Ndugu zangu wapendwa nahitaji kujua mpangilio wa kutoa mahari huko Iringa

lutamyo

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
641
159
Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kupata chaguo lilo bora zaidi. Nimepata mchumba anayetoka katika mkoa wa Iringa. Hapo ndo penyewe naomba mwenye kufahamu vizuri juu ya taratibu za utoaji wa mahari huko Iringa, hasa vitu gani vinapaswa kuzingatiwa na mposaji.
 
Sharti uwe na vitu vifuatavyo;
1. Kamba ya katani ilofumwa vizuri na Imara(Ya Kujinyongea)
2. Jembe
3.Gunia la Mahindi na Maharage(Kwa ajili ya kande)
4.Kidumla~cha kunywea ulanzi
5. Koti zito na blanket,na
6. Stuli moja kwa ajili ya kusimamia pale watakapo kujinyonga.
NB: Hivyo ndio vya msingi, pesa sio za muhimu.
 
Baba kaleta mbwa, baba kaleta mbwa
Baba kaleta mbwa, baba kaleta mbwa

We usiseme mbwa, sema mbuzi wa porini
Mwenye nyumba hii ni Mhehe, akikusikia atakufukuza

mkuu hebu wafungashie huo mfugo hao watani zangu mambo yako yatakuwa supaaa dupa!
 
hiyo kazi ya mshenga my dear!kaa nae chini atakueleza .maana mra nyingi washenga huwa ni wale wanaojua taratibu za nyumba/kabila unalotaka kuposa.
 
Back
Top Bottom