitisha wapiga kura halali?
Pili ni uzembe katika zoezi zima la upigaji kura ambapo idadi kubwa kabisa ya wapiga kura halali walikosa kutumia haki hiyo kwa kukosa kuyaona majina yao.
Kama kwamba hilo halitoshi, kero nyingine inayoweza kuhatarisha amani ni ile ya kuchelewesha kwa makusudi matokeo. Hivi inachukua masaa mangapi kuhesabu kura elfu sitini hata laki mbili na kuyaweka "Kwenye Kompyuta"?
Tumeshuhudia ucheleweshaji wa namna hii (Uchakachuaji?) kule Arusha, Mwanza, Ujiji, Kigoma mjini, Ubungo, Shinyanga mjini na karibu kila mahali.
Wakati umefika sasa wa wananchi kudai tume huru na siyo hii ya kuteuliwa na kina vikwete na CCM yao ambayo kama ikiachwa kuendelea italeta maafa makubwa siku moja.
 
Sasa wameanza kutangaza kuwa eti matokeo ya uraisi yatakamilika kuanzia Ijumaa na kuendelea. Jamani hii inakatisha tamaa sana maani hii tume inaonekana inataka kufanya ukiukaji wa haki hadharani kabisa. Hili linahitaji kukemewa kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom