OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema bado haijapata taarifa rasmi za hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora iliyomng'oa ubunge wa Igunga, Dk Dallaly Peter Kafumu.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Julius Mallaba alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii.
"Hatuwezi kutangaza kuwa jimbo la Igunga liko wazi hadi hapo tutakapopata nakala ya hukumu hiyo, tumezisikia habari za kutenguliwa ubunge wa mbunge huyo kupitia vyombo vya habari," alisema Mallaba.
Alisema tume inaweza kulitangaza jimbo hilo kuwa wazi baada ya kuipata hukumu hiyo.
Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Igunga, kimesema kimeanza kuipitia kwa umakini hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora ili kubaini upungufu uliopo.
Chama hicho ambacho Dk Kafumu alikuwa ni mbunge wake, kimesema kikibainisha upungufu uliomo kwenye hukumu hiyo, kitakata rufaa.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Igunga, Mary Maziku alisema wanawatumia wanasheria wao kuipitia hukumu hiyo.
"Tuna uhakika kwamba tutakata rufaa hivi karibuni baada ya wanasheria wetu kumaliza kuipitia hukumu hii kwa sababu tunataka kuwa na uhakika na uamuzi tutakaouchukua," alisema Maziku aliyekuwa akizungumza kwa njia ya simu.
Maziku alisema, "tukimaliza kuipitia hukumu hii na siku ya kukata rufaa tutawajulisha lakini haitachukua muda mrefu kuanzia sasa."
Kauli hiyo imekuja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye kutangaza uamuzi wa chama hicho kukata rufaa kwa sababu ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali.
Nape alisema chama kimeitafakari hukumu ya kesi hiyo na kujiridhisha kuchukua uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi hiyo.
Hata hivyo jana, Nape alipoulizwa kuhusu maendeleo ya kusudio la kukata rufaa alisema, "bado nawasiliana na wanasheria wa chama, kwa sasa sina taarifa za kukueleza."
Hivi karibuni Jaji Shangali alitoa hukumu iliyotengua ushindi wa Dk Kafumu baada ya kuridhishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.
Dk Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba mwaka jana baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.