Elections 2010 NEC: CHADEMA inaweza kuchukua hatua ya haraka dhidi ya Daily News?

Epa inavyozidi kuwanunua watz, ccm kwa nini muibe rasilimari za taifa ili kuwanunua watz masikini?..........mnapata dhambi kubwa sana......kikwete unabariki haya?
 
Wachukue hatua mara moja. Demokrasia haiwezi kubezwa na wababaishaji wa CCM kupitia serikali yetu. Kinachowaunganisha wote ndani ya CCM ni ulaji tu hakuna lingine. Dr. Slaa anatishia ulaji huo na ndiyo maana watendaji serikalini wamechanganyikiwa vibaya mno....
 
Na mimi nitaenda kuiba, then kama hutalalamika kwamba nimekuibia basi mimi si mwizi..... kama ni hivyo basi sheria na polisi wasingekua na kazi
 
Shule nimeenda na wewe hauko kwenye nafasi ya mahubiri ya elimu.

Kama "Humu watu wanaandika kuhusu kushinda kwa Dr. Slaa kwa sababu wanaona ndo atawafaa kwa Maendeleo yao na Vizazi vyao" basi na huyo Mhariri wa gazeti la serikali anaona vengine kwa maoni yake na ndiyo maana hayo yote yameandikwa kwenye column ya "Maoni ya Mhariri". Tatizo lako liko wapi? Au lazima kila mtu akubaliane na hayo mnayoyaandika na mnayoyaona kwa maoni yenu? Kwanini mtu asiwe na maoni tofauti na nyie?

Wapi umesikia kuwa whistle blower ni sifa ya kuwa kiongozi mzuri?

K,
Kutoa maoni sio mbaya. Tatizo ni forum aliyotumia. Daily News ni mali ya serikali, serikali inayoendeshwa na walipa kodi; walipa kodi wanajumuishwa na wapinzani pia. Sisi issues tulizonazo ni forum aliyotumia. Gazeti au chombo chochote cha serkali kinapaswa kuendeshwa bila biasness maana baada ya uchaguzi chama kitakachoshinda kitaendesha hiyo hiyo serkali.

Mkuu nakushangaa sana, tena ilizingatiwa umetueleza kuwa shule umeenda halafu huoni huu utofauti!!!! Labda tafsiri ya kwenda shule uliyo nayo si sawa na std definition!! uuh?

Ukweli ni kuwa Daily news limechemsha na NEC ilipaswa kulionya maana halipaswi kuwa na upande wowote!!!

Got this?
 
Chadema kulishtaki gazeti

Fredy Azzah na Exuper Kachenje

UONGOZI wa Chadema umefikia uamuzi wa kuishtaki Daily News kwenye Tume ya Uchaguzi (Nec) baada ya gazeti hilo la kila siku la serikali kuandika tahariri inayoeleza kuwa mgombea urais wa chama hicho hatashinda kwenye uchaguzi mkuu.

Katika toleo lake la Alhamisi, gazeti hilo liliandika kwenye tahariri yake likisema "na ukweli ni kwamba Dk Willibrod Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania" huku likitaka magazeti ambayo limedai yanamuunga mkono mgombea huyo kukanukuu msimamo huo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa juu wa Chadema kukutana jana na kujadili kwa kina suala hilo, huku wanasheria wa chama hicho shindani wakifikiria uwezekano wa kufungua kesi mahakamani dhidi ya gazeti hilo la Kiingereza.

Mkurugenzi wa kampeni za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kimefikia uamuzi huo kwa kuwa msimamo wa gazeti hilo la serikali ni uchochezi unaoweza kusababisha umwagaji damu.

"Chama kimekutana kujadili hilo suala na kwa hivyo kwa vyovyote tutapeleka malalamiko Nec na bado mawakili wetu wanaendelea kuangalia uwezekano wa kulifikisha mahakamani," alisema Profesa.

"Katika sheria za kawaida tu ukiachilia mbali sheria hii mpya ya uchaguzi, huu ni uchochezi unaoweza kusababisha mgogoro wa umwagaji damu."

Profesa Baregu, ambaye hakusema lini watalifikisha suala hilo Nec wala muda wa kufungua kesi hiyo, alibainisha kuwa hatua hizo zitachukuliwa mapema iwezekanavyo ili waweze kupata haki yao.

