Elections 2010 NEC na usalama wa kura zetu

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
NEC imetangaza mikakati ya kulinda kura wakati wa uchaguzi

Mkakati wa kwanza
- Matokeo yatajumlishwa kisayansi majimboni na ya urais yatabandikwa kila yatakapohesabiwa
- Kutakuwa na kituo cha matokeo, ambapo yatajumlishwa kwa uwazi na waandishi wa habari kuruhusiwa kushuhudia.

Mkakati wa pili
Kuhusu tetesi kuwa kuna masanduku ya kura yametengenezwa na kuhifadhiwa katika maeneo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ):

NEC imesema: Kwenye kila sanduku la kura kutakuwa na namba kulingana na namba ya jimbo. Kama kuna watu wametengeneza masanduku ya kura watakuwa wamejisumbua, kwani hayatatumiwa; masanduku ya Tume yatakuwa na namba maalumu kulingana na jimbo husika.

Mkakati wa tatu
Ingawa sheria inaitaka Tume kuwasilisha Daftari kwenye vituo siku nane kabla ya uchaguzi, lakini mwisho wa mwezi huu watavipelekea vyama vya siasa Daftari hilo, ili kupunguza malalamiko ya wapiga kura kutoona majina yao kwenye Daftari la wapiga kura.

Mkakati wa nne
Karatasi za kura zimechapishwa uingereza na si nchini kama inavyosikika, picha na majina ya wagombea yataandikwa kwa kufuata alfabeti na yataanza na chama chenye herufi ya A na kuendelea, mpango ambao umewekwa kuwarahisishia wasioona.

Kwa maana hiyo majina na picha za wagombea urais na vyama vyao vitakuwa katika mpangilio ufuatao:
1: APPT-Maendeleo; Peter Mziray
2: CCM; Jakaya Kikwete
3: CHADEMA; Dk. Willibrod Slaa
4: CUF; Profesa Ibrahim Lipumba
5: NCCR-Mageuzi; Hashim Rungwe
6: TLP; Mutamwega Mugahywa
7: UPDP; Fahmi Dovutwa
 
Nafikiri NEC wamesahau au wamefanya makusudi kutosema je nani atahakikisha usalama wa kura baada ya wao kuzikusanya hadi kutangazwa matokeo ya jumla.
 
Nafikiri NEC wamesahau au wamefanya makusudi kutosema je nani atahakikisha usalama wa kura baada ya wao kuzikusanya hadi kutangazwa matokeo ya jumla.

kila wakati wa uchaguzi kukusanya na kufanya majumuisho ya mwisho NEC huiachia ccm ndiyo ifanye.
 
Nafikiri NEC wamesahau au wamefanya makusudi kutosema je nani atahakikisha usalama wa kura baada ya wao kuzikusanya hadi kutangazwa matokeo ya jumla.

si wamesema zitahesabiwa mbele ya waandishi wa habari!!
 
NEC imetangaza mikakati ya kulinda kura wakati wa uchaguzi

Mkakati wa kwanza
- Matokeo yatajumlishwa kisayansi majimboni na ya urais yatabandikwa kila yatakapohesabiwa
- Kutakuwa na kituo cha matokeo, ambapo yatajumlishwa kwa uwazi na waandishi wa habari kuruhusiwa kushuhudia.

matokeo kujumlishwa kisayansi ndio vipi?.....naomba ufafanuzi
 
Nafikiri NEC wamesahau au wamefanya makusudi kutosema je nani atahakikisha usalama wa kura baada ya wao kuzikusanya hadi kutangazwa matokeo ya jumla.

Tuombe "ulinzi usioonekana" toka kwa Sheikh Yahya! Shida yote ya nini?
 
Nafikiri NEC wamesahau au wamefanya makusudi kutosema je nani atahakikisha usalama wa kura baada ya wao kuzikusanya hadi kutangazwa matokeo ya jumla.

Hapo kuna mianya miwili ya wizi wa kura:

(1) Kuna uwezekano wa kuweka "kura" zaidi kwenye masanduku wakati yakisafirishwa toka kituo cha kupiga kura hadi kituo cha matokeo.

(2) Bado kunaweza kuweko vituo feki vya kupigia kura. Masanduku yake yanaletwa kwenye kituo cha matokeo.

Katika uchaguzi uliopita, nilisikia kuna masanduku mengine hayakufikishwa kwenye vituo vya matokeo mpaka asubuhi kesho yake. Inatakiwa wananchi wakishapiga kura waweze kulitazama hilo sanduku hadi kura zenyewe zihesabiwe.

Kwanini kura zisihesabiwe pale pale kwenye kituo cha kupigia kura, na idadi yake ndiyo ipelekwe kwenye kituo cha matokeo?
 
Miye natabiri mwaka huu chama filisi cha mafisadi kitafanya wizi mkubwa wa kura ambao hatujawahi kuuona tangu tuingie katika chaguzi za vyama vingi. Na hili likitokea basi CHADEMA na CUF wayakatae kabisa matokeo hayo ya wizi utakaoshirikisha vyombo vya dola. CHADEMA na CUF inabidi wawe macho sana katika zoezi lote la kuzihifadhi kura mara baada ya kumalizika upigwaji kura na katika zoezi la kuhesabu kura.
 
hata wasemeje... mimi siamini kama CCM hawataiba kura - kwa mwendo unavyokwenda hali si hali, wapinzani wamekua stonger kuliko miaka ya nyuma
 
Back
Top Bottom