Ndugu wapendwa

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wana jf wote na hasa wasimamizi na wakuu wa jukwaa letu hili lenye mafunzo, manufaa,faida na fahari kubwa kwa jamii yetu.

binafsi nimejiunga na jukwaa hili mwaka huu ila nimefurahi sana kuwa mmoja wa wana jf na nimefurahi zaidi kujifunza na kufundisha kupitia jukwaa hili.mara nyingi najiuliza ni kwa nini jukwaa hili halikuwepo siku za ujana wetu?

napenda kuwapongeza wasimamizi wa jukwaa hili kwa umakini na mmefanya kazi yenu kwa uangalifu wa hali ya juu,ni kweli pamoja na kuwa nimejiunga mwaka huu ila nimewahi pigwa ban kama mbili hivi kutokana na mawazo fulani au misimamo fulani ambayo niliiamini,nashukuru kwa hilo na ninaomba muendelee na ukali na umakini huo kwani hii ndio njia pekee inayotujenga na kutufanya kuleta mawazo bora na imara wakati wote.

napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea kwa namna moja au nyingine kwa mwaka wote,na hii maalumu pia kwa wakuu wa jukwaa letu najua nimewaudhi mara kadhaa na mpaka mkanipiga ban kadhaa naomba mnisamehe sana.

nawaahidi kuwa sasa nimekomaa na ninajua maana ya jukwaa letu na mchango wake kwa jamii yetu na ninaahidi kwa mwaka ujao nitakuwa makini na naamini 2011 sitapigwa ban hata moja.

napenda pia kuwaambia kuwa kesho nasafiri kwenda kijijini kwetu marangu sembeti kwa ajili ya sikukuu ya kuzaliwa mwokozi wetu na sikukuu ya mwaka mpya hivyo sitakuwepo hapa mpaka mwakani,nitajitahidi kusoma jf kupitia simu yangu mara zote nikipata nafasi nitachangia ila itakuwa mara chache sana.

mwisho nawatakia wana jamii forum wote sikukuu njema na za furaha sana

ahsanteni tuonane mwakani.
 
iyo nyi wo morang sembeti?....anga ndao?...ke ngiwiye ma ngiche kuirikira....inyi ngikeri ala lamrakana.....karibu sana mochi kanyi
 
hi preta dear nitakuja kukuona tar 27 bana 2mia lugha ya taifa mwe!
 
usijali mpenzi...huyu amenigusa kumoyo kwa sababu ni wa nyumbani....sina zaidi ya hapo....kweli kabisa
 
napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wana jf wote na hasa wasimamizi na wakuu wa jukwaa letu hili lenye mafunzo, manufaa,faida na fahari kubwa kwa jamii yetu.

binafsi nimejiunga na jukwaa hili mwaka huu ila nimefurahi sana kuwa mmoja wa wana jf na nimefurahi zaidi kujifunza na kufundisha kupitia jukwaa hili.mara nyingi najiuliza ni kwa nini jukwaa hili halikuwepo siku za ujana wetu?

napenda kuwapongeza wasimamizi wa jukwaa hili kwa umakini na mmefanya kazi yenu kwa uangalifu wa hali ya juu,ni kweli pamoja na kuwa nimejiunga mwaka huu ila nimewahi pigwa ban kama mbili hivi kutokana na mawazo fulani au misimamo fulani ambayo niliiamini,nashukuru kwa hilo na ninaomba muendelee na ukali na umakini huo kwani hii ndio njia pekee inayotujenga na kutufanya kuleta mawazo bora na imara wakati wote.

napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea kwa namna moja au nyingine kwa mwaka wote,na hii maalumu pia kwa wakuu wa jukwaa letu najua nimewaudhi mara kadhaa na mpaka mkanipiga ban kadhaa naomba mnisamehe sana.

nawaahidi kuwa sasa nimekomaa na ninajua maana ya jukwaa letu na mchango wake kwa jamii yetu na ninaahidi kwa mwaka ujao nitakuwa makini na naamini 2011 sitapigwa ban hata moja.

napenda pia kuwaambia kuwa kesho nasafiri kwenda kijijini kwetu marangu sembeti kwa ajili ya sikukuu ya kuzaliwa mwokozi wetu na sikukuu ya mwaka mpya hivyo sitakuwepo hapa mpaka mwakani,nitajitahidi kusoma jf kupitia simu yangu mara zote nikipata nafasi nitachangia ila itakuwa mara chache sana.

mwisho nawatakia wana jamii forum wote sikukuu njema na za furaha sana

ahsanteni tuonane mwakani.

dah! wewe mtoto wa mkulima kweli aisee, naona mpaka font umeamua kutumia rangi ya mbolea. poa bana, all ze best
 
Preta
Nakupenda sana mdada, nitakuletea zawadi ya matopetope kwenye vacation au nitampa kaka mkubwa PJ on my behalf
 
anaelewa kiingereza? nimehisi bora nitumie forein lengueji kuomba razi ili kuonesha msisitizo wa regret zangu.

braza anapasua mayai mbaya kabisa....ya kuku, mjusi, kenge ,nyoka, kila kitu.....yoteyote....fanya hivyo mpenzi
 
Preta
Nakupenda sana mdada, nitakuletea zawadi ya matopetope kwenye vacation au nitampa kaka mkubwa PJ on my behalf

yum yum....asante sana...usisahau na mastafeli na fenesi.........huwezi amini hiyo ndio itakuwa lunch box
 
braza anapasua mayai mbaya kabisa....ya kuku, mjusi, kenge ,nyoka, kila kitu.....yoteyote....fanya hivyo mpenzi
dah kimeripuka! ilikuwaje ukawa ndugu na huyu jamaa? haiwezekani tukachakachua DNA yako ili msihusiane tena?
 
kila kitu utakachosema nitafanya.... kwako sipindui......honeypie
hata nikikuambia umtukane invizibo? dah! ndio maana nakuitaga selin dion. una mikwala ya mapenzi, si mchezo . senks switihati. tupendane kuliko ugoro na chafya.
 
yum yum....asante sana...usisahau na mastafeli na fenesi.........huwezi amini hiyo ndio itakuwa lunch box
ondoa shaka Preta, ulivyonikaa moyoni kwangu, nitakuletea chochote unachotaka mdada wewe
 
Back
Top Bottom