"Tutafanya haraka iwezekanavyo ili tutetee haki ukizingatia kuwa ni kweli hiyo makala (tahariri) imeandikwa na gazeti la serikali inatishia amani, hasa ukizingatia kuwa huu ndiyo msimamo wa gazeti la serikali," alisema Profesa Baregu.

Kikao hicho kilichoazimia kulishughulikia suala hilo kimefanyika wakati Dk Slaa akiwa ameshatoa msimamo wake akisema: "Hii inaonyesha kuwa serikali ina mpango mchafu ndio maana wametumia gazeti la serikali. Lakini nguvu ya Dk Slaa itathibitishwa kwa kushinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Na kwa maana hiyo siku za mhariri zinahesabika."

Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wake wa hadhara mkoani Kilimanjaro ambako pia mwenyekiti Freeman Mbowe alisema: "Tunataka uchaguzi huru na wa haki."

Alisema: "Vyombo vya umma vinatakiwa kutumika kwa ajili ya umma na si CCM. Tumesikitishwa na tahariri hiyo.Tunachotaka ni mhariri achukuliwe hatua haraka kwa sababu hiyo inaonyesha mkakati wa serikali si mzuri kwa wapinzani."

Akiongea na Mwananchi juzi, makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisema Nec itafanyia kazi suala hilo iwapo tu Chadema italalamika kuwa imeathiriwa na kuwasilisha malalamiko hayo kwenye chombo hicho.

"Sijalisoma hilo gazeti, lakini kauli hiyo inauma... inatakiwa walioumizwa walalamike. Wakikaa kimya, sisi hatuwezi kuchukua hatua. Kamati ya maadili ipo; Chadema au Dk Slaa akilalamika, tutawaita wanaolalamikiwa," alisema Jaji Makungu akisistiza: Tupo tayari kupokea malalamiko. Tuna kamati ya maadili, wakicomplain (wakilalamika), tutajadili na kutolea uamuzi.”

Wakati Chadema ikitoa tamko hilo Jukwaa la Wahariri lilikutana jana jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo kwa kina na kueleza kuwa litatoa taarifa yake baadaye.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Absalom Kibanda aliliambia gazeti hili jana akisema: “Tunalitafakari hilo na tutalifanyia kazi na kulitolea msimamo bila kuingilia uhuru wa habari na utendaji wake wa kazi kwa kuzingatia kuwa Daily News ni mwanachama wa Jukwaa letu."

Kibanda alifafanua kuwa jukwaa hilo litaangalia iwapo kuna maeneo katika tahariri hiyo yaliyoingilia masuala ya kitaaluma.
“Tutaangalia kama maoni hayo yamegusa taaluma na kwenda kinyume. Daily News ni gazeti la serikali ni mdomo wa serikali, linapotoa msimamo katika uchaguzi wa rais ambaye ndiye mhariri wake mkuu, lazima lifanyiwe kazi kwa njia iliyo bora,” alisema Kibanda.

"Tunajua maadili ya kazi zipo taasisi zinazosimamia uchaguzi, Nec ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo yoyote ya uchaguzi, katika hilo sisi tutaangalia kama imegusa matokeo ya kura za urais."

"Tunaangalia kama wameingilia matokeo ya urais. Hili ni jambo linahitaji umakini, huwezi kulikalia kimya, lakini litafanyiwa kazi na kukusudia kumuumiza yoyote,” alisisitiza.

Jana Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aligoma kuzungumzia suala hilo akisema: sihusiki nalo. Mimi sio msemaji wa serikali.”


Chanzo: Mwananchi wa leo Jumamosi.
 
K,
Kutoa maoni sio mbaya. Tatizo ni forum aliyotumia. Daily News ni mali ya serikali, serikali inayoendeshwa na walipa kodi; walipa kodi wanajumuishwa na wapinzani pia. Sisi issues tulizonazo ni forum aliyotumia. Gazeti au chombo chochote cha serkali kinapaswa kuendeshwa bila biasness maana baada ya uchaguzi chama kitakachoshinda kitaendesha hiyo hiyo serkali.

Mkuu nakushangaa sana, tena ilizingatiwa umetueleza kuwa shule umeenda halafu huoni huu utofauti!!!! Labda tafsiri ya kwenda shule uliyo nayo si sawa na std definition!! uuh?

Ukweli ni kuwa Daily news limechemsha na NEC ilipaswa kulionya maana halipaswi kuwa na upande wowote!!!

Got this?

Mkuu Nyunyu, sidhani kama atakuelewa hapo
 
Back
Top Bottom