Ndugu zangu nimefiwa na baba yangu

.......Ohhh!! Pole sana, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe. R.I.P baba.
 
Pole sana kaka Mungu mwenye enzi awajalie moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha mpito huu
 
Ndugu yenu nimefiwa na baba yangu jana tar. 18/2/2011 muda wa saa 11 jioni kwa habari toka kwa ndugu zangu,
mimi ndugu yenu nipo nje ya TZ, ni vizuri kukaa mbali lkn yanapotokea mambo kama haya inaumiza sn, natamani ningekuwa nyumbani ningewahi mazishi kwani mazazi wangu amefia kijijini kwetu na nimbali na motuary, inaniuma sn kwani sitakuja uona uso wa baba yangu.
Hapa jamvini ni kwetu sote ni vema kupeana habari hizi.
Mungu awabariki sana.
Chamkey.
pole sana.astarehe kwa amani
 
Mkuu Chamkoroma,

Pole sana kwa msiba mzito uloupata na BWANA yu pamoja nawe katika kipindi kizito kama hiki.

Ufikapo Iduo nipelekee salamu zangu Ukweni kwangu.
 
Pole sana ndugu yetu. Muumba aiweke roho ya Marehemu baba yetu mahali pema peponi.
 
Wewe ulimpenda baba yako, bali mungu alimpenda zaidi
aleluya tutaonana,
aleluya tutaonana,
tutaonana mbinguni kwa baba,
aleluya tutaonana
 
Comrade, Pole sana! Mwenyezi mungu akupe subra na stahimili katika wakati huu mzito sana.
Mwenyezi ampunzishe mzee kwa amani.
 
Pole sana ndugu kwa kuondokewa na Baba mzazi, yote ni mapenzi ya Mungu kwani yeye alitoa na sasa ametwaa. Amen
 
Pole sana kaka hii ndo Tanzania huduma za majokofu kama Mgao wa umeme~!
 
Pole sana.
Hiyo juzi ungesema msiba wapi, JF ingekuwakilisha maana JF ni omni present popote na saa zote.
RIP Baba wa Chamkoroma!.
 
Pole sana Ndg yangu na tupo pamoja na jipe moyo Mungu atakupa moyo wa kuvumilia na tumwombe mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu baba yako ikae mahali pema peponi Amen
 
Pole mkuu na jipe moyo! Hapa ndipo tunaona uduni wa huduma ya afya unavyokwaza jamii yetu.
 
R.I.P baba yetu... M'mungu akusamehe na akulaze mahala pema peponi.. amen

Pole rafiki yangu kipenzi CHAMKOROMA, mungu akupe iman katika kipindi hiki
 
Pole sana,Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
 
Back
Top Bottom