dah, mkuu wa Tetea Tete ameondoka? Aliugua muda mrefu kweli, dah, wacha apumzike tuNdynabo nakutakia mapumsiko ya amani na raha ya milele akuangazie Bwana.Amen.
Ndyanabo ninayemfahamu hakuwa mojawapo ya vyama tajwa hapo juu. RIP Ndyanabo!
Kwa mara ya mwisho nilionana naye mwaka 1996 baada ya yeye kushindwa kumbwaga Rwegasira (CCM) wakati yeye akigombea jimbo la Nkenge linaloongozwa na Mbunge D. Kamala (sijui kama bado linaitwa hivyo) huku yeye marehemu akigombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.
Nimetoa ufafanuzi mdogo huo kumwonesha GT kuwa huyu alikuwa nani, na wengine ambao hawakujua huyu alikuwa nani...
Well, ni Julius Ishengoma Ndyanabo. Mojawapo ya kesi unazoweza kusoma ni hii hapa:Invisible ahsante kwa hiyo tidbit ya political bio ya Marehemu.
Well, ni Julius Ishengoma Ndyanabo. Mojawapo ya kesi unazoweza kusoma ni hii hapa:
Ndyanabo v Attorney General (Civil Appeal No. 64 of 2001) [2002] TZCA 2 (14 February 2002)
Invisible, yani sijui umejuaje nilikuwa nataka kujua matokeo ya hiyo kesi ya Marehemu ambayo John Mnyika ameigusia kijuu juu. Ahsante sana Mkuu, nimetoka kuisoma, yani ni bonge moja la kesi ya haki, uchaguzi, na Katiba. I hope the government wameifuta hiyo sheria maana huwa wanadharau matokea ya kushindwa mahakamani.
Naona tumepoteza kinara wa demokrasia na haki katika Julius Ndyanabo. Alale kwa amani.
WAFIWA POLENI,Well, ni Julius Ishengoma Ndyanabo. Mojawapo ya kesi unazoweza kusoma ni hii hapa:
Ndyanabo v Attorney General (Civil Appeal No. 64 of 2001) [2002] TZCA 2 (14 February 2002)
mwenyezi mungu aliyemuumba wakili julius ndyanabo hatimaye amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana libarikiwe (ayubu 1:21). Amen.
Ninamkumbuka alikuwa jirani yangu pale sinza (karibu na namnani hoteli)
poleni sana mke, watoto, pamoja na ndugu wote ambao msiba huu unawahusu.
Raha ya milele umpe ee mungu muumba, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani. Amen.
Invisible ahsante kwa hiyo tidbit ya political bio ya Marehemu. Apumzike kwa amani, na wafiwa wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu sana na siku zote. Poleni sana.
Unajua Mleta taarifa, Ndugu John Mnyika, hakutaja hata jina la Marehemu. Ndio maana kulikuwa na sababu ya wengine kutaka kujua zaidi, kama mfano kutaka kujua kama ana political profile yeyote, hasa ukizingatia kwamba mleta habari ni kiongozi wa Taifa wa chama cha siasa. Ni hilo tu, na hawa viongozi wajue jinsi ya kutoa public statements. Nakumbuka mapema mwaka huu walipofariki watoto wa Mbunge kwenye ajali Dodoma Kiongozi wa Upinzani Bungeni alitoa ka statement kamoja kako very crummy. Hakakutaja hata ni Mbunge wa wapi kafiwa. Halafu akawashukuru viongozi na Wabunge waliosafiri kwenda eneo la ajali kulinda mali za marehemu!
Ahsante tena kwa kutupa snipets za political profile ya marehemu. Wafiwa poleni sana.
RIP Bro Ndyanabo..... Poleni wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki!!
Bwana alitoa naye ametwaa, Jina Lake lihimidiwe!!
Asante Mwigamba kwa hiyo picha