Ndugu wanaJF kuna tetesi kwamba NEC kwa kushirikiana na CCM wamebuni njia ya kuchakachukua matokeo (vote riging) kwa kutopeleka vifaa vya kutosha vya kupigia kura kwenye majimbo yote ambao upinzani unakubalika (strongholds). Usalama wa Taifa tayari umewakilisha majina ya majimbo ambayo CCM haikubaliki kwa "kikosi kazi" cha CCM (chini ya Makamba) majimbo yote ambayo mgombea wa CCM hakubaliki.
Tayari Makamba ameshapeleka orodha ya majimbo hayo kwa JK, na JK kwa kushirikiana na baadhi wa watendaji wa NEC (Jaji Lewis Makame hajui mpango huo) tayari wameshaandaa mpango huo wa kupelekaka vifaa pungufu vya upigaji kura ila wananchi wengi wa majimbo haya wasipate haki yao ya msingi ya kupiga kura. Tayari viongozi wa CCM wa wilaya wameshapewa maelekezo wawambie wanachama wa CCM wawahi mapema kwenye vituo vya kupigia kura ili wapige kura zao mapema kabla ya karatasi za kupigia hazijamazika.
Mkakati huo unafanana fanana na ule uliofanyika mwaka 1995 jijini DSM na baadhi ya majimbo ya Zanzibar ambapo mpeleka vifaa alipotea na karatasi za kupigia kura kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni wakati vituo tayari vimefungwa ndipo alipofika kituoni kwa kisingizio eti alipotea.
Sina uhakika kama uongozi wa CHADEMA tayari wameshaupata mpango huu. Mimi nimeelezwa na kada mmoja wa CCM wa ngazi ya juu wa wilaya. Ninaomba mtu yeyote aliyepo karibu na uongozi wa CHADEMA awafikishie huu mpango muovu unaondaliwa kutunyang'anya watanzania haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka.
Haki hupiganiwa, Mungu ibariki Tanzania